SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

Huna uhakika lakini
Reli ya kati imejifia kwa sababu hakuna matunzo na uendeshaji duni, ile reli ina uwezo mkubwa sana kama wangeitunza na kuifanyia matengenezo yanayotakiwa, TANESCO ndio hiyo hakuna umeme kwa sababu no maintenance ya mitambo, solution serikali ijiondoe kwenye hizi biashara waachie watu binafsi wenye taaluma zao na wanaojua biashara
 
Kuhusu Bandari ya Bagamoyo, tafadhali mkataba uwekwe wazi mapema, maana Chinese ni watu watata.
 
No ,Mimi nimewapa tu kaufunuo kahapo baadae

Mnapopinga ujenzi wa bandari na hili mlijue linawahusu
Wewe mwanaccm utambue pia kwamba hata Zambia Edgar Lungu na chama chake wameaadhibiwa kwenye kura baada kuwaachia Wachina Copper Belt na makampuni yao yanazokadiriwa kufika 6000 bila manufaa yoyote kwa Wazambia.
 
Wewe mwanaccm utambue pia kwamba hata Zambia Edgar Lungu na chama chake wameaadhibiwa kwenye kura baada kuwaachia Wachina Copper Belt na makampuni yao yanazokadiriwa kufika 6000 bila manufaa yoyote kwa Wazambia.
Achana na mambo ya Zambia, Niushamba kuilinganisha Tanzania na Zambia,
 
Ulaya ina mtandao mkubwa wa reli tena za uhakika ila malori yapo ya kutosha
 
Ila tukumbuke kuwa wenye malori ni;
wanasiasa wakubwa
wabunge
mawaziri
makatibu wakuu
na wenye ushawishi mkubwa ktk serikali hii.
Kwa mwendazake wangeshindwa kabisa kukwamisha mradi huu ILA kwa Mama SSH lolote linaweza kutokea na tukakwama na mradi huu bora.
 
Umeandika dhana kadhaa halafu ukashindwa kuzijengea hoja ili zitoke kuwa dhana na kuwa na uhalisia.

Bandari ya Bagamoyo ni JV Joint Venture kati ya serikali ya TZ na watu wa dubai ambapo China wanao ushawishi kwenye biashara yao.

Hivyo ni dhana tu kusema kuwa China itapokonya mali ikiwa deni litashindikana kulipwa. Ubalozi wa China umejenga hoja ya msingi kwamba mbona biashara nyingi zenye mtaji kutoka Magharibi zinakufa na hakuna aliyeporwa hizo biashara?.

Mzigo uingizwe kwa bandari kwa Tanzania ni fursa, uingizwe kwa malori kwa jamii ya wafanyabiashara pia ni fursa njema tu.
 
Mkuu hata kama Bandari ingekuwa ya Wachina bado SGR ni yetu tutapiga pesa tu,
Save your breath.
SGR haitakamilika Leo Wala kesho.
Tuliambiwa kipande Cha Dar Moro kitakamilika November 2019.
Leo Ni November 2021 hata dalili hakuna.
Unategemea hao wenye malori watakubali malori yao ya paki?
Kwanza jiulize wenye hayo malori Ni kina Nani?
Siongelei Hawa wenye fuso au scania za kubebea ng'ombe, naongelea wenye malori 200 ++
 
Hata kama 2030 itakamilika tu, Kaziiendelee
 
Asilimia kubwa ya mizigo kutoka bandarini inaelekea upande wa boda ya Tunduma ambako hakujapewa kipaumbele cha kujenga hiyo SGR, hiyo itakuwa inajengwa kwa ajili ya kusafirisha abiria sidhani kama target yao ilikuwa ni mizigo.
 
Umesema trip moja ya treni itakuwa inabeba tani 10,000..
Container moja la 40ft lina uzito wa wastani wa tani 25 maximum, na hilo linabebwa kwenye behewa moja.. So hiyo treni itakuwa inavuta mabehewa 400 at a go ? , nafikiri tutaingia katika World guiness record..
 
I like people who argue with facts and figures.
Misukule mingine ikiambiwa kitu na wanasiasa hawachukui muda wa ku assess, inakubali moja kwa moja Kama wabunge wa bunge hili.
 
Kontena la kitu gani unazungumzia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…