Shahidi adai Padri Rwegoshora aliahidi kumpa V8 baba wa Mtoto Albino 'Asimwe'

Suala siyo dhambi kufanyika au la. Shida ni kanisa kushiriki kuwaficha mabaladhuli wanaowalawiti watoto. Kwa miongo mingi, kanisa lilizima tuhuma za mapadri na watawa wengine za kuwanajisi watoto. Mpaka vyombo vya kimataifa vilipo ingilia kati ndipo Papa akaomba msamaha kwa wahanga wote.

Kanisa limemficha nani? Huyo Padro amevuliwa upadri na ameshitakiwa. Mbona ukatoliki unawahangaisha sana? Ukatoliki sio mali ya mtu kama mnavyodhani. Ndio maana unaendelea kuwepo na utakuwepo mpaka ukamilifu wa dahali.
 
Kitendo cha padre kutiwa hatianI kwa kosa la mauaji, huo ni udhalilishaji mkubwa kwa kanisa katoliki
Umeshasahau mara hii kuna mashehe wa uamsho walishakuwa na kesi ya ugaidi, wakaachiwa kwa msamaha??
 
'Mwenye jina la kiarabu ndio mchinjaji na wenye majina ya kigalatia ndio washikilia miguu na mikono' Nawaza tu kwa sauti ila hizi dini ni za kwenda nazo kwa akili sana. Hakuna kumwamwini padre wala shekhe kushinda na wanao.
 
Upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath (2) umewasilisha maelezo ya ushahidi katika hatua ya awali, ukieleza utakuwa na mashahidi 52 na vielelezo 37.

Katika maelezo hayo ya ushahidi, mmoja wa mashahidi ameeleza mbinu iliyotumiwa na washtakiwa kumpora mtoto huyo na kutokomea, pia ikitajwa ahadi ya gari aina ya Toyota V8, maarufu kama shangingi, kwa baba wa mtoto.

Asimwe aliporwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwao Kijiji cha Bulamula, Kata ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera, Mei 30, 2024 saa 2:00 usiku na kutokomea naye kusikojulikana.

Siku 17 baadaye mabaki ya mwili wake yalipatikana yakiwa yamefungwa kwenye mfuko wa sandarusi (kiroba) na kutelekezwa chini ya kalavati lililoko Barabara ya Makongora, Kitongoji Kabyonda, Kata ya Ruhanga wilayani humo.

Pia Soma:

- Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Siku kadhaa baadaye, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kuwashikilia watu tisa akiwemo baba wa marehemu, Novath Venanth na Padri Elpidius Rwegoshora na kuwafungulia kesi ya mauaji namba 17740/2024, katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani humo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nurdini Masudi, Ramadhani Selestine, Rweyangira Alphonce, Dastan Bruchard, Faswiu Athuman, Gozbert Alikad na Desdery Everigist wote wakazi wa mkoani Kagera.
Hawa watawa utaka pesa za nini ilhali hawana watoto na uhudumiwa na Kanisa Maisha yao yote!!.
Ushahidi usio wa kweli huu.
Huu ni uthibitisho wa wazi kabisa kwamba Kesi hii ni ya kupikwa, wala haina ukweli wowote ule.
 
Attachments

  • Screenshot_20240803_182210_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20240803_182210_WhatsApp.jpg
    194.8 KB · Views: 1
Upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath (2) umewasilisha maelezo ya ushahidi katika hatua ya awali, ukieleza utakuwa na mashahidi 52 na vielelezo 37.

Katika maelezo hayo ya ushahidi, mmoja wa mashahidi ameeleza mbinu iliyotumiwa na washtakiwa kumpora mtoto huyo na kutokomea, pia ikitajwa ahadi ya gari aina ya Toyota V8, maarufu kama shangingi, kwa baba wa mtoto.

Asimwe aliporwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwao Kijiji cha Bulamula, Kata ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera, Mei 30, 2024 saa 2:00 usiku na kutokomea naye kusikojulikana.

Siku 17 baadaye mabaki ya mwili wake yalipatikana yakiwa yamefungwa kwenye mfuko wa sandarusi (kiroba) na kutelekezwa chini ya kalavati lililoko Barabara ya Makongora, Kitongoji Kabyonda, Kata ya Ruhanga wilayani humo.

Pia Soma:

- Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Siku kadhaa baadaye, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kuwashikilia watu tisa akiwemo baba wa marehemu, Novath Venanth na Padri Elpidius Rwegoshora na kuwafungulia kesi ya mauaji namba 17740/2024, katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani humo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nurdini Masudi, Ramadhani Selestine, Rweyangira Alphonce, Dastan Bruchard, Faswiu Athuman, Gozbert Alikad na Desdery Everigist wote wakazi wa mkoani Kagera.
Baba mpumbavu iyo v8 angeiendesha kwa madako yake , samahi mod ,tumia neno gum ,nimejikuta nipo na hasira sana aisee
 
Na mazuri mangapi wameshiriki pia? Kuna matatizo yaliyoletwa na watu. Kuna mazuri yaliyoletwa na watu pia. Msijisahaulishe

Ni sawa kuna mazuri, lakni mazuri yao hayawezi kufuta mabaya yao, vivyo hivyo mabaya yao hayawezi kufuta mazuri yao. Ila penye ukweli, lazima tuseme. Kanisa katoliki lilificha ukweli kuhusu watawa walio wanajisi watoto.
 
Kanisa limemficha nani? Huyo Padro amevuliwa upadri na ameshitakiwa. Mbona ukatoliki unawahangaisha sana? Ukatoliki sio mali ya mtu kama mnavyodhani. Ndio maana unaendelea kuwepo na utakuwepo mpaka ukamilifu wa dahali.

Mbona unajibu kwa mihemko ivoo
Fuatilia uone jinsi papa alivyoomba msamaha kwa maadhila yaliyosababishwa na watawa.
 
Back
Top Bottom