Seti Mbili za Treni ya Umeme na vichwa 8 vya Umeme "Samia Express" vyawasili Nchini

Nimezoom hapo nimeona SAMIA EXPRESS 🙌

Kweli 2025 is Loading ..........
Alieamua ziitwe Samia Express ni nani, Abdul na Mwigulu? Samia anatafuta kuwaudhi Watanzania, hasa wa bara

Hizi kampeni kuna wakatii zitamrudi Samia zimfanye watu ndio wasimtake kabisa. Aliyefanya hili hakuwaza sawasawa, this is too much
 
Aliyethubutu kuanzisha mradi mkubwa kabisa, aliyethubutu kuziba masikio kusikiliza wapuuzi, aliyeanzisha mega projects...

This man, the one and only!
Wanajaribu kila njia lakini wapi mwamba yupo midomoni mwa watu. Si treni si bwawa la umeme! Mgao wa umeme umeisha kwasababu ya bwawa walilopinga na kumtukana aliekomaa nalo. Hixi treni nazo walisema hazina maana leo wanahangaika kuziita majina yao. Ndege nazo bado wanaendelea kununua vyote hivyo alieanzisha alipondwa sana.
 
Amka ukakojoe dogo
 
izi makitu zote alistahili kupewa jina magufuli. samia hajaanzisha huu mradi, jasho la magufuli hili.
 
Tatizo nini Mbona tuliwahi kuwa na Treni ya Mwakyembe, na sasa haipo na hakuna anayejali. Mjidai hamlioni jina hilo.
 
KAZI INAENDELEA KWA KASI,
SHUKRANI KWA RAIS WETU SAMIA
 
Alieamua ziitwe Samia Express ni nani, Abdul na Mwigulu? Samia anatafuta kuwaudhi Watanzania, hasa wa bara

Hizi kampeni kuna wakatii zitamrudi Samia zimfanye watu ndio wasimtake kabisa. Aliyefanya hili hakuwaza sawasawa, this is too much
Itakuwa washauri wake waliopo Ikulu 🙌

Kuna watu wanaweza kukushauri jambo baya kama mtego wa kukunasa, nawe usipokuwa na hekima kuling'amua hakika utaanguka kweli

Ngoja tuone mwisho wa hili jambo
 
Alieamua ziitwe Samia Express ni nani, Abdul na Mwigulu? Samia anatafuta kuwaudhi Watanzania, hasa wa bara

Hizi kampeni kuna wakatii zitamrudi Samia zimfanye watu ndio wasimtake kabisa. Aliyefanya hili hakuwaza sawasawa, this is too much
Tunasubr CHADEMA mkifurahi na kupga picha safi ndani ya SAMIA EXPRESS
 
Ahsante sana Mama Samia.

Tutaona muda wa kusubiri treni za abiria unapunguwa kila siku zinatokwenda.

Naamini siku za usoni itafikia kila one-hour treni moja inaondoka na nyingine inaingia, za mizigo mbali.

Kuishi Morogoro kufanya kazi Dar itakuwa jambo la kawaida.

Sisi wa kusini tunaisubiri reli ya Dar Mtwara.
 
SETI MBILI ZA TRENI ZA EMU (ELECTRIC MULTIPLE UNIT) ZAWASILI

Dar es Salaam, Tarehe 02 Julai, 2024

Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa Seti mbili (2) za treni ya kisasa inayotumia nishati ya umeme EMU (Electric Multiple Unit) na vichwa nane (8) vya treni vya umeme vimewasili Tanzania kutoka nchini Korea ya Kusini.

Serikali kupitia TRC ilifanya manunuzi ya Seti kumi (10) za treni za EMU zinazotengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea Kusini, Seti moja ya EMU ina jumla ya mabehewa nane yakijumuisha kichwa kimoja mbele na kingine nyuma ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 589 na kutembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa.

Seti mbili (2) za EMU zinafikisha idadi ya seti tatu zilizowasili nchini mpaka sasa, seti ya kwanza iliyowasili mwezi Aprili 2024 inaendelea na majaribio.

Shirika la Reli Tanzania limeshapokea jumla ya mabehewa 65 ya abiria, vichwa 17 vya umeme na Seti tatu za EMU. Upokeaji wa vifaa vya uendeshaji vya reli ya kiwango cha SGR unaendelea kwa awamu tofauti, vifaa vipya vilivyowasili vitaendelea kufanyiwa majaribio kwaajili ya kujiridhisha kabla ya kuanza kutoa huduma.

Shirika linaendelea na uendeshaji wa awali na utoaji huduma ya usafiri wa treni za umeme kupitia reli ya kiwango cha kimataifa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, uendeshaji rasmi kati ya Dar es Salaam hadi Dodoma unatarajiwa kuanza Julai 25, 2024.

Jamila Mbarouk Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano

Kweli Samia express hongera sana kwa kuupiga mwingi
 
Mchongoko haujafika 100%
 
Back
Top Bottom