CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Chama kinachotetea masilahi ya wanyonge wote bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini cha Mapinduzi kimewataka wakuu wote wa Mikoa, Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuhakikisha wanalinda maslahi ya wananchi wanaofanyakazi na wakandarasi kama watoa huduma.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Mhe Shaka Hamdu Shaka wilayani Kaliua mkoa wa Tabora. Shaka ametoa kauli hii baada ya kusimamishwa wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Ushokora pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Mama mmoja alitoa malalamiko yake mbele ya Shaka, akimuomba amsaidie kupata haki yake kutoka kwa Mkandarasi(jina linahifadhiwa) ambaye baada ya kandarasi yake kusitishwa na halmashauri akaondoka na deni la mama huyo, kitendo ambacho kimemfanya kufilisika kibiashara.
Akiongea kwa uchungu Shaka amewataka waliopewa dhamani wasimamie masilahi ya watoto hawa wa masikini wanaorudishwa nyuma kwa faida za watu walioshindwa majukumu yao.