Shaka: Ni marufuku kwa hospitali za Serikali kumtoza Mama mjamzito kiasi chochote cha fedha wakati, kabla na baada ya kujifungua

Rais Samia alisema atapunguza vifo vya mama na mtoto na sasa amefanikisha hii ni hatua kubwa sana katika sekta ya afya
 
Ameeen
 
Vipi lile begi la mama mjamzito analotembea nalo kwa miezi kadhaa kabla ya lujifingua lenye gloves ma khanga nalo wamesamehewa? Sisiyemu bhana.
Begi hilo ni mhimu kuwa nalo kwa sababu unaweza kujikuta umejifungulia nyumbani au njiani na huna vifaa vya kukusaidia
 
Jamani kutoa agiza sio tatizo, je serikali inaweza kupeleka dawa na vifaa tiba vyote kutosheleza? Badala ya kutoa kauli kama hizi kila mwaka na mambo yale yale kujirudia ni heri serikali na wanasiasa kuhamasisha kila mwananchi kuwa na bima za CHF la sivyo watu wataendelea kudanganywa kila mara
 
CCM chama kinachojari raia wake, Viva CCM
Lkn wanashindwa kusimama wanayo yasema. Tena kwa sasa hivi watoa huduma wa umma wengi wanadai malipo ili watoe huduma.
Ni juzi tu mwenye no. ya simu hapo chini kapigwa laki kadhaa kwenye hospital za serekali, hatimaye alimpoteza mtoto na almanusra ampoteze mke.
No ni hizo. 0684532854.
 
Je usipowatoza wanawake wajawazito wanapojufungua unadhani vituo vya Afya vitapata wapi vitendea kazi kama nyuzi, gloves, pamba, bandages etc?

Kuliko kuropoka namna hii vijijini Shaka aende akapambane na Mwigulu Nchemba kuhakikisha kuwa anapeleka fedha kwa ajili ya jamii iliyo na msamaha kwenye matibabu; wazee miaka 60+, watoto chini ya miaka 5 na wazazi wanaojifungua. Sera ipo ni nzuri lakini kwenye reality fedha haipelekwi.
 
Huyu bwana naomba niseme tu wazi kuwa ni kiongozi mahiri na muhimu Sana kwa Taifa, mengine tumwachie Mungu wetu.
 
Kinachofanya mtu atoe pesa ni uchungu ukikuzidia na wanakuangalia kama vile hawakuoni ukiacha unaona kifo mbele yako au unashuhudia mtu anapoteza uhai kisa elfu 5.

Tutafute namna Bora ya kuwahudumia wenye shida
 
Kinachofanya mtu atoe pesa ni uchungu ukikuzidia na wanakuangalia kama vile hawakuoni ukiacha unaona kifo mbele yako au unashuhudia mtu anapoteza uhai kisa elfu 5.

Tutafute namna Bora ya kuwahudumia wenye shida
😍😍😍Umeambiwa usitoe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…