Mrs Thabo Bester
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 3,144
- 7,937
Bora kukiri haya!Mimi ni mkazi wa gairo nimefanyakazi kwa shabiby kwenye miaka 90 mwishoni.jamaa ni mpambanaji hakuna uchawi wala pembe za ndovu.
Shabiby aliacha shule kidato cha 2 akaingia shambani kulima mahindi huku akianzisha biashara ya kuuza mafuta kwenye videbe,mtaji ukakua akaanzisha kijisheli pale gairo na wateja wake wengi wakiwa ni wakulima wa mahindi wenye matrekta.
Nikweli baada ya muda mfupi akanunua basi bovubovu akalikatabari na akaanza safari za mpwapwa,basi mpwapwa alipiga hela sana na akaanza kununua chases mtumba za scania na volvo.pale kwake gairo kwenye shell akafungua gereji kwa ajili ya kutengeneza body za mabasi kipindi hicho mabasi ya yutong bado hayajaingia.na wafanyakazi wa kuunda bodi aliwatoa kenya akawaleta gairo hiyo ilikuwa kwenye 2004-2005 hivi,kwahiyo akawa na mabasi zaidi ya 10. Na alilishika soko la abiria karibia wote wa dodoma= dar,dodoma- mbeya na dodoma -arusha kupitia chalinze.
2000 mwanzoni akafungua shell nyingine dodoma mjini pale round about ya makole na wakati huohuo ana trekta kama zaidi ya 15 analima mahindi kibaigwa na .kwahiyo kwa kifupi utajiri wa shabiby hauna makandokando kwasababu anaanza 0 namuona kwahiyo sishangai huku 100 alikofika.
Utajiri uliomfanya awe juu zaidi ni mafuta,kipindi hicho alikuwa anauza mafuta kwa bei ya chini sana kiasi kwamba wateja walikuwa wanapigana vikumbo kwenye shell zake.Haina maana kwamba alikuwa anachanya na mafuta ya taa NO! Sijui alitumia mbinu gani kupata mafuta kwa bei raisi,kumbuka kipindi hicho hakuna EWURA.
Bado akajenga hotel MORENA iliyopo dodoma.
Haya ndio niliyoyashuhudia wakati nafanyakazi kwake kama kuna mengine nyuma ya pazia siyajui.
Sent from my SM-A105FN using JamiiForums mobile app
Na wewe umeamini aha ha a,Mfanyabiashara anayemiliki Mabasi ya Shabiby, Ahmedy Shabiby ambaye pia ni Mbunge wa Gairo amesema alifanikiwa kununua Basi lake la kwanza akiwa na umri wa miaka 19 kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kusisitiza kuwa hakuna mbadala mwingine wa mafanikio zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.
Shabiby amesema wakati anasoma alikuwa akijishughulisha na biashara ndogondogo na kilimo jambo lililomfanya akiwa na umri wa miaka 19 aweze kununua basi lake la kwanza la kusafirisha abiria.
Shabiby ameongeza kuwa Watu wengi wamekuwa wakidhani mafanikio aliyoyapata yametokana na kuzaliwa kwenye familia ya kitajiri na kurithi mali jambo ambalo amesema sio la kweli bali siri ni kufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii bila kukata tamaa.
Aya ya mwisho, hajui alikuwa anapata wapi mafuta ya bei Rahisi.Bora kukiri haya !
Yatafute na wewe uanze kupiga faida ..sio kuwa negative kwa matajiriAya ya mwisho, hajui alikuwa anapata wapi mafuta ya bei Rahisi.
Hata hizo kazi ulizozitaja ukizifanya bila bidii unazeeka huna meno wala nguvu za kiumeFanya kazi kwa bidii na maarifa mtu wangu.😂😂Stori za wenye fedha wanakwambia siri ni kufanya kazi kwa bidii wakati ni wapigaji wa madili ya meno ya tembo, wezi wa mali za uma, wazee wa madawa ya kulevya na mfanano wake
Ila kwenye media, walifanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya fedha.
Mimi huwaga Sina shidaa na historia za matajiri wa Tanzania.Yatafute na wewe uanze kupiga faida ..sio kuwa negative kwa matajiri
"Maarifa"👊Hata hizo kazi ulizozitaja ukizifanya bila bidii unazeeka huna meno wala nguvu za kiumeFanya kazi kwa bidii na maarifa mtu wangu.😂😂
Tupo wengiMimi huwaga Sina shidaa na historia za matajiri wa Tanzania.
Maana hazinisaidii
Shukria sana boss!🙏"Maarifa"👊
Vyote hivyo fanya kwa BIDIIIwe kazi halali au haramu ifanye kwa bidii.
Bidii (maana yake kwa kujituma na kuifanya kwa njia mbadala za giza au za mwanga, kuwadhulumu wafanyakazi mishahara, kutapeli, kuvusha magendo nk) hivyo ndivyo shabiby anavyosomeka
Faraja yetu masikini ni kujiambia mtu huwezi kuwa Tajiri bila dhuluma,uchawi,uuaji na njia zozote za mkato. Yaani hii inatufariji kuwa sisi si matajiri kwasababu hatuui,hatufanyi uchawi wala uhalifu ndio maana sio matajiri.Yatafute na wewe uanze kupiga faida ..sio kuwa negative kwa matajiri
Hakuna kitu nakereka kama hayo maneno uloandika hapo...aloturoga alituweza aise...inakera mno.....Faraja yetu masikini ni kujiambia mtu huwezi kuwa Tajiri bila dhuluma,uchawi,uuaji na njia zozote za mkato. Yaani hii inatufariji kuwa sisi si matajiri kwasababu hatuui,hatufanyi uchawi wala uhalifu ndio maana sio matajiri.
[emoji23]Yap ndio hivyo
Sema huyu kashapata ela kwa njia zake anawachagulia tu maneno ya kuwapa [emoji1]
Nikizipata na mimi ntawaambia tu nilivyokuwa nasoma nilijishughulisha na biz ndogondogo wakti wenzangu wanaenda kudimbwi mpaka sasa namiliki hotel 5 [emoji14]
Hizo ulizotaja ndio kazi zenyewe, ukisoma kwa umakini utagundua wanakwepa kusema ni kazi ganiStori za wenye fedha wanakwambia siri ni kufanya kazi kwa bidii wakati ni wapigaji wa madili ya meno ya tembo, wezi wa mali za uma, wazee wa madawa ya kulevya na mfanano wake
Ila kwenye media, walifanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya fedha.