Seti Mbili za Treni ya Umeme na vichwa 8 vya Umeme "Samia Express" vyawasili Nchini

SETI MBILI ZA TRENI ZA EMU (ELECTRIC MULTIPLE UNIT) ZAWASILI

Dar es Salaam, Tarehe 02 Julai, 2024

Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa Seti mbili (2) za treni ya kisasa inayotumia nishati ya umeme EMU (Electric Multiple Unit) na vichwa nane (8) vya treni vya umeme vimewasili Tanzania kutoka nchini Korea ya Kusini.

Serikali kupitia TRC ilifanya manunuzi ya Seti kumi (10) za treni za EMU zinazotengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea Kusini, Seti moja ya EMU ina jumla ya mabehewa nane yakijumuisha kichwa kimoja mbele na kingine nyuma ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 589 na kutembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa.

Seti mbili (2) za EMU zinafikisha idadi ya seti tatu zilizowasili nchini mpaka sasa, seti ya kwanza iliyowasili mwezi Aprili 2024 inaendelea na majaribio.

Shirika la Reli Tanzania limeshapokea jumla ya mabehewa 65 ya abiria, vichwa 17 vya umeme na Seti tatu za EMU. Upokeaji wa vifaa vya uendeshaji vya reli ya kiwango cha SGR unaendelea kwa awamu tofauti, vifaa vipya vilivyowasili vitaendelea kufanyiwa majaribio kwaajili ya kujiridhisha kabla ya kuanza kutoa huduma.

Shirika linaendelea na uendeshaji wa awali na utoaji huduma ya usafiri wa treni za umeme kupitia reli ya kiwango cha kimataifa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, uendeshaji rasmi kati ya Dar es Salaam hadi Dodoma unatarajiwa kuanza Julai 25, 2024.

Jamila Mbarouk Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano

Ukweli ni kwamba.
Naipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha usafiri wa treni.

Ila mafisadi yametuchelewesha sana.
 
Ndio maana watu wamechoka mpaka wanachoma picha ya raisi maisha magumu mtaani hasa kwa vijana ajira hakuna na ukipata ajira mshahara hautoshi gharama za maisha....bora treni zingeitwa trc express na zipewe namba kutofautisha sijawahi kusikia nchi yoyote treni zikipewa majina ya raisi ukizingatia mradi wenyewe tunajenga kwa mkopo na tuta suffer kuzilipa
 
Ndio maana watu hawapendi kulipa kodi, huku mtaani TRA ni kama malaika mtoa roho
 
Wanajaribu kila njia lakini wapi mwamba yupo midomoni mwa watu. Si treni si bwawa la umeme! Mgao wa umeme umeisha kwasababu ya bwawa walilopinga na kumtukana aliekomaa nalo. Hixi treni nazo walisema hazina maana leo wanahangaika kuziita majina yao. Ndege nazo bado wanaendelea kununua vyote hivyo alieanzisha alipondwa sana.
Kati ya makosa makubwa sana aliyofanya Magufuli ni ______.
 
Cijaona nionyeshe
Screenshot_20240703_095916_Firefox.jpg
 
Ila hizi treni ukiziona zikiwa kwenye mwendo Ile nginja nginja yake haina tofauti na zile za TRC na vile zinavyotembea sidhani kama nitakuja kupanda
 
Back
Top Bottom