Shahidi Muhimu wa Kesi ya Albert Ojwang Afariki Kabla ya Kusema Alichokuwa Anajua

Shahidi Muhimu wa Kesi ya Albert Ojwang Afariki Kabla ya Kusema Alichokuwa Anajua

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Kesi ya mauaji ya blogger na mwalimu Albert Ojwang imepata mgeuko mwingine baada ya afisa wa polisi aliyekuwa protected witness kufariki kabla hajatoa ushahidi wake mahakamani.

Stephen Maina Nderitu, aliyekuwa akifanya kazi katika ofisi ya OCS katika Central Police Station, alifariki Jumatatu, Septemba 7, baada ya kuripotiwa kuanguka muda mfupi baada ya kutoka kazini. Postmortem imetaja acute ulcers, cardiac arrest na depression katika sababu za kifo chake. Kwa sasa, hakuna ushahidi wa umma unaohusisha kifo chake na kesi ya Ojwang.

Lakini umuhimu wake kwenye kesi ndio unaozua maswali.

Wachunguzi walikuwa wamemtambua Nderitu kama shahidi ambaye angeweza kutoa taarifa kuhusu kile kilichotokea katika Central Police Station na kusaidia kueleza madai ya kuingiliwa kwa CCTV hard drive baada ya kifo cha Ojwang.

IPOA tayari ilibaini mwaka 2025 kuwa mfumo wa CCTV katika ofisi ya OCS ulikuwa umeingiliwa; power cable ya DVR ilikuwa imetolewa na records zilionesha discs zilikuwa zimebadilishwa na kufanyiwa formatting.

Mahakama pia tayari imesikia ushahidi kutoka kwa mashahidi wengine kuhusu footage inayodaiwa kufutwa. Mmoja wa protected witnesses alidai alielekezwa ku-format DVR, huku shahidi mwingine akieleza kile alichokiona kwenye CCTV kabla recordings kutoweka. Washtakiwa wote wamekana mashtaka yanayowakabili.
 

Attachments

  • IMG-20260910-WA0002-1788988722.jpg
    IMG-20260910-WA0002-1788988722.jpg
    69 KB · Views: 20
Back
Top Bottom