Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unatwanga maji kwenye kinu. Hivi unadhani huko nje nako kuna vichwa matikiti kama ilivyo ndani ya CCM? Huko nje hawadanganywi na propaganda za kijinga kama hizi za Shaka. Wanajua fika kuwa 2020 hakukuwa na uchaguzi, hivyo kuutumia uchaguzi wa 2020 kutengeneza legitimacy ya aina yoyote ni uwendawazimu.Tunaitaka Chadema kubadilika na kuanza kufanya siasa za hoja, zenye kutoa kipaumbele maendeleo ya wananchi na Taifa badala ya siasa hizi za kuhimiza ghasia, vurugu na kueneza uongo na chuki nchini.
Kadhalika Mnyika aache upotoshaji na kumlisha maneno Rais Samia ambayo hakuyasema au kuingilia mwenendo wa kesi ya Mbowe mahakamani kama anavyotumia nguvu kubwa kutaka kuaminisha umma.
Rais Samia katika maelezo yake alisema hakuna mahali nchini Demokrasia imeminywa na ndio maana vikao vya kikatiba vya vyama mbalimbali vya siasa nchini vinaendelea. alisisitiza siasa zenye mrengo wa vurugu na ghasia hazina nafasi na wala hazitavumiliwa kwani hiyo sio demokrasia.
Kuhusu sakata la kesi ya mwenyekiti wa chama hicho inayoendelea mahakama ya kisutu hakuna pahala katika maelezo yake Rais Samia wakati wote wa mahojiano aliingilia uhuru wa mahakama kama Mnyika alivyopotosha zaidi alitaka watu kuwa watulivu waipe nafasi mahakama kutekeleza wajibu wake.
CDM waache vioja vya kudai demokrasia imeminywa na hawaruhusiwi kufanya mikutano wala vikao wakati wameendesha operesheni haki, chadema kidigitali na vikao mbalimbali vya ndani bila bugudha yoyote. Lakini cha ajabu (leo) Mnyika ameendelea kuingilia uhuru wa mahakama jambo ambalo linaoonyesha jinsi alivyo na papara na jazba na kudhihirisha juu ya uchanga wake kisiasa.
Muhimu wakafahamu ikiwa maandalizi yao ya mikutano au vikao na operesheni zozote za kisiasa yatakuwa na viashiria au dhamira ya kupanga, kuratibu, kuasisi au kutekeleza vurugu na ghasia nchini vyombo vya dola havitakaa kimya sio kwao tu bali kwa yeyote yule.
Bahati mbaya ni kwamba hawana desturi ya kufanya mikutano, vikao au operesheni zao za kisiasa kwa amani na kwa kufuata taratibu na sheria hivyo wabadilike ili kuepuka kusigana na vyombo vya dola. Wao kukiuka taratibu na sheria ili kupata matukio ya kukabiliana na vyombo vya dola kwao umekuwa mradi wa kutafuta fedha kwa wafadhili wao nje ya nchi ndio maana hawataki kubadilika.
Rais Samia ameapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania, ikiwemo kuhakikisha ustawi wa amani na utulivu nchini. Hivyo haitatokea hata mara moja akakubali watu wachache kwa maslahi yao wakavuruga nchi.
Jambo jingine watanzania wanapaswa kujua Chadema sio chama kikuu cha upinzani wakati huu kwani kina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa hivyo hawana sifa hiyo.
Tunashangazwa na dhamira ya Chadema kutaka kuonana na Rais Samia wao kama wao ilihali wao sio chama pekee cha upinzani nchini. Rais Samia alitoa msimamo wa kuonana na vyama vyote vya upinzani kwa umoja ambapo atatoa tarehe na muda wakukutana nao.
Hili la Chadema kutaka kukutana na Rais Samia wakiwa pekee yao ni muendelezo wa siasa za ubinafsi na ubaguzi ambao umekuwa utamaduni wao jambo ambalo Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Samia haitazipa nafasi.
Nitoe rai kwa watanzania na wadau wote wa maendeleo ndani na Nje ya Nchi kuiunga mkono serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kwa pamoja tuifikishe Tanzania katika maendeleo endelevu.
End
Nina mashaka na elimu ya huyu mzamzibar anatoa maelezo meengi kujaza kurasa point za maana hakunaNa Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka chadema kubadilika na kuanza kufanya siasa za hoja, zenye kutoa kipaumbele maendeleo ya wananchi na Taifa badala ya siasa hizi za kuhimiza ghasia, vurugu na kueneza uongo na chuki nchini.
Pia chama hicho kimemtaka Mnyika kuacha upotoshaji na kumlisha maneno Rais ambayo hakuyasema au kuingilia mwenendo wa kesi ya Mbowe mahakamani .
Hayo yameelezwa na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka alipoulizwa kuhusu tuhuma alizozitoa katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika mapema leo dhidi Rais Samia.
Shaka amesema katika maelezo ya Rais Samia aliyoyatoa wakati wa mahojiano na kituo cha BBC Swahili cha nchini Uingereza yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam alisema hakuna mahali Demokrasia imeminywa nchini na ndio maana vikao vya kikatiba vya vyama mbalimbali vya siasa nchini vinaendelea. Aidha alisisitiza siasa zenye mrengo wa vurugu na ghasia hizo hazina nafasi na wala hazitavumiliwa kwani hiyo sio demokrasia. Hivyo Mnyika aache kumlisha maneno Rais Samia.
Abainisha kuwa Kuhusu sakata la kesi ya mwenyekiti wa chama hicho inayoendelea mahakama ya kisutu hakuna pahala katika maelezo yake Rais Samia wakati wote wa mahojiano aliingilia uhuru wa mahakama kama Mnyika alivyopotosha zaidi alitaka watu kuwa watulivu waipe nafasi mahakama kutekeleza wajibu wake.
"Chadema waache vioja vya kudai demokrasia imeminywa na hawaruhusiwi kufanya mikutano wala vikao wakati wameendesha operesheni haki, chadema kidigitali na vikao mbalimbali vya ndani bila bugudha yoyote. Lakini cha ajabu tena (leo) Mnyika ameendelea kuuingilia uhuru wa mahakama jambo ambalo linaoonyesha jinsi alivyo na papara na jazba Mnyika zinazvyomzidisha hofu kadri anavyolalamika." Alisema Shaka
Amesema ni muhimu wakafahamu ikiwa maandalizi yao ya mikutano au vikao na operesheni zozote za kisiasa yatakuwa na viashiria au dhamira ya kupanga, kuratibu, kuasisi au kutekeleza vurugu na ghasia nchini vyombo vya dola havitakaa kimya sio kwao tu bali kwa yeyote yule.
"Bahati mbaya ni kwamba hawana desturi ya kufanya mikutano, vikao au operesheni zao za kisiasa kwa amani na kwa kufuata taratibu na sheria hivyo wabadilike ili kuepuka kusigana na vyombo vya dola. Wao kukiuka taratibu na sheria ili kupata matukio ya kukabiliana na vyombo vya dola kwao umekuwa mradi wa kutafuta fedha kwa wafadhili wao nje ya nchi ndio maana hawataki kubadilika." Alieleza Shaka
Hata hivyo Shaka amefahamisha kusema Rais Samia ameapa kuilinda na kuitetea Katiba ikiwemo kuhakikisha ustawi wa amani na utulivu nchini. Hivyo haitatokea hata mara moja akakubali watu wachache kwa maslahi yao wakavuruga nchi.
"Jambo jingine watanzania wanapaswa kujua Chadema sio chama kikuu cha upinzani wakati huu kwani kina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa hivyo hawana sifa hiyo" Alisema shaka
Ameshangazwa na dhamira ya Chadema kutaka kuonana na Rais wao kama wao ili hali wao sio chama pekee cha upinzani nchini. Rais Samia alitoa msimamo wa kuonana na vyama vyote vya upinzani kwa umoja ambapo atatoa tarehe na muda wakukutana nao.
"Hili la Chadema kutaka kukutana na Rais Samia wakiwa pekee yao ni muendelezo wa siasa za ubinafsi na ubaguzi ambao umekuwa utamaduni wao jambo ambalo serikali haitazipa nafasi." Shaka
Shaka ametoa rai kwa watanzania na wadau wote wa maendeleo ndani na Nje ya Nchi kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kwa pamoja tuifikishe Tanzania katika maendeleo endelevu.
View attachment 1887678
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.Yule aliyesema Mbowe alikimbilia Kenya kukwepa mkono wa Sheria dhidi ya Mashtaka ya Ugaidi alipohojiwa na BBC Swahili nae apewe onyo kwa kuingilia uhuru wa Mahakama
Pamoja na madhaifu na shida zote za Polepole nafasi yake ya Katibu wa itikadi na uenezi kulinganisha na aliyeshika nafasi hiyo sasa hakika ni mbingu na ardhi, Polepole hashikiki, kwanza alikuwa mtu wa tafiti hata kama ni propaganda lkn alijaribu kui twist ilingane na mazingira halisi, Shaka alihitaji sana muongozo wa Polepole.Shaka ni katibu mwenezi ama msemaji na mtetezi wa Samia??
Kwakuwa ni ya kisiasa.View attachment 1887933
Nimeona hii na jana kulikua na mjadala mkali juu ya mamlaka ya Raisi juu ya maamuzi ya DPP. Kwanini Mnyika ambaye ni katibu wa CDM aombe Raisi Samia aingilie kati suala hili? Kwa mujibu wa ibara ya 59 (4) B ya katiba ya JMT, Raisi hana mamlaka juu ya maamuzi au utendaji wa DPP. Na kwamba Raisi akiingilia au kumuamrisha DPP cha kufanya atakua anakiuka #katiba aliyoapa kuilinda.View attachment 1887936
Lakini baadhi ya wafuasi wa wa CDM bado wanalazimisha raisi akiuke kwakua yeye ndie amiri jeshi mkuu na ndie boss wa DPP, hili limekaaje jamani? Wengine wameenda mbali mpaka kusema kwakua Magufuli alifanya hivyo kwa wahujumu uchumi basi na Samia nae afanye hivyo kwa Mbowe. Peoplesssssssss ?
View attachment 1887935
Yote kwa yote, nimefurahi kuona tumesomesha wanasheria ambao wapo tayari kua tofauti na upepo na mahaba ya kisiasa. Pascal Nkololo 👊👊👊. Hili la ibara ya 59 lingetupita wengi usingekua na ujasiri wa kupaza sauti ya kitaalamu. Endelea hivyo hivyo kaka, sisi tunakuona.View attachment 1887951
CHADEMA tusiwe wanafiki, kama sisi hatutailinda na kuifuata katiba iliyopo, tusiwaseme CCM.
Peopleeeeeeeeeeeeezzzzzzz .....
Biashara ya Free Bargain na uhujumu uchumi kilitumika kifungu gani?Kwani zile kesi za mafisadi na wahujumu uchumi alizifutaje!? Kumbukumbu mnazo kweli, au!?
huu ni ushahidi mwingine kwamba rais ana uwezo mdogo sana wa kujua mamboYule aliyesema Mbowe alikimbilia Kenya kukwepa mkono wa Sheria dhidi ya Mashtaka ya Ugaidi alipohojiwa na BBC Swahili nae apewe onyo kwa kuingilia uhuru wa Mahakama
Hatari snHao ni ving'ang'azi inabidi kukubaliana na hali halisi tu.