The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Hili jambo halipo Kwa hao Ma DED na Ma DC pekee hata Kwa wakandarasi wengine wanaopewa Kazi na taasisi zingine kama TanRoads na Tarura nk hawasimamii maslahi ya wafanyakazi wa hizo kampuni kwa sababu wanapewa vihela na wakandarasi..View attachment 2327010
Chama kinachotetea masilahi ya wanyonge wote bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini cha Mapinduzi kimewataka wakuu wote wa Mikoa, Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuhakikisha wanalinda maslahi ya wananchi wanaofanyakazi na wakandarasi kama watoa huduma,
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Mhe Shaka Hamdu Shaka wWlayani Kaliua mkoa wa Tabora,
Shaka ametoa kauli hii baada ya kusimamishwa wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Ushokora pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Mama mmoja alitoa malalamiko yake mbele ya Shaka akimuomba amsaidie kupata haki yake kutoka kwa Mkandarasi (jina linahifadhiwa ) ambaye baada ya kandarasi yake kusitishwa na Halmashauri akaondoka na deni la mama huyo, kitendo ambacho kimemfanya kufilisika kibiashara.
Akiongea kwa uchungu Shaka amewataka waliopewa dhamani wasimamie masilahi ya watoto hawa wa masikini wanaorudishwa nyuma kwa faida za watu walioshindwa majukumu yao,
Hii tabia ya kuzurumu watu maskini wasio na pa kusemea ikomeshwe mara moja maana na waliopewa dhamana kusimamia hawafany.Pia.kuna hadi Wizara ya Kazi na Ajira na ofisi za kazi kila mkoa lakini hakuna wanachofanya.