Heaven Seeker
JF-Expert Member
- May 12, 2017
- 479
- 1,071
Wakuu bila kupoteza muda.
Kama mnavyojua, gharama za ndege, miaka michache hapo nyuma zilipanda kwa speed ya mwendokasi. Basi kama ujuavyo sisi wazee wa uchumi wa kuunga unga tunakuwa hatuna option nyingine zaidi ya kupanda ma-bus.
Nipo hapa nafanya plan yangu ya safari zangu za Dar - Mbeya, Mbeya-Mwanza, kisha Mwanza- Dar. Safari ambazo nitazifanya miezi michache ijayo.
Sasa niwe mkweli kuwa, kipindi cha nyuma kidogo, gharama ya usafiri ilikuwa ndio primary factor ya ku-determine aina ya usafiri nitakaotumia.
Sasa baada ya kufika nchi za wenzetu Ulaya, nikagundua kumbe kwa kiasi kikubwa ajali zinazotokea bongo zinaweza kuepukwa hasa kwa njia zifuatazo,
1) Kuwa na barabara ambazo ni nzuri. Mfano kunakuwa na two lanes za one way. Yaani kwa lugha rahisi magari yanayoenda hayakutani uso kwa uso na magari yanayorudi.
2) Kuwa na magari yenye ubora kwa kuzingatia usalama wa abiria
3) Kuwa na madereva wenye weledi
4) Kuwalipa mishahara mizuri madereva
5) Dereva mmoja kutoendesha gari kwa muda mrefu sana
6) Dereva kutotumia vilevi
7) Magari kuwa na speed ambayo ni optimal.
8) Kuzingatia kanuni zote za barabarani
Kwa hiyo zile kauli uchwara eti kwa mfano;
1) Ajali haina kinga.
2) Siku zako zikifika zimefika
3) Kifo hakiepukiki
4) Mungu ndiye sijui kapanga ufe siku hiyo kwa ajali
(Mbona matajiri wengi hawapati hizo ajali?) Au Mungu katupangia tufe sisi tu makabwela? Hii si kweli.
Baada ya kutembelea nchi za wenzetu nimegundua kauli zote hizo ni kauli uchwara tu na zinakwepa jukumu la kuchukuwa hatua dhidi ya kulinda maisha ya mwanadamu dhidi ya vifo vinavyosababishwa na wanadamu wenyewe.
Baada ya kuzingatia yote hayo, nimegundua angalau kampuni ya Shabiby (angalau) inaendana na sifa za magari yenye usalama wa maisha ya mwanadamu, ukiachana na factors nyingine kama hali ya barabaraba.
Sasa kwa bahati mbaya, nimeingia online kwenye website yao sioni route ya Dar- Mbeya. Hii route nadhani ilikuwepo ila sijui kwa nini siioni saivi.
Chakusikitisha zaidi, sijawahi kuona magari ya Sabiby kutoka Dodoma kwenda Mwanza.
Tafadhali sana Shabiby, tunaomba usikie kilio chetu sisi wazee wa uchumi wa kuunga unga ila inapokuja suala ya usafiri tupo tayari hata kulipia zaidi (siyo lakini kama zile bei za ndege).
Yaani mfano mie nipo tayari nilipie hata mara mbili ya nauli ya kawaida kutokea Dodoma - Mwanza. Ilimradi tu chombo cha usafiri kiwe cha uhakika na usalama mkubwa zaidi.
Hapa nimeshindwa hata kuchagua kuwa nitumie ma-bus yapi. Maana haya mengine unasafiri roho ikiwa inaelea juu juu. Unakuwa unahisi kama roho anytimne inaweza kuchomoka ikuachie mwili wako.
Mliopo karibu na tajiri Shabiby muulizeni kwanini hapendi kupeleka magari yake kwenye hii route ya Dar/Dodoma - Mwanza? Tatizo ni nini?