Shabiby, baadhi yetu tunazipenda huduma za magari yenu, kwanini hamna route ya Dar/Dom - Mwanza? Hamtutendei haki

Shabby "Live royal Travel Royal " hata ukikaaa site ya nyuma huwezi rushwarushwa kwenye matuta ya barabara madereva wako so smart. Huku wahudumu wanatoa maelekezo kama upo kwenye Ndege.
Mkuu sahihi kabisa. Tungepata hata kampuni tano tu kama Shabiby, nakwambia safari zingekuwa tamu sana bongo. Unasafiri kwa amani kabisa. Siyo hawa ndugu zetu wengine ambapo ukipabda magari yao inabidi roho ikae juu juu kama inataka kuchomoka.

Sijui kwanini matajiri wengi wa Bongo hawapendi ku-invest kwenye sector ya usafiri wa uhakika kama Shabiby.
 
Dar Mwanza panda happy nation wako vizuri
Mhh Mkuu safari ndefu kama hiyo huwa siunganishi. Mie huwa naikata. Dar - Dom, kisha kesho yake ndio naanza tena Dom-Mwanza.

Magari ya kuunganisha yanakuwa na speed za ajabu na usalama barabarani ni mdogo sana kutokana na kutaka kuokoa muda.
 
Kwa bongo mabasi ni
Shabby
ABC
Kilimanjaro
 
Hii ya AC kumwaga maji ndani inaonekana ni changamoto iliyomshinda mchina.

Apelekewe feedback juu ya hili.
 
Jamani Mwenye kujua usafiri wa uhakika, Dar to Bujumbura, Mbeya to Bujumbura, anijulishe na ghalama zao. Iwe usafiri wa bus.
 
Mhh Mkuu safari ndefu kama hiyo huwa siunganishi. Mie huwa naikata. Dar - Dom, kisha kesho yake ndio naanza tena Dom-Mwanza.

Magari ya kuunganisha yanakuwa na speed za ajabu na usalama barabarani ni mdogo sana kutokana na kutaka kuokoa muda.
Happy nation ni moja kwa moja nauli 50000 hutojutia ni mabasi mapya huduma zao zipo poa sana.Na ukichelewa kufanya booking mpaka sa 10 yote mawili utaambiwa yameshajaa.

Ally's star yupo njema ila hiyo mi bio huko njiani!!! Mana kipaumbele Chao kutokupitwa.
Nilitoka nalo mwanza kurudi dar kufika dodoma ikaanza kukimbizana na V9 na tukaiacha nikaona ohooo hii shida Sasa,dar tuliingia sa 5.
 
Kwa bongo mabasi ni
Shabby
ABC
Kilimanjaro
Hapa ongezea na BM.

Wanakuja moto sana japo Shabiby bado atabaki kuwa juu hasa kwenye kipengele cha "Customer Care, Service & Satisfaction".

Kumfananisha Shabiby na Ma-bus mengine si sawa. Ni kama umfananishe Mondy na Wasanii wengine.

Shabiby anaweza kwasababu ya Kuwekeza Kukubwa.

Tz: Elimu, Uzoefu na Kujizatiti kutakufanya utoboe.
 
Ally's iko vizuri Ila gia sio mchezo na wanakera wakifika shinyanga kushusha shusha Abiria yaan ni kero Sijui wanakwama wapi kupakia Abiria kulingana na route ya simiyu na Mwanza

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Haiendi huko tena, kwa sasa ni VIP dom - dar!!
Pamoja na magari ya Dom - Dar kuwa mengi ila hiyo route inaonekana inalipa sana. Ndio maana kuna magari mengi zaidi. Maana inashangaza, kwanini kusiwe na VIP kama Shabiby ya kutokea Dom -Mwanza? Au kwakuwa umbali umekuwa mrefu zaidi?
 
Umbali ulikuwa ni kigezo japo kwa sasa siyo hoja!

Uhitaji wa VIP dom - mwanza umekuwa mkubwa sana hivyo wamiliki watalifanyia kazi!!!
 
Umbali ulikuwa ni kigezo japo kwa sasa siyo hoja!

Uhitaji wa VIP dom - mwanza umekuwa mkubwa sana hivyo wamiliki watalifanyia kazi!!!
Hebu wahusika walifanyie kazi jambo hili. Safari ya Mwanza inawazisha sana kama hutopata gari nzuri.

Au watahofia Train ya standard gauge? Sidhani kama safari za Train zitakuwa za kila siku.
 
Hebu wahusika walifanyie kazi jambo hili. Safari ya Mwanza inawazisha sana kama hutopata gari nzuri.

Au watahofia Train ya standard gauge? Sidhani kama safari za Train zitakuwa za kila siku.
Hahaha wala hiyo train haizuii uwepo wa magari mazuri kwenye hiyo route!

Ni swala la mipango tu mkuu!
Huku kigoma tumekumbukwa tumeletewa luxury hata njia ya mwanza zitakuja tu.
 
Hahaha wala hiyo train haizuii uwepo wa magari mazuri kwenye hiyo route!

Ni swala la mipango tu mkuu!
Huku kigoma tumekumbukwa tumeletewa luxury hata njia ya mwanza zitakuja tu.
Duh. Hongereni sana. Kwa kuletewa luxury. Kwa sasa kuna barabara ya lami inaunganisha mikoa ya jirani na Kigoma? Nimewahi kuja Kigoma mwaka 2015. Kipindi hicho kulikuwa na vipande havijakamilika hasa kutokea Kaliua kuja Uvinza.
 
Panda ally's star [emoji93] usafir wangu pendwa dar to mwz
 
Panda ally's star [emoji93] usafir wangu pendwa dar to mwz
Ni nzuri Sana niliwahi kusema sipndi Tena walitukatia ticket kumbe gari inabeba wanafunz na wasiseme walitusumbua Sana ikabidi tuanze kuhangaika aisse nilifika dar alfajiri Ila ndo tunapnda tu tufanyaje[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…