Shabiby ndiye pekee mwenye sifa ya kutoa huduma za safari za barabarani hapa nchini! Nilikuja Moshi kwa wife hapa chap siku mbili. Nikajiskia homa kali sana ila nikaona sio kesi,kesho naweza kusafiri. Nikaingia online fasta kikachagua siti yangu nikajaza taarifa fupi chap kwa haraka nikalipia tiketi yangu!
Jioni homa imezidi,nikalazwa hospitali nikabugia drip 3 za maji chapchap na madawa kibaao na mashart kibao ya daktari. Saa moja usiku niko kitandani nikaona kabisa safari haiwezekani. Kikapiga Shabiby Customer care nikawaeleza. Kwanza nikapewa pole sana na yule mrembo,kisha nikapewa namba ya Mrema Agent wao hapa Moshi
Nilimpigia huyu mwamba huku nikiongea kwa taabu sana. Mrema akanipa pole sana. Akanishauri bro endelea kupumzika na kuzingatia maelekezo ya daktari...unataka tuisogeze safari yako mpaka lini? Au unataka tuifute? Nikamwambia isogeze mpaka ijumaa! Mrema akasema hilo limefanyiwa kazi jomba...limeishaa!
Sasa ijumaa yenyewe leo bado sijakaa vizuri. Kwa ubora wa huduma waliyonipa nimeamua tu niiache hiyo tiketi na kumzawadia buree! Yaani atajua atafanyia nini! Mimi nikipona tu naingia Online nakata tiketi nyingine fastaaa! Shabiby ninyi mnatoa huduma kwa viwango vya kimataifa! Nimeanza kusafiri nanyi toka niko kidato cha kwanza na sijawahi kupata taabu
Meneja wa hii kampuni aongezewe mshahara mara mbili na apewe miaka mitano tena!