Shafii Dauda anafaa kuadhibiwa kwa uchochezi

Shafii Dauda anafaa kuadhibiwa kwa uchochezi

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Akitoa maoni yake jana katika kipindi cha sports extra, alitilia shaka maamuzi ya kamati iliyoamua kuwajadili waamuzi na kuwalaumu kwa kushindwa kuumudu mchezo wa Simba na Yanga.

Akienda mbali zaidi kwa kusema eti maamuzi hayo yanachukuliwa kwa kuwa wajumbe wengi ni wapenzi wa Simba.Huu ni uchochezi na amekuwa akifanya fitina nyingi za namna hii dhidi ya Simba.

Anachokitafuta hatukijui lakini ajue ameshaeleweka msimamo wake dhidi ya Simba na si vizuri kuendelea kuprovoke wapenzi wa Simba kwa kutumia majungu pasipokuwa na sababu za kisayansi.

Hafai kuyafanya haya katika media kama Clouds.Anaweza akafanya haya katika blog yake tu.
 
Mpira wa TZ una stress nyingi burudani kidoogo

bora ulipie DSTV ufaidi EPL
Ukiwa na dstv utajiepusha na haya[emoji116] [emoji116]
1475683967729.jpg
 
Mkude alimdondosha mwamuzi kwa kumpuga mtama, then mwamuzi aliposimama akamlima red card, baada ya siku tatu kamati ya 'wahuni' inakaa na kuifuta red card na kumpa kalipio mwaluzi, tena bila hata kusoma report ya mechi ile......
Mkuu unaweza kusaidia kavideo kanakoonyesha hilo tukio, ili tujipange kukata rufaa?
 
Tuwe wakweli. TFF na Kamati zake ina udhaifu mkubwa katika kusimamia Ligi Kuu hapa nchini. Wenye makengeza nimekuwa nikiwasikia wakilalama kwamba TFF na Kamati zake inaibeba Yanga. Nashangaa. Hakuhitajiki hata miwani ya plastiki kibaini kwamba:
1. Maamuzi ya TFF na kamati zake ni ya kuabudu Timu tatu kubwa za Dar kwa kuziridhia matakwa yao hata kama ni kinyume na Sheria, kanuni na taratibu zinazotawala mpira wa miguu hapa nchini. Pale mmoja wapo anapobebwa, ndiyo wenzake wawili na washabiki wao ndio hulalamika kwamba mwenzao amebebwa.
2. Anayebisha kwamba Azam haibebwi aseme ruhusa ya kuacha Ligi Kuu na kwenda kucheza bonanza nje ya nchi huku akiwalazimishia wenzake viporo ni nini.
3. Anayebisha kwamba Yanga habebwi aseme nini maana ya hukumu ya Ngoma kumpiga kiwiko mchezaji wa Simba kwenye Ligi ya Msimu uliopita kutotolewa mpaka leo, na imeishia wapi.
4. Anayesema kwamba Simba haibebwi atueleze ilikuwaje kanuni ya mchezaji kuchagua mechi ya kuikosa baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ikatumika kabla ya kutangazwa na kuinufaisha Simba pekee, baada ya hapo mlango ukafungwa kwa komeo la chuma na ufunguo ukatoswa baharini. Au aeleze utamaduni wa kufuta kadi bila ya mhusika kuilalamikia umeanza lini hadi hii ya Mkude ikawa angalau ya pili.
Najua kuna wanaonishangaa sizungumzii magoli yanayolalamikiwa na Simba dhidi ya Yanga, lakini mwenye akili ya tafakuri hawezi kulihusisha hilo moja kwa moja na TFF na Kamati zake. Maana hata tukijaalia kuwa ni kweli waamuzi waliboronga kwa makusudi, huo kisheria ni ukorofi wao na si wa TFF na Kamati zake. Lakini anayenufaika na maamuzi yanayoaminika kuwa ni ya kiushikaji siyo Yanga peke yake. Ndio maana hata kwenye mechi hiyohiyo, Yanga nao wanalalamika kwamba mwamuzi aliliweka kwenye mizani pambano hilo mara tu baada ya nyekundu ya Mkude. Julio naye anawalalamikia waamuzi kwa kufungwa na Mbeya City. Na kadhalika. Ni dhambi kupuuza malalamiko ya timu nyengine dhidi ya waamuzi wanapocheza na isiyo Yanga, kwa sababu tu wao ni timu ndogo. Ama tuyape uzito malalamiko ya timu zote dhidi ya marefa uzito sawa na ya Simba dhidi ya Yanga, au yote tuyatupilie mbali.
Nionavyo, majigambo ya kijinga ya viongozi, wachezaji na wapenzi kabla ya michezo yao ndiyo chanzo kikuu cha dhana hii potofu ya timu kubebwa na TFF ilhali hata kama madai ya ubebaji yakithibitika bado hayatoshi kuhitimisha kwamba yamefanywa na TFF na kamati zake. Kusingizia marefa ni mbinu ovu ya wanamajigambo hawa kutawala kushindwa (defeat management) kwao kwenye mechi waliyotangulia kuisema kwamba ' tutashinda kwa hali yoyote, tutawafunga watake wasitake, wapenzi wasiwe na hofu, hakuna timu ya kutufunga, nani kama timu yetu?, wao ni wateja wetu tu, tuna uhakika wa pointi tatu' n.k. Msemaji wa timu hiyo anapoambulia kipigo ama sare huishia kutafuta kisingizio ili asihojiwe kushindwa kwa majigambo yake. Ndio maana makocha wasio tabia hii huwasikii kulalamika hivyo. Kocha wa Burnley hakujigamba kwamba lazima angeifunga Arsenal ndio maana walipofungwa goli linaloweza kuwa kweli la mkono hawakun'goa viti uwanjani.
Ni upuuzi kudhani mechi zetu kuchezeshwa na marefa wa nje ndio kutaondoa ghasia za aina hii viwanjani, kama kudhani kwamba tunahitaji wageni kuongoza Kamati zetu za Uchaguzi ndio malalamiko ya kuibiwa kura yataondoka. Tunachohitaji ni wadau wa timu zetu kujitambua, na kwamba kufungwa siyo lazima maana yake iwe ni ubovu wa timu, na kwamba hakuna timu isiyofungwa, na kwamba waamuzi ni wanadamu na kwa hivyo kukosea kwao ni lazima, na kwamba hakuna namna ya kubadilisha maamuzi ya refa ukiwa ndani au nje ya uwanja, na kwamba mpira haujafikia uadilifu wa kuwa kila anayestahiki ndiye anayefanikiwa kwa mujibu wa anavyostahiki, na kwamba wachezaji nao ni wanadamu na kwa hivyo lazima watakosea mara nyengine hata kusababisha timu kufungwa, na kwamba mpira ni mchezo wa kistaarabu usiohitaji hasira.
 
Nadhan wakati huu ni muda muafaka kabisa kwa tff ya malinzi kuzifumua hizi kamati kwa kuwaondoa ma-simba na ma yanga wanaosababisha 'fujo' na kupindisha maamuzi ya hizo kamati kwani wanajulikana
 
Nadhan wakati huu ni muda muafaka kabisa kwa tff ya malinzi kuzifumua hizi kamati kwa kuwaondoa ma-simba na ma yanga wanaosababisha 'fujo' na kupindisha maamuzi ya hizo kamati kwani wanajulikana
Tatizo hauwezi kupata viongozi wa soka ambaye sio Simba au Yanga...
 
Nilishangaa juzi Julio kustaafu mpira kwa ubabaishaji wa waamuzi,hapa sio waamuzi tu shida iko pale TFF
Ngoja niendelee kufurahia maisha mwaka wa nne sasa sishabikii kitu kinachoitwa mpira wa Tanzania hata timu ya Taifa.....maana niliona napata stress zisizo na maana bila sababu.....eti Simba mara Yanga....siku hizi si kuna Azamu...ni ujinga mtupu!!!
 
Hivi Julio aliwacha kufundisha ndani ya Ligi ipi vile - EPL au La Liga?
 
Mi nilikuwa nakazia tu kwamba mpira wa Tanzania ni pasua kichwa ni maumivu yaani hata Julio alichelewa kustaafu kwa maono yangu mwangalingimungu
 
Akitoa maoni yake jana katika kipindi cha sports extra, alitilia shaka maamuzi ya kamati iliyoamua kuwajadili waamuzi na kuwalaumu kwa kushindwa kuumudu mchezo wa Simba na Yanga.

Akienda mbali zaidi kwa kusema eti maamuzi hayo yanachukuliwa kwa kuwa wajumbe wengi ni wapenzi wa Simba.Huu ni uchochezi na amekuwa akifanya fitina nyingi za namna hii dhidi ya Simba.

Anachokitafuta hatukijui lakini ajue ameshaeleweka msimamo wake dhidi ya Simba na si vizuri kuendelea kuprovoke wapenzi wa Simba kwa kutumia majungu pasipokuwa na sababu za kisayansi.

Hafai kuyafanya haya katika media kama Clouds.Anaweza akafanya haya katika blog yake tu.
HII NDIO KAMATI YA MASAA 72 ILIYOBATILISHA KADI NYEKUNDU YA JONAS MKUDE NA KUMFUMGIA MARTIN SANYA MIAKA. 2

WAJUMBE
1. MSAFIRI MGOYI (SIMBA) kamati utendaji tff
2.SALUM CHAMA (SIMBA)M/kit chama cha marefa
3.STEVIN MGUTO (SIMBA)mjumbe bodi ya ligi
4. SAID MOHAMED (SIMBA)makam mwenyeki bodi ya ligi
5.BARUHANI MUHUZA (SIMBA)mjube
6.BONIFAS WAMBURA (SIMBA) C.E O. bodi ya ligi
7.JONAS KIWIA (SIMBA)Mkurugenzi wa mashindano tff
8.JOEL BALISIDYA (SIMBA)Afsa wa ligi bodi ya ligi
9.FATMA ABDALLAH (SIMBA) ofice maneger bodi ya ligi
10. CHARLES NDAAGALA (YANGA) katibu chama cha marefa
11.PHELEMON NTAHILAJA (YANGA) mjube
12.ROSE MSAMILA (YANGA) Asst afsa wa ligi bod ya ligi
13.MACHAEL NGOGO (AIJULIKANI) Asst afsa wa ligi bodi ya ligi

Hawa ndio wajumbe walishiriki kikao cha maamuz yaliyo fanyika jana na kwa uhuwiano huu mlitegemea nn kama sio kutoa maamuzi ya ajabu ya kufuta kadi ya mkude na mengine ya siyo faa ili kuwaaminisha wana simba kwamba kweli walionewa katka mchezo uliomalizika kwa sare ya moja moja
1475698807565.jpg
 
HII NDIO KAMATI YA MASAA 72 ILIYOBATILISHA KADI NYEKUNDU YA JONAS MKUDE NA KUMFUMGIA MARTIN SANYA MIAKA. 2

WAJUMBE
1. MSAFIRI MGOYI (SIMBA) kamati utendaji tff
2.SALUM CHAMA (SIMBA)M/kit chama cha marefa
3.STEVIN MGUTO (SIMBA)mjumbe bodi ya ligi
4. SAID MOHAMED (SIMBA)makam mwenyeki bodi ya ligi
5.BARUHANI MUHUZA (SIMBA)mjube
6.BONIFAS WAMBURA (SIMBA) C.E O. bodi ya ligi
7.JONAS KIWIA (SIMBA)Mkurugenzi wa mashindano tff
8.JOEL BALISIDYA (SIMBA)Afsa wa ligi bodi ya ligi
9.FATMA ABDALLAH (SIMBA) ofice maneger bodi ya ligi
10. CHARLES NDAAGALA (YANGA) katibu chama cha marefa
11.PHELEMON NTAHILAJA (YANGA) mjube
12.ROSE MSAMILA (YANGA) Asst afsa wa ligi bod ya ligi
13.MACHAEL NGOGO (AIJULIKANI) Asst afsa wa ligi bodi ya ligi

Hawa ndio wajumbe walishiriki kikao cha maamuz yaliyo fanyika jana na kwa uhuwiano huu mlitegemea nn kama sio kutoa maamuzi ya ajabu ya kufuta kadi ya mkude na mengine ya siyo faa ili kuwaaminisha wana simba kwamba kweli walionewa katka mchezo uliomalizika kwa sare ya moja mojaView attachment 412872

Umemsahau na Mjumbe mwingine muhimu sana MWIGULU NCHEMBA ( YANGA ) Kiongozi wa Hakikisha Yanga inashinda kwa gharama yoyote ile nchini.
 
Akitoa maoni yake jana katika kipindi cha sports extra, alitilia shaka maamuzi ya kamati iliyoamua kuwajadili waamuzi na kuwalaumu kwa kushindwa kuumudu mchezo wa Simba na Yanga.

Akienda mbali zaidi kwa kusema eti maamuzi hayo yanachukuliwa kwa kuwa wajumbe wengi ni wapenzi wa Simba.Huu ni uchochezi na amekuwa akifanya fitina nyingi za namna hii dhidi ya Simba.

Anachokitafuta hatukijui lakini ajue ameshaeleweka msimamo wake dhidi ya Simba na si vizuri kuendelea kuprovoke wapenzi wa Simba kwa kutumia majungu pasipokuwa na sababu za kisayansi.

Hafai kuyafanya haya katika media kama Clouds.Anaweza akafanya haya katika blog yake tu.

Shafii Dauda kuna anachikotafuta Simba na atakipata tu muda si mrefu.
 
Mkude alimdondosha mwamuzi kwa kumpuga mtama, then mwamuzi aliposimama akamlima red card, baada ya siku tatu kamati ya 'wahuni' inakaa na kuifuta red card na kumpa kalipio mwaluzi, tena bila hata kusoma report ya mechi ile......
Sio kweli. Nenda you tube tazama. Jamaa hakumgusa wala. Refa ni muhuni sana
 
Back
Top Bottom