SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

Bondi mnaweka nn maana isije kua km uganda na je tumejipanga kupunguza mi kodi ya ajabu ili nchi jirani warudi kutumia bandari zetu ...maana tunaweza kujenga hiyo bandari ya bagamoyo harafu sera zikawa mbovu ikawa hasara tu kwetu .Hili swala inatakiwa utulivu sana tukikurupuka itakua km maswala ya gas tuliambiwa kua gas ya mtwara ikiianza kuchimbwa swala la umeme litabaki history je mpaka sasa ina faida gani hata hatujui.
Sijawahi ona huo mkataba mimi ila naamini Rais wetu ni mtu mzalendo Sana,

So let's hope the best
 
Umeshajiuliza kuwa relu ya sasa ina uwezo wa kubeba mzigo kiasi gani na ni kiasi gani chazigo unapita kwenye reli as compared na kile kinachopita kwenye malori?

Kimsingi ulichokifanya ni kama kile kilimo cha matikiti kwenye karatasi.

Uhalisia hauko kama unavuo ongea. Shippers wana prefer malory kuliko train kwa sababu mbalimbali. Google ujielimishe
Kwa Sasa Malori yanabeba mizigo mingi,

Factor, Ni Reli ya Meter gauge haina tofauti sana na Gari,

So they choose either of
 
Mimi sina mkuu kama unao lete tuujadili hapa,

Mimi nimeonesha analysis yangu hali itakuwaje hapo baadae nimeishia hapo,
Basi uwe makini sana

Kama hata wewe huo mkataba hujauona basi uwe makini sana hii nchi ni yetu mkileta uhuni tunawaloga tu mjifie huko
 
Utapiga je Pesa wakati mchina anakusanya mapato yote,pole pole alikuwa sawa tena sana.
Faida ya kusafirisha mizigo ndani na nje ya Tanzania ni kubwa kuliko ile kupakua mizigo,

Wachina watapata nasisi tutapata pia,

Bandari hii mpya itakuwa yapili baada ya ile ya Durban SA,
 
===
SGR ikikamilika inaweza kubeba mizigo yote ya Bandari ya Dar es Salaam kwa siku 250 Tu,

Kama SGR itakamilika bila ya Bandari ya Bagamoyo kujengwa basi Malori yote ya mizigo mnayoyaona hapa nchini yatalazimika kupaki

Iko hivi,treni moja ya mizigo ya SGR inauwezo wa kubeba Jumla ya Tani elfu 10 karibu sawa na Malori 500 kwa Safari moja,

TRC ikiwa na Treni mbili tu za mizigo zinazopishana kwa kila siku basi tutasafirisha Jumla ya Tani elfu 20 kwa siku moja sawa na Malori 1,000.

Nimejaribu kutafuta wastani wa mizigo iliyopakuliwa pale bandari ya Dar es salaam kati ya mwaka 2016|2020 nimepata ni wastani wa Jumla ya Tani milioni tano ( 5M )

Kwamsiofahamu, 98% ya mizigo yote inayoingia na kutoka Tanzania na nchi jirani inapitia bandari ya Dar es Salaam,

Tujiulize, Kama tani elfu 20 kwa SGR zinaweza kubebwa kwa siku moja kwa kutumia treni mbili za SGR zinazopishana,

Je hizi tani 5M zinazopakuliwa pale bandari ya Dar es salaam kwa mwaka mzima zitabebwa kwa muda gan kwa kutumia hii SGR?

Fanya hivi,gawanya tani 5M kwa tani elfu 20 utapata Jumla ya siku 250 za kuisafirisha mizigo yote ya mwaka ya bandari ya Dar es salaam kwa kutumia SGR,

Mkumbuke kuwa, Safari ya Treni ya Mzigo toka Dar -Mwanza ni wastani wa masaa tisa ( 9 ) wakati Safari ya Lori ni zaidi ya masaa 48,

Lakini pia,bei ya kusafirisha mizigo kwa SGR ni ndogo kuliko ile ya Lori na Usalama wa mzigo kwenye SGR ni mkubwa kuliko ule wa kwenye Lori,

Sikia,Nimfanyabiashara mjinga tu ndio anaweza kuacha kupakia SGR yenye nafasi akapakia mzigo kwenye Lori

Sababu pekee inayoweza kuyanusuru haya Malori yetu ni kuwa na bandari nyingine kubwa itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kushusha mizigo mingi zaidi ya ile ya Dar es salaam ili SGR ibebe na isaze na Malori ya bebe pia,

Kama hili halitafanyika kuna watu wengi mnakwenda kukosa ajira zenu hapo baadae kidogo,

Nadhani hii ni moja ya sababu ya kwanini Rais Samia anataka bandari hii ijengwe tena kwa haraka kabla ya kumalizika kwa SGR,


NB, Mnaolalamika kuhusu Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo rudieni tena kusoma andiko hili kwa makini
Akili kisoda sana hii
 
Faida ya kusafirisha mizigo ndani na nje ya Tanzania ni kubwa kuliko ile kupakua mizigo,

Wachina watapata nasisi tutapata pia,

Bandari hii mpya itakuwa yapili baada ya ile ya Durban SA,
Entebbe ipo chini ya nani Sasa hivi unajua?
Licha ya tishio la ugaidi Uganda unajua kwann mpaka Sasa Museven yupo TZ?
Ukijua hilo utajua kwann bandari ya Bagamoyo ni upuuzi KWA sasa
 
Entebbe ipo chini ya nani Sasa hivi unajua?
Licha ya tishio la ugaidi Uganda unajua kwann mpaka Sasa Museven yupo TZ?
Ukijua hilo utajua kwann bandari ya Bagamoyo ni upuuzi KWA sas

Hebu fafanua vizuri Mkuu
 
Unajua mpango mikakati wa Reli?
Hivi huo uchumi mnasomeaga wapi nyinyi?
Kweli reli ikikamiliki ndo malori yatapaki?


Umewahi ona Dunia Gani hiyo,Acha mawazo ya kikoloni weweee
Sasa Yataendelea kubeba nini?
 
Kwani hizo contena zitabebwa na hiyo Reli mpaka mlangoni KWA tajiri?

Je ni mikoa yote Reli imepita?
Mimi nilimaanisha Local & Transit, Haya Malori ya vichochoroni yanaishaje mkuu?
 
Kaja kuomba hela huyo akakwamue uwanja wa ndege huo,na ndo sababu ya kuja wangu wangu TZ.
KWA tishio la ugaidi lilotokea,Museven asingeweza kuja haraka namna hii akaiacha nchi Zaid ya siku3
Daaah, Ila namwini sana Mama, Anawatu wazalendo sana, So relax
 
Back
Top Bottom