Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Katika hali isiyotarajiwa, shahidi wa tatu kwenye kesi inayomkabili Zephania Ndalawa anayeshtakiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia, amemtambua Jaji Graffin Mwakapeje kama mtuhumiwa wa mauaji ya Thomas Masumbuko.
Shahidi huyo, Salome Cheyo (9) akiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Musa Mlawa alipotakiwa kwenda kumuonyesha mtuhumiwa kama anamkumbuka, alitoka kizimbani na kwenda hadi alipo jaji na kumuonyesha kuwa ndiye.
Hata aliposhuka kutoka alipo jaji na kurudi kizimbani na Wakili Mlawa kumuuliza tena kuhusu mtu mweupe aliyemfukuza siku ya tukio, mtoto huyo aliendelea kusisitiza ni jaji anayeendesha kesi hiyo, jambo lililozua vicheko mahakamani hapo.
Shahidi huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Burigi, alikuwa anatoa ushaidi wa tukio la mauji ya Thomas Masumbuko (12), jana Alhamisi Julai 3, 2024.
Masumbuko aliuawa kwa kufungwa kamba mguuni, mikono na kusokomezwa matambara mdomoni, hivyo kukosa hewa na kufariki dunia, huku akiwa amefunikwa kitambaa usoni.
Shahidi huyo akiwa kizimbani, Jaji alimhoji maswali ya ufahamu ili aweze kuapishwa, ikiwa ni pamoja na kumuuliza majina, dini na kama anajua nini maana ya dhambi au ukweli, maswali ambayo alishindwa kuyajibu kwa ufasaha.
Kutokana na kushindwa kujieleza, nini maana ya uongo au ukweli, Mahakama iliridhia shahidi huyo achukuliwe ushahidi wake bila kiapo.
Mwananchi