Wewe acha longolongo, leta ushahidi unaonyesha kwamba WB walisema kwamba SGR is not viable project.
Wewe hujui lolote lile zaidi ya kupiga domo tupu. Ngoja tukufunze.. Kipindi cha Jakaya Kikwete, serikali iliomba fedha WB kukarabati bandari ya Dar Es Salam na kufufua reli ya kati, WB ikakubali na kutoa hizo pesa, serikali ya Kikwete haikuwa na mpango wa kujenga reli ya SGR kwa haraka, lengo lilikua ni kuharakisha kupanua bandari ya Dar na kusafirisha cargo ambayo ilikua inalimbikizana.
Magufuli yeye alitoa sana kipaumbele ktk SGR, ili kufingua fursa za uchumi, hasa kusafirisha chuma kule Liganga na Mchuchuma, uwekezaji wa kuchimba Nickel na Bati huko Kigoma na Burundi, na Copper, madini haya ni mazito sana, bila kuwepo kwa train yenye uwezo mkubwa, yataendelea kubaki ardhini, huku tukiendelea kujisifia kwamba nchi hii ni tajiri lakini watu ni masikini.
Sera ya WB ni kutofadhili parallel projects, hiyo ni sawa na "duplication of Projects", kama umeshawahi kufanya kazi katika "NGO" nadhani utaelewa maana yake, hiyo ndio sababu hata serikali haikuomba WB wafadhili SGR kwasababu ilijulikana wazi kwamba WB walishatoa pesa za kufufua reli ya zamani, aiwezekani tena walipie reli mbili katika nchi moja. Kama wangekua hawakutoa pesa za kukarabati reli ya zamani, wangetoa bila kigugumizi pesa za SGR.