Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Hii inaitwa kukurupuka na kukosa watu walio serious kwenye uandaaji na utetezi wa kesi ya jinai. Kwa mahakama zilizo huru na ambazo zinajitegemea kilichofanywa na shahidi wa pili kinatosha kumfunga au kutaka Chama cha mapinduzi kinachotuhumiwa kutumia Polisi na wanachama wa chama hicho kuidanganya mahakama kufika mahakamani kujieleza kuhusu utata uliojitokeza juu ya ushahidi unaoendelea.
Katika ushahidi uliotolewa shahidi huyu wa pili amekana kutokuwa na affiliation na chama cha siasa. Lakini jamii au public ambayo inamjua shahidi imesambaza Taarifa zake zinazothibitisha kuwa alikuwa kada wa CCM.
Jambo la pili shahidi huyu imethibitika kwamba alikuwa mwajiriwa wa Sabaya lakini walihitilafiana kisha akakamatwa na kubambikiwa kesi ambayo baadaye ilifutwa. Leo anasimama mahakamani kusema kwamba alishirikishwa na Mbowe kumdhuru Sabaya. Huu ni ukakasi wa pili kuhusu credibility ya mahakama kumruhusu mtu Kama huyu kusimama mbele ya Jaji akajitungia. Story.
Lakini kwa kiburi baada ya kuona ushahidi wake unakinzana na ukweli wa akaunti yake ya Facebook amedelete akaunti hiyo. Je, hao waliompanga walishindwa kupitia hata account zake za mitandao ya kijamii kuona zinavyoweza kuathiri kesi jhii hadi anafika kutoa ushahidi? Huu uzembe mkubwa hivi unaashiria nn kuhusu umakini wa vyombo vya dola?
Lakini pia huyu bwana aliajiriwa kuwa msaidizi wa katibu wa CCM longido na hata alipohitilafiana na Sabaya alirejea huko, je huko alikoajiriwa mwajiri alimwajiri mtu aliyekinyume na itikadi ya chama ?
Ila pia uhusika wa Pole pole, Bashiru, Gambo na Dagaro unamtenganisha vipi na chama Tawala?
Kitu chakushangaza wakati anakamatwa alikutwa na dola zakutosha na tshs zakutosha ambazo anadai alitoka kuuza mbogamboga lakini mtu huyo anayetembea na zaidi ya milioni mbili mfukoni anasema alikuwa akipewa shs elfu hamsini na Mbowe.......huu ugaidi huu
Hii Ni fedhea nyingine kwa mahakama na Serikali ,tengenezeni mambo yenye logic siyo watu wa aina hii ambao wamekaririshwa.