SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

Bandari ya Tanga! ambayo inakuzwa na pesa zipo!
 
Hawana utamaduni wa kufanya maintenance!! Wanadhani wakinunua kitu kipya kitakua hivyo hivyo kila siku!! Hata hizo Ndege za ATCL sidhani kama zinafanyiwa check zake kama inavyotakiwa!!!!
Huna uhakika lakini
 
Hata huko SGR itafika mkuu
 
Imefanya nini mkuu?
Point yangu hakuna haja ya bandari ya bagamoyo wakati tunatakiwa kukuza bandari ya Tanga ambayo itapitisha mafuta. Ushauri wangu ni kukuza bandari ya Tanga serikali ikiwekeza $2B itatosha kabisa badala ya kuwekeza $10B kwa bandari mpya!!
 
Umeandika mengi lakini mwishowe umeharibu kabisa! Hakuna mtu hasiyetaka bandari ya Bagamoyo isijengwe. Tatizo lipo kwenye uwazi wa huo mradi. Kumbuka mradi ni wa wachina, na hadi sasa wakati hii bandari ya Bagamoyo inapigiwa chapuo sana yaani kwa udi na uvumba tumejionea na tundelea kujionea wenyewe ni kwa kiasi gani China imekuwa na ajenda isiyo rasmi ya kujimilikisha baadha ya huduma/miradi mikubwa iliyo chini ya usimamizi wa Serikali nyingi za Kiafrica. Mfano: Kenya, Zambia, Uganda na hata Sudan ya Kusini kwa kigezo cha kushindwa kulipa mikopo yao. Husikurupuke tu bila kufanya upembezi yakinifu kwa maslahi mapana ya Nchi!
 
Point yangu hakuna haja ya bandari ya bagamoyo wakati tunatakiwa kukuza bandari ya Tanga ambayo itapitisha mafuta. Ushauri wangu ni kukuza bandari ya Tanga serikali ikiwekeza $2B itatosha kabisa badala ya kuwekeza $10B kwa bandari mpya!!
Wataalam wetu wanamajibu ni kwanini iwe hivyo
 
Ondoa hofu mkuu wangu,
 
Wataalam wetu wanamajibu ni kwanini iwe hivyo

Hakuna jibu la msingi mpaka sasa. Tunajua kuwa watu wanategemea kufaidika lakini haitakuwa na manufaa kwa taifa kuwa na badari tatu karibu vile.
 
Kama kuna kitu umenifungua macho basi ni hii logic

Kwa hesabu hii ni kweli Malori karibu yote yatapaki

Mungu mbariki Samia wetu,
C
Hakuna jibu la msingi mpaka sasa. Tunajua kuwa watu wanategemea kufaidika lakini haitakuwa na manufaa kwa taifa kuwa na badari tatu karibu vile.
Huoni kama ufanisi utaongezeka?
 
Point yangu hakuna haja ya bandari ya bagamoyo wakati tunatakiwa kukuza bandari ya Tanga ambayo itapitisha mafuta. Ushauri wangu ni kukuza bandari ya Tanga serikali ikiwekeza $2B itatosha kabisa badala ya kuwekeza $10B kwa bandari mpya!!
Tujenge tuu zote kama mahitaji yapo na pesa zipo
 
Tujenge tuu zote kama mahitaji yapo na pesa zipo
Hakuna pesa wala mahitaji. Ukweli ni kwamba tunatakiwa kuongeza uwezo wa mizigo tayari bandari ya Dar inapanuliwa na ya Tanga baada ya mkataba wa mafuta huko Uganda. sasa kwanini wasiongeze pesa kwenye hizo ambazo yatari kampuni ya total wanatupa na kuwa na bandari kubwa pale Tanga. Na gharama zitakuwa nafuu sana kwa uwezo huohuo. Kwanza bandari ipo, pesa za upanuzi wa bomba zipo hivyo unaongezea pale tu na sio kukopa $10B kwa uchumi wa $60B tu pesa zitaishia kulipa madeni. Lakini hiyo mizigo ambayo inasubiri bandari mpya iko wapi?. Uganda wanatumia ya Tanga, Zambia ya Dar sasa mizigo iko wapi?? ya bandari ya $10B? Lazima tufanye vitu kwa mpangilio hakuna pesa ya bure
 
Hii ya Bagamoyo itakuwa na kuvutia meli kubwa kubwa mkuu Wangu
 
Hii ya Bagamoyo itakuwa na kuvutia meli kubwa kubwa mkuu Wangu

Sasa kwanini wasipanue ya Tanga wakati tayari kuna mafuta yanapita pale!, nafasi ipo na itakuwa bei nafuu sana sana. Yaani nachosema hapa serikali isidakie tu kama vile pesa ni ya bure au mizigo ya bandari ya Dar itabaki hivi hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…