Shabibiy: Nilinunua basi langu la kwanza nikiwa na miaka 19. Asema mafanikio yake siyo ya kurithi

Mimi ni mkazi wa Gairo nimefanyakazi kwa Shabiby kwenye miaka 90 mwishoni. Jamaa ni mpambanaji hakuna uchawi wala pembe za ndovu.

Shabiby aliacha shule kidato cha 2 akaingia shambani kulima mahindi huku akianzisha biashara ya kuuza mafuta kwenye videbe, mtaji ukakua akaanzisha kijisheli pale Gairo na wateja wake wengi wakiwa ni wakulima wa mahindi wenye matrekta.

Ni kweli baada ya muda mfupi akanunua basi bovubovu akalikarabati na akaanza safari za Mpwapwa, basi Mpwapwa alipiga hela sana na akaanza kununua chases mtumba za scania na volvo. Pale kwake Gairo kwenye shell akafungua gereji kwa ajili ya kutengeneza body za mabasi kipindi hicho mabasi ya yutong bado hayajaingia na wafanyakazi wa kuunda bodi aliwatoa Kenya akawaleta Gairo hiyo ilikuwa kwenye 2004-2005 hivi, kwahiyo akawa na mabasi zaidi ya 10. Na alilishika soko la abiria karibia wote wa Dodoma-Dar, Dodoma- Mbeya na Dodoma -Arusha kupitia Chalinze.

2000 mwanzoni akafungua shell nyingine Dodoma mjini pale round about ya Makole na wakati huohuo ana trekta kama zaidi ya 15 analima mahindi Kibaigwa na kwahiyo kwa kifupi utajiri wa Shabiby hauna makandokando kwasababu anaanza 0 namuona kwahiyo sishangai huku 100 alikofika.

Utajiri uliomfanya awe juu zaidi ni mafuta, kipindi hicho alikuwa anauza mafuta kwa bei ya chini sana kiasi kwamba wateja walikuwa wanapigana vikumbo kwenye shell zake. Haina maana kwamba alikuwa anachanya na mafuta ya taa NO! Sijui alitumia mbinu gani kupata mafuta kwa bei rahisi, kumbuka kipindi hicho hakuna EWURA.
Bado akajenga hotel MORENA iliyopo Dodoma.

Haya ndio niliyoyashuhudia wakati nafanya kazi kwake kama kuna mengine nyuma ya pazia siyajui.

Sent from my SM-A105FN using JamiiForums mobile app
 
We endelea kubishana na shabiby na una miaka 30 kitu pekee unachomiliki ni kisosi cha kuzimia sigara, na viatu pea mbili kwaajili ya kwenda bar kununuliwa pombe za bure
Hahahaaa
 
Unaweza ukaanza kuuza vitunguu reja reja baadae jumla then unakuja benk unaomba mkopo unakuza biashara inaenda Ivo Ivo mpaka unanunua hiace then hiace inazalisha unakuja kununua basi.
 
Baada ya kuyashuhudia yote haya kwa Shabiby vile anatajirika wewe una nini? Au huna bidii?
 
Urongo bhana huo ni uwongo
 
Tunachokijua: Si bidii pekee

Sent from my G3121 using JamiiForums mobile app
 
Mafanikio ni siri nzito na nyingi, M/Mungu aendelee kumjaalia mema InshAAllah
 
Inatokana na bidii yako unaifanyia wap mkuu,kuna tofauti ya anaefanyia bidii yake kwny kubeba mizigo ya buku each na ambae yuko mgodini
Tena mgodini ndio kuna mambo mengi ya ajabu; kule sio bidii tu bali maarifa mengine ya ziada
 
Angesema ni kazi zipi ili na sisi wengine tufanye maana 19 yrs. Ununue gari enzi hizo mhhh?? Hata sasa hivi wenyewe huwezi labda uuze ngada au uwe na duka sinza (mdangaji)
 
Bado huwezi kujua chanzo cha mapato cha huyo jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…