Sitapoteza muda mwingi kukujibu maana ni kama huwa unavuta mmea fulani, maana hii mada huwa unaibuka nayo kwa mwezi mara moja, mwanzoni tulihangaika kukuelimisha, tukakuletea data nyingi tukitegemea utakua na akili. Lakini baada ya mwezi mmoja unarudia hoja ile ile huku ukitumia kichwa tofauti.
Kifupi ni kwamba nchi yetu ya Kenya tumejijengea wenyewe, tulishaorodhesha humu miradi yote ambayo imekua ikiendelea Kenya. Sina haja ya kuyarudia yote. Lakini miaka ya themanini tulicheleweshwa na chama tawala dhalimu cha wakati ule, kama jinsi Tanzania inacheleweshwa na CCM hadi leo. Tanzania ya leo inayojinadi ya kubana matumizi, mnajenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini maeneo ya Chato ambapo hamtegemei mtu yeyote wa kimataifa kutua pale. Bora hata mngeboresha Bukoba iwe ya kimataifa. Mambo kama hayo ndio yalituchelewesha sana kipindi cha uongozi wa chama tawala cha wakati ule.
Lakini punde tu, tulipokibadilisha na kukipiga chini hicho chama, Kenya ilipepea na kuiacha Tanzania kwenye vumbi na lindi la umaskini. Hata Tanzania itawabidi mfikie huo uamuzi, ikiwezekana kwenye uchaguzi wa 2020 hapo ndio mtaona nchi inaanza kupiga hatua za kweli. Lakini kwa sasa mtaendelea kuona vioja na ukurupukaji wa hali ya juu, mara mnahamia Dodoma, mara naona eti Makonda kasema watu wa Mikoani msije Dar bila sababu maalum, mara watu wasiokua na kazi wahesabiwe Dar, mara kushtukiza kule mara hiki, mara kile, yaani hakuna mikakati, hakuna mpango wowote, ni kukurupuka full kwenda mbele.