SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

IMG-20220129-WA0014.jpg

===​

Reli ya SG ikikamilika bila uwepo wa bandari ya uhakika kama Bagamoyo tegemeeni malori mengi kupaki​


SGR ikikamilika inaweza kubeba mizigo yote ya Bandari ya Dar es Salaam kwa siku 250 tu,

Kama SGR itakamilika bila ya Bandari ya Bagamoyo kujengwa basi Malori mengi ya mizigo mnayoyaona hapa nchini yatalazimika kupaki kwa kukosa mizigo,

Iko hivi,treni moja ya mizigo ya SGR inauwezo wa kubeba Jumla ya Tani elfu 10 karibu sawa na Malori 500 kwa Safari moja,

TRC ikiwa na Treni mbili tu za mizigo zinazopishana kwa kila siku basi tutasafirisha Jumla ya Tani elfu 20 kwa siku moja sawa na Malori 1,000.

Nimejaribu kutafuta wastani wa mizigo iliyopakuliwa pale bandari ya Dar es salaam kati ya mwaka 2016|2020 nimepata ni wastani wa Jumla ya Tani milioni tano (5M)

Kwamsiofahamu, 98% ya mizigo yote inayoingia na kutoka Tanzania na nchi jirani inapitia bandari ya Dar es Salaam,

Tujiulize, Kama tani elfu 20 kwa SGR zinaweza kubebwa kwa siku moja kwa kutumia treni mbili za SGR zinazopishana,

Je hizi tani 5M zinazopakuliwa pale bandari ya Dar es salaam kwa mwaka mzima zitabebwa kwa muda gan kwa kutumia hii SGR?

Fanya hivi,gawanya tani 5M kwa tani elfu 20 utapata Jumla ya siku 250 za kuisafirisha mizigo yote ya mwaka mzima ya bandari ya Dar es salaam kwa kutumia SGR,

Mkumbuke kuwa, Safari ya Treni ya Mzigo toka Dar -Mwanza ni wastani wa masaa tisa ( 9 ) wakati Safari ya Lori ni zaidi ya masaa 48,

Lakini pia,bei ya kusafirisha mizigo kwa SGR ni ndogo kuliko ile ya Lori na Usalama wa mzigo kwenye SGR ni mkubwa kuliko ule wa kwenye Lori,

Sikia,Nimfanyabiashara mjinga tu ndio anaweza kuacha kupakia SGR yenye nafasi akapakia mzigo kwenye Lori

Sababu pekee inayoweza kuyanusuru haya Malori yetu ni kuwa na bandari nyingine kubwa itakayokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kushusha mizigo mingi zaidi ya ile ya Dar es salaam ili SGR ibebe na isaze na Malori ya bebe pia,

Kama hili halitafanyika kuna watu wengi mnakwenda kukosa ajira zenu hapo baadae kidogo,

Nadhani hii ni moja ya sababu ya kwanini Rais Samia anataka bandari hii ijengwe tena kwa haraka kabla ya kumalizika kwa SGR,


Mnaolalamika kuhusu Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo rudieni tena kusoma andiko hili kwa makini,
 
Kama kuna kitu umenifungua macho basi ni hii logic,
Kwa hesabu hii ni kweli Malori karibu yote yatapaki

Mungu mbariki Samia wetu,
Ona na wewe unashindwa tafakari, maloli yataendelea kuwepo na kuwepo mizigo ya bandari sio yote inaenda mahali pamoja hapana, MTU anacontena lake linaenda kondoa sgr inafika huko ndio maana hata sasa hivi sio kwamba reli ya kati au tazara zimezidiwa ila wateja wanataka urahisi zaidi na kukimbizana na soko
 
Mizigo inayokuja bandarini dar inakwenda along the central line tu mpaka malori yapaki? Ile inayowenda Zambia, Malawi, Mbeya Iringa, Kilimanjaro Arusha, Tanga Manyara?
Kote huko SGR itafika mkuu wangu,
 
Ona na wewe unashindwa tafakari, maloli yataendelea kuwepo na kuwepo mizigo ya bandari sio yote inaenda mahali pamoja hapana, MTU anacontena lake linaenda kondoa sgr inafika huko ndio maana hata sasa hivi sio kwamba reli ya kati au tazara zimezidiwa ila wateja wanataka urahisi zaidi na kukimbizana na soko
Kama ni Kondoa Reli iko Dodoma, Sio Dar tena ona hio hesabu
 
Bondi mnaweka nn maana isije kua km uganda na je tumejipanga kupunguza mi kodi ya ajabu ili nchi jirani warudi kutumia bandari zetu ...maana tunaweza kujenga hiyo bandari ya bagamoyo harafu sera zikawa mbovu ikawa hasara tu kwetu .Hili swala inatakiwa utulivu sana tukikurupuka itakua km maswala ya gas tuliambiwa kua gas ya mtwara ikiianza kuchimbwa swala la umeme litabaki history je mpaka sasa ina faida gani hata hatujui.
 
Una uhakika baada ya hiyo bandari kufunguliwa hii mizigo inayopitia bandari ya dar itaendelea kupitia hapo?
Hata kama yote itapitia hiyo bandari mpya bado SGR na Malori ni yetu,

Meli baadhi pia ni zetu
 
Umeshajiuliza kuwa reli ya sasa ina uwezo wa kubeba mzigo kiasi gani na ni kiasi gani chamizigo unapita kwenye reli as compared na kile kinachopita kwenye malori?

Kimsingi ulichokifanya ni kama kile kilimo cha matikiti kwenye karatasi.

Uhalisia hauko kama unavyo ongea. Shippers wana prefer malory kuliko train kwa sababu mbalimbali. Google ujielimishe
 
Back
Top Bottom