Sh102.3 bilioni kwaajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT)

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Serikali kutoa Sh102.3 bilioni kwaajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT).

Chuo kikuu cha sokoine kilianzishwa mwaka 1984 hadi leo wasomi wake wanahaha mitaani hawana ajira na wameshindwa kujiajiri, wengine wameamua kutengeneza mapanya ya kulipua mabomu naTanzania hakuna vita.

Sasa wanaanzisha chuo kikuu kingine cha kisiasa cha kwenda kuzslisha wasomi wa kilimo cha kuzalisha wasomi wa kujiuza mjini, kuendesha bajaji, boda boda, madalali, na watazamaji wa michezo ya simba na yanga.

Je serikali haioni inakwenda kuwekeza kwenye chuo kikuu kingine cha kuzalisha wasomi ambao hata serikaki imeshindwa kuwatumia?

Kwanini wasiboreshe chuo kikuu cha sokoine kwa kuanzisha campus ya kilimo huko butiama badala ya kuanzisha chuo kikuu kingine cha kilimo huko butiama?
 
Bora wangeiwezesha SUA, kuliko kuongeza vyuo kwenye mkoa ambao kilimo ni changamoto

Eti wanaenda jenga chuo cha tehama
Kwanini wasiendeleze Udom?
 
Hiki kinaonyesha ni chuo kikuu cha kisiasa na kitakuja kufa tu.
 
Tatizo mnajadili yanayowazidi kimo! Wewe Nadhani hata kadegree kamoja huna unaanza kuzungumzia vyuo vikuu

Kwa hapa Tanzania hakuna tofauti ya mwenye elimu ya chuo kikuu, na mwenye elimu ya msingi. Kama profesa alipakia ndege akaenda Madagascar kuchukua dawa ambayo haikuwa na udhibitisho wa Kimaabara, hapo kuna wasomi kweli?
 
Serikali kutoa Sh102.3 bilioni kwaajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT).

Chuo kikuu cha sokoine kilianzishwa mwaka 1984 hadi leo wasomi wake wanahaha mitaani hawana ajira na wameshindwa kujiajiri, wengine wameamua kutengeneza mapanya ya kulipua mabomu naTanzania hakuna vita.

Sasa wanaanzisha chuo kikuu kingine cha kisiasa cha kwenda kuzslisha wasomi wa kilimo cha kuzalisha wasomi wa kujiuza mjini, kuendesha bajaji, boda boda, madalali, na watazamaji wa michezo ya simba na yanga.

Je serikali haioni inakwenda kuwekeza kwenye chuo kikuu kingine cha kuzalisha wasomi ambao hata serikaki imeshindwa kuwatumia?

Kwanini wasiboreshe chuo kikuu cha sokoine kwa kuanzisha campus ya kilimo huko butiama badala ya kuanzisha chuo kikuu kingine cha kilimo huko butiama?
Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology? Kenya hawatushindi.......
 
Kwahiyo kama Serikali ina Chuo cha Afya Muhimbili haipaswi kuanzisha Chuo kingine cha Afya Dodoma, Mbeya au sehemu nyingine!!?

Au kama Serikali ina SUA haipaswi kuanzisha Chuo Kikuu kingine Mzumbe?

What a school of thought you guys have! Acheni kuona siasa kwenye kila kitu.
 
Kitasaidia ajira kwa wale ambao waliomaliza na ramani hazisomi
 
Kwahiyo kama Serikali ina Chuo cha Afya Muhimbili haipaswi kuanzisha Chuo kingine cha Afya Dodoma, Mbeya au sehemu nyingine!!?

Au kama Serikali ina SUA haipaswi kuanzisha Chuo Kikuu kingine Mzumbe?

What a school of thought you guys have! Acheni kuona siasa kwenye kila kitu.
Zungumzia impact ya chuo kwenye jamii mkuu.
SUA imekuwa kaa la moto kwa wanaomaliza pale kupata ajira.
Sasa unazalisha SUA nyingine karne ya 21?
 
Kama profesa alipakia ndege akaenda Madagascar kuchukua dawa ambayo haikuwa na udhibitisho wa Kimaabara, hapo kuna wasomi kweli?
Huyo si alimuita magufuli Mungu! Popote ambapo magufuli angemtuma kufanya chochote angeenda. Alisema pia magufuli alimtoa jalalani.
 
Nahisi wengi hapa ni vijana hawaelewi hama ni nia ya kuhadaa watu.

Chuo hiki hakianzishwi kesho na hakijaanzishwa jana ni almost 8yrs past sasa, nakumbuka mwaka 2014 akiwa naibu waziri wa elimu Jenister Mhagama alitoa taarifa bungeni juu ya wizara ya fedha kukubali kutoa fedha kwa ajili ya chuo hicho.

Na mwaka huo huo 2014 mwezi wa 12 akiwa wa Rais wa JMT, Jakaya Kikwete alimteua Prof, Dominic Kambarage kuwa VC na hata leo pia yupo ndg yangu Prof. Msafiri.

Baada ya danadana nyingi za ujenzi wa chuo hicho naona leo kama siyo jana, juzi rasmi serikali inatoa fedha, kinachofanyika sasa kwa vijana wa jana msilete upotofu.

Hata tukiwa na vyuo vya kilimo kila kanda si sababu ya kusema wasomi hawana kazi na wapo mtaani, dhima ya maisha ni kila mtu asome na apate elimu ya kiwango hata chuo kikuu.
 
Tanzania mwenye degree= mwenye diploma =mzururaji
Bora la saba wanajituma na wanajitambua
Tatizo letu Tanzania siyo Vyuo. Tatizo letu ni Wahitimu. Kama umehitimu Chuo Kikuu, lakini ukawa sawa na Darasa la Saba, tatizo ni la Mhitimu, siyo Chuo alichosoma. Kama uliokuwa nao darasani wanafanya mambo makubwa, kama vile Mwl Kuku, jiulize wewe tatizo lako ni nini.
Naunga mkono kujenga Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolijia. Bora Tanzania ifurike wazururaji wenye elimu ya Chuo Kikuu, kuliko wenye elimu ya Kidato cha Nne. Watanzania, tutambue kuwa Uwekezaji mkuu katika Nchi, ni Uwekezaji katika Elimu.
 
Back
Top Bottom