Shahidi wa pili kesi ya Mbowe, Bw. Kaaya afunga akaunti ya facebook baada ukweli kuhusu uachama wake wa CCM kuwekwa wazi mitandaoni

Shahidi wa pili kesi ya Mbowe, Bw. Kaaya afunga akaunti ya facebook baada ukweli kuhusu uachama wake wa CCM kuwekwa wazi mitandaoni

Wanachama wa CCM siku hizi wapo kwenye database. Ni rahisi kuprove uanachama wake kidigitali, siyo kama zamani kadi inatoka kianaligia.
Then wanasheria wa utetezi watafute ushahidi kuonesha kama ni mwanachama, wakiweza hilo then ushahidi wake utatupiliwa mbali na yeye atashitakiwa kwa kuidanganya mahakama
 
We mfuasi wa kampuni ya Mbowe acha kuangaika usiku...mbowe atafungwa tu ni guide yule...mnakosea mnapo tafsiri hili swala la mbowe kisiasa...mbona ushahidi upo wazi sana kuliko hata zile kesi za Sabaya za kuunga unga ushahidi
Tour guide ama guide wa nini?
 
CCM hawajui hata kumkaririsha shahidi uongo akautoe mahakamani nayo ni kazi inayohitaji uzoefu.

Pia walimu wao wakukaririsha nao hawajielewi hawajui kuna mambo ya kufuatilia nje ili kuondoa uwezekano wa mgongano kati ya kile atachoongea shahidi na uhalisia wa maisha yake mtaani.

Huy
Wewe kumbuka ulivyokua shuleni ukikariri ukifika kwenye mtihani inakuaje pale swali limeenda kinyume kidogo tu.
 
Ni guide au gaidi? ubongo wako umejaa kamasi
We mfuasi wa kampuni ya Mbowe acha kuangaika usiku...mbowe atafungwa tu ni guide yule...mnakosea mnapo tafsiri hili swala la mbowe kisiasa...mbona ushahidi upo wazi sana kuliko hata zile kesi za Sabaya za kuunga unga ushahidi
 
Hii inaitwa kukurupuka na kukosa watu walio serious kwenye uandaaji na utetezi wa kesi ya jinai. Kwa mahakama zilizo huru na ambazo zinajitegemea kilichofanywa na shahidi wa pili kinatosha kumfunga au kutaka Chama cha mapinduzi kinachotuhumiwa kutumia Polisi na wanachama wa chama hicho kuidanganya mahakama kufika mahakamani kujieleza kuhusu utata uliojitokeza juu ya ushahidi unaoendelea.

Katika ushahidi uliotolewa shahidi huyu wa pili amekana kutokuwa na affiliation na chama cha siasa. Lakini jamii au public ambayo inamjua shahidi imesambaza Taarifa zake zinazothibitisha kuwa alikuwa kada wa CCM.

Jambo la pili shahidi huyu imethibitika kwamba alikuwa mwajiriwa wa Sabaya lakini walihitilafiana kisha akakamatwa na kubambikiwa kesi ambayo baadaye ilifutwa. Leo anasimama mahakamani kusema kwamba alishirikishwa na Mbowe kumdhuru Sabaya. Huu ni ukakasi wa pili kuhusu credibility ya mahakama kumruhusu mtu Kama huyu kusimama mbele ya Jaji akajitungia. Story.

Lakini kwa kiburi baada ya kuona ushahidi wake unakinzana na ukweli wa akaunti yake ya Facebook amedelete akaunti hiyo. Je, hao waliompanga walishindwa kupitia hata account zake za mitandao ya kijamii kuona zinavyoweza kuathiri kesi jhii hadi anafika kutoa ushahidi? Huu uzembe mkubwa hivi unaashiria nn kuhusu umakini wa vyombo vya dola?

Lakini pia huyu bwana aliajiriwa kuwa msaidizi wa katibu wa CCM longido na hata alipohitilafiana na Sabaya alirejea huko, je huko alikoajiriwa mwajiri alimwajiri mtu aliyekinyume na itikadi ya chama ?

Ila pia uhusika wa Pole pole, Bashiru, Gambo na Dagaro unamtenganisha vipi na chama Tawala?

Kitu chakushangaza wakati anakamatwa alikutwa na dola zakutosha na tshs zakutosha ambazo anadai alitoka kuuza mbogamboga lakini mtu huyo anayetembea na zaidi ya milioni mbili mfukoni anasema alikuwa akipewa shs elfu hamsini na Mbowe.......huu ugaidi huu

Hii Ni fedhea nyingine kwa mahakama na Serikali ,tengenezeni mambo yenye logic siyo watu wa aina hii ambao wamekaririshwa.
Kama mnaona shahidi hafai siuende wewe. Yaani unajiona unaweza ujaji... Mbowe ni gaidi na atafungwa nyie endeleeni kuupiga....
 
We mfuasi wa kampuni ya Mbowe acha kuangaika usiku...mbowe atafungwa tu ni guide yule...mnakosea mnapo tafsiri hili swala la mbowe kisiasa...mbona ushahidi upo wazi sana kuliko hata zile kesi za Sabaya za kuunga unga ushahidi
ni gaidi au guide
 
Alisema siyo mwanachama, hakusema siyo mkereketwa!! Kama kadanganya ni kazi ya mawakili wa utetezi kuprove, ila huwezi kuprove uanachama wa mtu kwa sababu kavaa nguo za chama fulani cha siasa kwenye social medias! unaweza kuwa mkereketwa na siyo mwanachama pia!

Mbele ya sheria Mbowe na Sabaya wote ni sawa, hamna mwenye haki zaidi ya mwenzake kwenye jicho la sheria, mambo ya huyu ni muhalifu or siyo tunayajua sisi huku mtaani! Rekodi ya uhalifu inasaidia tu kupewa minimum/maximum adhabu pale unapokamatwa na kosa!

Kwa hiyo wewe unaamini yote aliyosema shahidi jana ni uongo??? And unaamini pia ukishakuwa na rekodi ya uhalifu basi watu wako wa karibu hawawezi kuwa mashahidi wa upande wako?? Acha ushabiki Chief
Whatever the case, kama alisema sio mwanachama lakini ana nguo ya kijani maana yake nini? ni mkereketwa, kwa hiyo hata kama hakusema yeye ni mkereketwa lakini huo ndio ukweli, kuwa mkereketwa ni sawa na kuwa shabiki, kama shabiki wa Simba anavyovaa jezi ya timu yake lakini hana kadi ya uanachama wa klabu yake, nakufundisha uelewe sio kubisha bisha tu.

Kuhusu Mbowe na Sabaya, Mbowe mpaja sasa ni mtuhumiwa, Sabaya ni mfungwa baada ya kukutwa na hatia, hawa wawili hawafanani, usihangaike kuwalinganisha, sheria haiwezi kuwalinda watu wenye status isiyofanana, huyo Sabaya sasa hivi analindwa na sheria za magereza, kama kulala saa 9 alasiri.

Pia, kuhusu kumuamini mtu aliyewahi kufanya kazi na jambazi mimi siwezi, kwasababu inafahamika ulimwenguni kote, "birds of the same feather fly together" usiponielewa hapo tafuta mwalimu mwingine.
 
Whatever the case, kama alisema sio mwanachama lakini ana nguo ya kijani maana yake nini? ni mkereketwa, kwa hiyo hata kama hakusema yeye ni mkereketwa lakini huo ndio ukweli, kuwa mkereketwa ni sawa na kuwa shabiki, kama shabiki wa Simba anavyovaa jezi ya timu yake lakini hana kadi ya uanachama wa klabu yake, nakufundisha uelewe sio kubisha bisha tu.

Kuhusu Mbowe na Sabaya, Mbowe mpaja sasa ni mtuhumiwa, Sabaya ni mfungwa baada ya kukutwa na hatia, hawa wawili hawafanani, usihangaike kuwalinganisha.
Ishu ni wewe kusema kadanganya yeye siyo mwanachama, kuvaa nguo za CCM haimaanishi wewe ni mwanachama wa CCM! Wanasheria wenu sasa wakaprove kuwa jamaa kadanganya yeye siyo mwanachama, siyo kuleta bla bla za picha za fb
 
Wewe kumbuka ulivyokua shuleni ukikariri ukifika kwenye mtihani inakuaje pale swali limeenda kinyume kidogo tu.
Huyo shahidi akili fupi, sioni sababu yake kuogopa wakati jaji na yeye ni timu moja.
 
Ishu ni wewe kusema kadanganya yeye siyo mwanachama, kuvaa nguo za CCM haimaanishi wewe ni mwanachama wa CCM! Wanasheria wenu sasa wakaprove kuwa jamaa kadanganya yeye siyo mwanachama, siyo kuleta bla bla za picha za fb
Alisema aliwahi kujihusisha na siasa na wanasiasa au hajawahi?

Mwenzio kafunga akaunti ya fb kwasababu anajua dhamira imemshtaki, wewe unaleta sound hapa.
 
Hii kesi yaweza kuwa kesi rejewa vyuoni. Sijui itakuwaje kwa wanafunzi tarajali watakapokuwa wainaifanyia marejeo
Nimemkataza Binti yangu asisome sharia, ni ujinga mtupu! Ataenda kufanya Health acha akawe Doctor tu
 
Ishu ni wewe kusema kadanganya yeye siyo mwanachama, kuvaa nguo za CCM haimaanishi wewe ni mwanachama wa CCM! Wanasheria wenu sasa wakaprove kuwa jamaa kadanganya yeye siyo mwanachama, siyo kuleta bla bla za picha za fb
Ndio nasikia hili Leo kutoka kwako! Mnapinga mambo kiboya sana sana

IMG-20211027-WA0037.jpg
 
Sioni haja ya wafuasi wa gaidi Mbowe kulialia humu,yule hatoboi,ambieni ndugu zake waanze matanga
 
CCM imepofushwa na Mungu ili nchi ikombolewe
nchi huru unasema ikombolewe na nani ? nchi gani inaweza kukombolewa mara mbili yaani mnajisumbua tu ushahidi uko wazi kabisa mbowe ametenda makosa wala msikomaze shingo ni muda tu unasubiriwa hukumu itoke na huyo wakili wenu anayejifanya msomi kibatala ndiyo anaichelewesha kwa maslahi yake binafsi kufungua vikesi vidogovidogo anawalisha maneno watuhumiwa kudanganya mahakama lakini jaji akawasitukia akatupilia mbali ndiyo maana kibatala hakubisha maana ajua alichokifanya kimegundulika mashahidi wameshamkaanga mbowe vyakutosha hachomoki hapo
 
Alisema aliwahi kujihusisha na siasa na wanasiasa au hajawahi?

Mwenzio kafunga akaunti ya fb kwasababu anajua dhamira imemshtaki, wewe unaleta sound tu hapa.
Kuna mtu asiyejihusisha na siasa? Ishu ni moja tu, ni mwanachama or siyo mwanachama? Kujihusisha na chama fulani haimaanishi wewe ni mwanachama wa chama hicho! And kuwa mwanachama wa chama fulani haikunyimi haki ya kuwa shahidi wa kesi ambayo hiko chama kinahusishwa, ndiyo maana kuna kuapa na kuhojiwa na mawakili wa pande zote mbili! Ni kazi ya mawakili wenu "akili kubwa" kudhibitisha uongo wake
 
Back
Top Bottom