SGR kuziba njia za watu bila kuweka utaratibu mbadala Dodoma mjini

SGR kuziba njia za watu bila kuweka utaratibu mbadala Dodoma mjini

Katika mradi wa ovyo ulivotumika kujenga reli.
Subirini mvua zije?. Hii kauli mtaikumbuka
Halafu ndo mnaanzaga hivi hivi kulihujumu Taifa.
Utashangaa kweli mwakani au baada ya miaka miwili, huu utabiri "uchwara" unatimia kweli kwa hasara ya nchi!
 
Huu mradi ni kizungumkuti, Morogoro mitaro ya maji imeelekezwa kwenye makazi ya watu. Ni mafuriko tu.
 
Nahisi wewe uzunguki maporini. Kuna sehemu reli imepitishwa juu na kuzibwa njia za mishipa ya maji. Subiri tu kwani mi mvua
Mkuu Tanzania yote hii nimeshazunguka ikiwa ni pamoja na sehemu reli ilikopita.
Swali langu kwako ni Je, umejuaje kwamba hadi mvua zinanyesha hiyo miundombinu itakuwa haijarekebishwa ilhali sote tunajua kazi bado inaendelea?!
 
Katika mradi wa ovyo ulivotumika kujenga reli.
Subirini mvua zije?. Hii kauli mtaikumbuka
Mvua za El Nino zimenyesha. Zimeleta mafuriko na kuharibu miundombinu kibao lakini hii reli iko intact. Watu wamezoea kuvuka kila mahali kama mbuzi wamewekewa sehemu maalum wanaona shida.
 
Mkuu Tanzania yote hii nimeshazunguka ikiwa ni pamoja na sehemu reli ilikopita.
Swali langu kwako ni Je, umejuaje kwamba hadi mvua zinanyesha hiyo miundombinu itakuwa haijarekebishwa ilhali sote tunajua kazi bado inaendelea?!
Anaropoka tu huyo. El Nino si imeisha miezi michache iliopita? Au reli haikuwepo.
 
Halafu ndo mnaanzaga hivi hivi kulihujumu Taifa.
Utashangaa kweli mwakani au baada ya miaka miwili, huu utabiri "uchwara" unatimia kweli kwa hasara ya nchi!
Ukijenga bondeni ukaambiwa toka kuna mafuriko. Ukakaza fuvu mvua zikijaa nyumba ikaezuliwa unasubiri kuja kulaumu serikali?

Alichosema jamaa sio utabiri bali ni Fact
 
Hii ni aibu kwa kweli reli hii inavopendwa na wa tz lakini sasa sgr wamefanya kituko ambacho hata kusema ni reli ya kimataifa ni aibu tena aibu sana ! Yani nyumba zilizopo karibu na reli sgr (Dodoma makulu )umepita uzio kwenye njia walizokuwa wakitumia hata gari za dharura haziwez kufika . Hata bajaji haziwezi kufika je wananchi hao serikali haioni ama ni kuwanyima haki yao ya msingi na kudhoofisha maendeleo?

Kwamba watu wa upande mmoja hawana jinsi yeyote ya kwenda upande mwingine hata kwa kuzunguka umbali fulani?

Uzio umewekwa kwa ajili ya usalama wenu, reli ya treni za umeme si ya kukatiza kama zile za kawaida...
 
Shida yetu wa Tanzania ndio hii. Huwa mtu akisema kitu kama hakikuhusu unapita kama huoni! Hizi habari watu wa banana na gongolamboto walilalamika sana ila kwa kuwa kwenu Dodoma ilikuwa hamjakatazwa bado mkasoma mkapotezea. Sasa mmekatazwa mnalalamika the same! Laiti mnge join forces kipindi kile pengine kungekuwa na impact.

Sasa we unalalamika saa hizi mtu wa Masasi au Gairo anakuona chizi subiri ahamie Dodoma ataleta uzi upya kulalamika kuzuiwa kuvuka relini
 
Back
Top Bottom