SGR itasafirisha nini?

SGR itasafirisha nini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nadhani ujenzi wa reli ya kisasa ni jambo ghali Sana. Wakoloni walijenga reli kibiashara je SGR inajengwa kibiashara pia? Bidhaa zipi kutoka wapi zitasafirishwa kifaida kwenda wapi?

Sioni mazao ya kilimo, bidhaa za viwandani wala mizigo ya bandari mingi Sana inayohitaji kuyafikia masoko haraka na Kwa wingi.

Ujenzi wa SGR ungeendana na upanuzi wa bandari, mashamba na viwanda. Lakini hata tukipanua bandari, kilimo na viwanda je, masoko ya bidhaa hizo ni akina nani ambao wanaishi wapi?
 
Ulichokiandika tulio wengi wavivu wa kufikiri, na kuamua jambo kwa kutazama sura, tutakuona mjinga. Mantiki iliopo kwenye hoja yako ni kubwa. Hata barabara za kupitika muda wote toka mashambani kuleta mazao kwa walaji ni shida. Kupanga ni kuchagua. Nahisi wapangaji na wachaguaji wetu hawana muda japo wa kutujulisha. Wangefanya hilo, mengi tungesema no!
 
Nadhani ujenzi wa reli ya kisasa ni jambo ghali Sana. Wakoloni walijenga reli kibiashara je SGR inajengwa kibiashara pia? Bidhaa zipi kutoka wapi zitasafirishwa kifaida kwenda wapi?
Sioni mazao ya kilimo, bidhaa za viwandani wala mizigo ya bandari mingi Sana inayohitaji kuyafikia masoko haraka na Kwa wingi.
Ujenzi wa SGR ungeendana na upanuzi wa bandari, mashamba na viwanda. Lakini hata tukipanua masoko ya bidhaa hizo ni akina nani ambao wanaishi wapi?

Itakuwa ikisafirisha watumishi kutoka dar kwenda dom, maana hawataki kuishi dom
 
Watakuwa wanaonekana Dodoma mapaka saa1 jioni giza likiingia tu wanarudi kulala dar,kesho yake asubuhi unamkuata tena ofisini
 
Inawezekana watu wanafikiria zaidi DRC, Rwanda, Burundi na Uganda? siasa za nchi hizo sio za kuaminika kibiashara hata kidogo, huwezi kuingia gharama kwaajili Yao. Hizi ni nchi ambazo zitakupa masharti makali ya kutimiza kabla ya kuwauzia chochote.
 
Watakuwa wanaonekana Dodoma mapaka saa1 jioni giza likiingia tu wanarudi kulala dar,kesho yake asubuhi unamkuata tena ofisini

Ndo hivo Mzeee baba ,,, maana Dodoma hamna kikubwa cha kubeba huko labda mpaka watakapo kuja na awamu ya pili maana kwa sasa inaishia Dom
 
tutaweka train ya mwendo kasi toka dodoma saa tatu usiku kwenda dar,kisha toka dar saa kumi na moja alfajiri ili wafanyakazi wawahi dom kazini,kusafirisha ngombe na mazao toka kanda ya ziwa etc,mazao kama viazi vitamu,mahindi,maharagwe etc
 
Tunatakiwa kumuunga mkono Mkulu. Kwani Kuna ubaya gani nasisi tukiwa navyo.
 
Watakuwa wanaonekana Dodoma mapaka saa1 jioni giza likiingia tu wanarudi kulala dar,kesho yake asubuhi unamkuata tena ofisini
Hilo haliwezekani, kwa safari ya masaa 6 njia moja,kazi watafanza saa ngapi Kama watumia masaa 12 njiani(to&fro).....
 
tutaweka train ya mwendo kasi toka dodoma saa tatu usiku kwenda dar,kisha toka dar saa kumi na moja alfajiri ili wafanyakazi wawahi dom kazini,kusafirisha ngombe na mazao toka kanda ya ziwa etc,mazao kama viazi vitamu,mahindi,maharagwe etc
Masaa 3 kwenda Dom haitawezekana..........
Reli inayojengwa itakuwa na uwezo juu wa spidi 140km/hr, reli kwa njia inayopita na kandarasi iliyo sainiwa Ni km 600+ Hadi Dom......

Kwa hesabu rahisi; treni itakoyopita juu ikienda kwa spidi ya juu kabisa Ni 140km/hr (usalama pembeni+ hakuna kusima vituo katikati),umbali 600km....

600km ÷ 140km/hrs (umbali gawa kwa spidi)= 5hrs

Vipi ukiweka usalama kwa kutomaliza spidi ya mwisho na ikasima hata vituo 2(Moro, kilosa) haya itachache kutumia 6hrs kufika Dom.....

Nani ataenda kufanya kazi (kwenda na kurudi) kwa siku, masaa 12 kwenye treni na bado huishi/hukai stesheni ya dar(umbali wa kwenda nyumbani/kazini)
 
Itatumia masaa nane na nusu Hadi mwanza
 
@COSMOLOGIST,hapo umenijibu kitaalamu,sina ubishi
Mkuu kwani umesahau jinsi ambavyo tz tukitaka kufanya mradi flani jinsi ambavyo huwa unakuzwa Tena kwa tambo......
2000s songas- tuliambiwa mgao/kukatika kwa umeme ingebaki historia tz....
2010 gasi mtwara- tz mkaa itakuwa hadithi...
2010/16 brt- foleni dar itakwisha kabisa ...
2005 Richmond/dowans/aggreco- tutazalisha mega Hadi kuzidi mahitaji....
Na n.k
 
Itatumia masaa nane na nusu Hadi mwanza
Duh........labda
Masaa 3 kwenda Dom haitawezekana..........
Reli inayojengwa itakuwa na uwezo juu wa spidi 140km/hr, reli kwa njia inayopita na kandarasi iliyo sainiwa Ni km 600+ Hadi Dom......

Kwa hesabu rahisi; treni itakoyopita juu ikienda kwa spidi ya juu kabisa Ni 140km/hr (usalama pembeni+ hakuna kusima vituo katikati),umbali 600km....

600km ÷ 140km/hrs (umbali gawa kwa spidi)= 5hrs

Vipi ukiweka usalama kwa kutomaliza spidi ya mwisho na ikasima hata vituo 2(Moro, kilosa) haya itachache kutumia 6hrs kufika Dom.....

Nani ataenda kufanya kazi (kwenda na kurudi) kwa siku, masaa 12 kwenye treni na bado huishi/hukai stesheni ya dar(umbali wa kwenda nyumbani/kazini)
Ila Hadi mwanza umbali lazma ufike km 1500(Kama itazunguka tabora Kama hii ya Kati/iliyopo)....

Kumbuka;kwa barabara Dar - Dom Ni km 460, ila mzungukuko wa reli Ni 600
 
Back
Top Bottom