Mbeya to Dar ni mbali.....hivyo mwaga engine oil na uweke oil filter genuine...achana na zile za buku 3..
Puliza air filter.
Fanya wheel alignment
Zingatia upepo wa tairi zako 30 psi mbele na nyuma 35. Na tairi zako ziwe nzima.
Hakikisha radiator haivuji..
Beba maji ya akiba angalau Lita 10....SAFARI NI SAFARI
Hakikisha maji ya kuoshea kioo yamejaa kwenye kimtungi chake.
Hakikisha wipers zinafanya kazi vizuri...njiani kunaweza kukawa na mvua baadhi ya maeneo.
Triangle,fire extinguisher, sticker ya bima na sticker ya nenda kwa usalama viwepo up to date.
Hakikisha una spana muhimu kama vile wheel spqnner na plug spanner.....huwezi kujua ni pori lipi utapata pancha au plug itakufa..
Kuwa na angalau spark plugs mbili za spea.
Hakikisha taa zote zinawaka vizuri.
Osha gari lako vizuri liwe na muonekano wake halisi...
HAYO NI MAANDALIZI KABLDA YA SAFARI[emoji115][emoji115]
UKIANZA SAFARI NA UTAKAPOKUWA SAFARINI[emoji116][emoji116][emoji116]
Weka mpango wa muda wa kuondoka, utasimama wapi kupumzika na kula na unatajia kufika saa ngapi
Sali kulingana na imani yako ili Mungu aibariki safari yako.
Hakikisha wote mnafunga mkanda.
Zingatia alama zote za barabarani....vivuko, 50kph na kadhalika.
Kumbuka, safarini kuna magari mengi yanayoelekea uelekeo mmoja ila hamfahamiani....hivyo epuka kufukizana na mtu aliyekupita kwanza hamjui, pili hujui katoka wapi na anaenda wapi, tatu speed yake hujui amelewa au anawahisha mgonjwa, nne kila mtu barabarani ana safari yake hivyo heshimu safari yako.
Acha ligi za kukimbiza magari yenye uwezo kuliko lako mf V8,Subaru na kadhalika.
Usimpe lifti mtu usiyemjua....ni hatqri sana...wanadamu leo hii tumebadilika.
Kuwa makini kukaa umbali angalau wa Mita 50 kutoka gari lililopo mbele yako....hii itakusaidia kujitetea endapo atafunga breki za ghafla.
Usiovertake kwenye blind spot areas....
REMEMBER YOU HAVE THE WHOLE FAMILY WITH YOU.
Kwenye Mpesa uwe na angalau 50k za dharura ya miamala endapo itahitajika na kwenye wallet uwe na angalau 50k ya dharura ya cash endapo itajitokeza.....hii balance ya pesa ni nje y ile bajeti yako ya kula njiani..
Nakutakia safari njema bosi...Ukifika hapo mikumi kuna jamaa yangu atakupa kqmzigo flani, then ukifika Dar kapakie kwenye Dar Express nitakapoke Arusha[emoji41][emoji41][emoji41]