Service ya kufanya kwa ajili ya masafa marefu

Mkata-tamaa

Senior Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
180
Reaction score
312
Wakuu poleni na pilika za kutafuta tonge la kila siku

Wiki mbili zijazo natarajia kusafiri mimi na familia yangu kwa kutumia usafiri binafsi

safari ni kutoka mbeya kuja Dar

Lengo la kufungua uzi huu ni kuomba ushauri kwenu,ni servise gani hasa natakiwa kufanya ili niweze kusafiri salama na ki ISt changu?

Maana binafsi servise nilizozoea ni zile za kumwaga oil tu na kubadili filter.

Nini nikifanye hasa kwenye gari langu ili kuliweka katika hali salama ya kusafiri nalo?

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Cheki kwanza fan belt kama haijachoka engine oil iwe mpya maji kwenye betri na regetor na mfuta ya brek jeki na tringle angle reflector(huo ni uangalizi wa ndani)kwa nje check stads tyre zako zote kama zimekaza vizuri uwe na tyre spare nzima upepo kwenye tyre mafuta ya kutosha kwenye tank na majibya reserve kwenye kidumu au mle kwenye reserve yake og.
Nyongeza: uwe na angalau kalaki ka emegency njiani wale wa nguo nyeupe same time wanazinguaga sana huko njiani
 
Mimi nasema weka tairi mpya.
Tembea na jeki.
Tembea na spana inayozifungua na kuzifunga vizuri nati zako.

Kuna balaa lilinipata nilisafiri na IST haina jeki, spana, wala tairi la akiba. Nilienda kukwama kijiji fulani hivi nyuma ya Ruaha Mbuyuni na kilometa 15+ baada ya Mikumi. Jina limenitoka.

Ila hapo hakuna netwek siyo ya simu tu hata ya redio. Safari ya kutoka Dar kwenda Mbeya nilitumia siku 2 na nusu badala ya saa 10.
Matairi jambo la msingi sana chief.

PS. Jf inadhalilisha mno wenye baby walker hadi mtu anaandika 'Ki IST changu' badala ya 'IST yangu'

Pia mi sina gari nilikua dereva tu

Update: Eneo linaitwa Iyovi
 
Baada ya kumwaga oil na kubadilisha oil filter inafaa zaidi ukibadilisha air filter.
Pia Fanya wheel alignment (hii ni muhimu mno tena Sana) na kama fan belt imechoka badilisha....
Ukiwa safarini jitahidi kuacha papara za hapa na pale usipende league na akina Subaru au crown utapasua engine yako
 

Umenipa mwanga mzuri sana mkuu
 

Ubarikiwe sana boss

Kwenye matairi kuna suala zima kubalance upepo

Wengine wananiambia upepo wa tairi za mbele uwe mdogo kuliko upepo wa tairi za nyuma ,je kuna ukweli hapa?

Na ni upepo kiasi gani unaotakiwa kwa tairi za mbele na tair za nyuma ni upepo kiasi gani?
 
Hii sio necessary Sana ni concepts Tu kama vipi jaza upepo Kwa Matairi yote Kwa pressure ya 35 Kwa kila tairi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…