Shahidi adai Padri Rwegoshora aliahidi kumpa V8 baba wa Mtoto Albino 'Asimwe'

Shahidi adai Padri Rwegoshora aliahidi kumpa V8 baba wa Mtoto Albino 'Asimwe'

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath (2) umewasilisha maelezo ya ushahidi katika hatua ya awali, ukieleza utakuwa na mashahidi 52 na vielelezo 37.

Katika maelezo hayo ya ushahidi, mmoja wa mashahidi ameeleza mbinu iliyotumiwa na washtakiwa kumpora mtoto huyo na kutokomea, pia ikitajwa ahadi ya gari aina ya Toyota V8, maarufu kama shangingi, kwa baba wa mtoto.

Asimwe aliporwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwao Kijiji cha Bulamula, Kata ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera, Mei 30, 2024 saa 2:00 usiku na kutokomea naye kusikojulikana.

Siku 17 baadaye mabaki ya mwili wake yalipatikana yakiwa yamefungwa kwenye mfuko wa sandarusi (kiroba) na kutelekezwa chini ya kalavati lililoko Barabara ya Makongora, Kitongoji Kabyonda, Kata ya Ruhanga wilayani humo.

Pia Soma:

- Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath


Siku kadhaa baadaye, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kuwashikilia watu tisa akiwemo baba wa marehemu, Novath Venanth na Padri Elpidius Rwegoshora na kuwafungulia kesi ya mauaji namba 17740/2024, katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani humo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nurdini Masudi, Ramadhani Selestine, Rweyangira Alphonce, Dastan Bruchard, Faswiu Athuman, Gozbert Alikad na Desdery Everigist wote wakazi wa mkoani Kagera.
 
Katibu wa baraza la maaskofu anasubiri nini kutoa tamko kuhusu huyo padiri? Huenda anaona sawa tu! Ni aibu kwa kanisa.
 
Hawa watawa utaka pesa za nini ilhali hawana watoto na uhudumiwa na Kanisa Maisha yao yote!!.

Muulizie Cardinal Mstaafu, na maaskofu wenzake na zile seminary za malezi. Injili mpya ilikuwa excommunication ya wabaya wake badala ya kuimarisha malezi na umahiri wa mapadri na wafanyakazi ndani ya kanisa.
Corruption is everywhere. Kuanzia chini kabisa mpaka juu. Inaogopesha kweli
 
Back
Top Bottom