Shaka: Vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA viwe huru kususia uchaguzi

Shaka: Vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA viwe huru kususia uchaguzi

Shaka anadhani Eti watasusiwa!!!!

2025 hapatakuwa na huo uchaguzi,

Wananchi tutahakikisha Haufanyiki. Bila KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Ni Kweli watz walifungwa pingu, kitu pekee mlichosahau ni kuwa yupo aliyekwisha wafungua waende Kwa Amani.
 
Mbona hatukuona ukisisitiza Katiba wakati unamlamba Jiwe buttocks zake? Kwa Nini saizi?
Jiwe si mnasema alikuwa dikteta hivyo hakutaka katiba mpya, Sasa Samia si ni kiongozi mzuri muumini wa demokrasia. Sasa kuna ubaya gani kudai katiba mpya sasa hivi wakati kuna kiongozi mzuri?
 
Kinachofanya ionekane Katiba Mpya ni hitaji la kisiasa ni kutokana na mpiga debe mkuu kuwa chama cha siasa, hii ndio sababu inayotumiwa na CCM kuwafunga midomo wapinzani wao kuhusu hayo madai.

Lakini kama madai hayo yangetokea kwenye makundi tofauti ya kijamii, naamini CCM wangekuwa kwenye wakati mgumu zaidi ya ilivyo sasa, na kujikuta wanalazimika kuyafanyia kazi.

Hii mbinu ya kuunganisha makundi tofauti japo itaonekana itachukua muda mrefu, lakini naamini kama ikiwezekana, ndio itakuja na mafanikio makubwa zaidi ya ilivyo sasa.
Nini kilitokea sasa maana wananchi wenyewe ndio waliyotaka hiyo au kuona kuna uhitaji wa katiba mpya halafu tena wao ndio wanakaa nyuma na kuacha wanasiasa kuwa ndio mstari wa mbele kupigania katika mpya?
 
Habari za leo wadau.

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake Wa Uenezi komledi Shaka kimesema Vyama vya upinzani viwe huru kabisa Kususia uchaguzi hususani CHADEMA ambao ndio wamekuwa wakisema watasusia chaguzi zozote bila Tume huru na Katiba Mpya.

Shaka amesema wakisusa CCM wao wataendelea kula.

Wanachadema pokeeni dongo Hilo mtaamua kula au kushinda na njaa.[emoji116]

=====

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamidu Shaka amevitaka baadhi ya vyama vya upinzani kuwa huru kususia uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ni haki yao na hata vikifika maamuzi hayo chama hicho hakitayumba kwa kuwa kimejipanga kuchukua tena dola mwaka 2025.

Ameyasema hayo Unguja wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo amesema kuwa mapokezi makubwa aliyoyapata Rais Dkt. Mwinyi ni ishara ya wazi kuwa wananchi wameridhishwa na uongozi wake.

“Nimekuwa nikisikiasikia wameanza kusemasema kwamba wanafikiria sijui tutasusa, sasa sijui msuse msisuse shughuli ipo kitu hiki hapa. Niwaombe wana-CCM wenzangu msipoteze muda wa malumbano na majibizano, tuna kazi ya kujenga chama, tuna kazi ya kujenga nchi hii,” amesema.

Ameongeza kuwa kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama hicho ni ‘kutesti mitambo’ tu na kwamba muda ukifika wapinzani wataupata ujumbe, hivyo wakae kwa kutulia kwa kuwa hakuna mjadala katika hilo na wala hakuna kubembelezana.


CHANZO: Swahili Times
Huyu Shaka nadhani naye ni akili kibaba. Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kutoa kauli ya namna hiyo.

Watu wenye akili ndogo kama Shaka ndio watakaomwangusha Rais Samia.
 
Rais Magufuli alipora uchaguzi 2020 ili atawale maisha. Je, anatawala mpaka sasa.

Kila mwenye hekima huitafuta haki na kuilinda haki. Lakini mpumbavu hudhulumu haki ili afaidi visivyo halali kwa miaka mingi bila hata ya kutambua kuwa Duniani hakuna mwenye uhakika wa miaka mingi.

Wenye hekima ndani ya CCM mpuuzeni MPUNGUKIWA KICHWANI, Shaka.
 
Japo naunga mkono hoja, ya "ukisusa sie twala...," na siungi mkono hii tabia ya kususa susa.... Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto? na hapa Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! na Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA is almost dead, due to deadly mistakes! This is your only survival -- do or die. Msirudie kosa

Lakini kama wanasusa for genuine reasons za kutotendewa haki, kama tulivyo shauri hapa Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Najua by now wasoma trends wanajua the consequences za kutotenda haki kwenye uchaguzi, sisi washauri huru tuliisha shauri kabla Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! hivyo Shaka asijitape wakisusa kwa kutetendewa haki sisi twala, badala ya kula wakajikuta wao ndio wanaliwa vichwa!.

Karma haina mswalie Mtume, walishindwa kumlinda Blaza, karma ikafanya yake!, ili kumlinda Maza na karmic consequences, sisi tunao ijua karma, lazima tumsaidie Maza kwa kumweleza ukweli ili aepuke the consequences na yeye asije... hivyo kwa kuanzia tumemshauri Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
Karma haina mswalie Mtume, walishindwa kumlinda Blaza, karma ikafanya yake!, ili kumlinda Maza na karmic consequences, sisi tunao ijua karma, lazima tumsaidie Maza kwa kumweleza ukweli ili aepuke the consequences na yeye asije... hivyo kwa kuanzia tumemshauri Voices From Within:

☝☝☝umeongea kitu kizito sana kwa mara ya kwanza kuwa blaza alitafunwa na karma.
 
Ni kweli alichosema huyo jamaa, mbinu ya kususa haiwezi kuwa na nguvu sana kwasababu CCM itawaambia vyama rafiki vyao vya upinzani washiriki, nao watashiriki huku wakisema ulikuwa huru na haki, na wakija waangalizi wa kimataifa nao waseme hivyo, na shughuli ndio iishie hapo.

Bila kufanyika jitihada za ziada, naona haya madai ya Katiba Mpya, na Tume Huru ya uchaguzi yatakuwa endelevu yasiyojulikana lini utakuwa mwisho wake, hivyo kuendelea kuinufaisha CCM.

Muhimu Chadema wasionekane wanahodhi madai ya Katiba Mpya, kwani hii inawapa CCM sababu nyepesi za kujibu hoja hiyo ikiwemo wananchi hawali Katiba Mpya.

Naona kuna haja sasa kwa Chadema kuhakikisha wanapeleka somo la umuhimu wa Katiba Mpya kwa makundi mengine ya kijamii, ikiwemo, kilimo, uvuvi, wafanyabiashara, na kada nyingine.

Ili hawa wakishapewa somo na kulielewa, nao wageuke walimu, waanze kupaza sauti zao kwa pamoja, kwa kufanya hivyo; kwanza itasaidia kuondoa dhana kwamba madai ya Katiba Mpya ni ya Chadema, au ya kisiasa, lakini pia, itayafanya madai ya Katiba Mpya yachukuliwe kwa uzito zaidi, na kuleta impact kubwa zaidi ya ilivyo sasa, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kufikia malengo kwa wakati.
Cha muhimu ni kutoshiriki uchaguzi haramu, na kuhakikisha, iwe jwa shari au amani, haufanyiki.
 
Kamwe siwezi unga mkono ususaji.
Utasusa ACT watashiriki, hakuna nchi inaweza zuia uchaguzi usifanyike kisa Chadema imesusa.

Hawa CCM ni kupambana nao kwa njia watakazo wao.

Kati ya mwaka ambao Upinzani utapeleka Wabunge wengi bungeni ni 2025, maana najua tayari hapo kati itakuwepo fair ground.

Na ili Katiba ipatikane lazima Wabunge waipitishe, je Upinzani upo tayari ccm pekee wapitishe?
 
Lini walionesha Kutaka? Mbona tunawaona Chadema tuu huko front?
Labda kama hukuwepo Tanzania, au wakati huo ulikuwa mgonjwa?

Tume ya Jaji Warioba ilisema wananchi wanataka nini?

Walihojiwa vyama vya upinzani au wananchi wote wa makundi yote?

Jukwaa la JF inaonekana kwa sasa limejaa low brains ambao hawajui chochote zaidi ya Kuandika, Kuhesabu na Kusoma. Analysis kwao ni zero.

Yaani baada ya miaka zaidi ya mitano, mtu bado hajui kuwa wananchi kwa kupitia ushiriki mpana wa Tume ya Jaji Warioba, wote walitamka kuwa WANATAKA KATIBA MPYA. Halafu mtu huyo naye anaona ana kiwango cha kuchangia hoja hapa JF ambapo ilikusudiwa kuwa jukwaa la watu wenye uelewa.
 
Labda kama hukuwepo Tanzania, au wakati huo ulikuwa mgonjwa?

Tume ya Jaji Warioba ilisema wananchi wanataka nini?

Walihojiwa vyama vya upinzani au wananchi wote wa makundi yote?

Jukwaa la JF inaonekana kwa sasa limejaa low brains ambao hawajui chochote zaidi ya Kuandika, Kuhesabu na Kusoma. Analysis kwao ni zero.

Yaani baada ya miaka zaidi ya mitano, mtu bado hajui kuwa wananchi kwa kupitia ushiriki mpana wa Tume ya Jaji Warioba, wote walitamka kuwa WANATAKA KATIBA MPYA. Halafu mtu huyo naye anaona ana kiwango cha kuchangia hoja hapa JF ambapo ilikusudiwa kuwa jukwaa la watu wenye uelewa.
Kwanini sasa wanachi wako nyuma kwenye kudai katiba mpya na kuwaachia chadema hadi inaonekana katiba mpya ni kama hitaji la wanasiasa tu wakati wao ndio waliona uhitaji wa katiba mpya?
 
☝☝☝umeongea kitu kizito sana kwa mara ya kwanza kuwa...
Mkuu Glenn, sio kwa mara ya kwanza, ni vile tuu wengi humu hawana uwezo to read in between the lines!, kumhusu Blaza niliisha sema kila kitu tangu ile 2014! Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" nilisema
Wanabodi,

Hili la kuamua ni ...., limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia utendaji kazi wa .... kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, japo kiukweli ni mchapa kazi, yaani ni jambo la ukweli, lakini mtu huyu ameonyesha wazi sio mzuri sana in terms of stability in decision making!, amefanya baadhi ya maamuzi mengi tuu kwa jazba, pupa, papara na kukurupuka kwa mtindo wa nimeamua mimi na liwalo liwe!, mwisho wa siku baadhi ya maamuzi yake ambayo mengine ni very rational yanakuja kutu cost sisi kama taifa, mifano ipo, ikiwemo kuvunjwa ile Petro Station Mwanza, Uuzaji wa nyumba za serikali, Samaki wa ... just to mention but few, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi hii, kama huu ndio mfumo wake wa kufikia maamizi, then you can just imagine, akiwa rais, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia kwa hulka yake, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!. Tuombe Mungu asaidie, hili likitimia, huyu mtu abadilike, na kuwa a benevolent one, labda karma ije kuingilia kati, vinginevyo...!.

Paskali
P
 
Rais Magufuli alipora uchaguzi 2020 ili atawale maisha. Je, anatawala mpaka sasa.

Kila mwenye hekima huitafuta haki na kuilinda haki. Lakini mpumbavu hudhulumu haki ili afaidi visivyo halali kwa miaka mingi bila hata ya kutambua kuwa Duniani hakuna mwenye uhakika wa miaka mingi.

Wenye hekima ndani ya CCM mpuuzeni MPUNGUKIWA KICHWANI, Shaka.
Ujumbe mzuri na logic notion.Shaka akumbuke kipindi cha mwendazake akina Makonda,Bashiru,Polepole,Musiba,Sabaya,Mnyeti,Ally Happy nguvu waliyokuwa nayo je inaendelea?Na je walipenda wawe pembeni kwenye madaraka yao na nguvu zao?Na je kulifanyika uchaguzi wowote ambao ulisababisha hao watajwa kuondolewa kwenye nafasi zao?
Anasema CHADEMA wakisusa sisi yetu ni kuendelea kuchukua dola,je ana uhalali na uhakika kuwa ataendelea kutawala miaka kumi ijayo?Mwenye akili atajifunza kile kilichojitokeza kwa Magufuri ambaye lengo lake ilikuwa kubadilisha Katiba na kuwa Rais wa Milele kama Gaddafi ingawa siyo mara zote kujitokeza kama ya Magufuri lakini mapinduzi yanaweza kuja kwa njia nyingine.Hili ni Taifa lenye watu wengi na mitazamo tofauti.Shaka akumbuke kuwa Cheo ni dhamana na cheo siyo passport ya kufanya unalolitaka wewe.
 
Mkuu Glenn, sio kwa mara ya kwanza, ni vile tuu wengi humu hawana uwezo to read in between the lines!, kumhusu Blaza niliisha sema kila kitu yangu ile 2014! Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
P
Braza, kuna kipindi unayumba sana hasa inapitokea fursa mbele yako unayumba sana.
Mifano hai;
1. Ulipoitamani Kawe uliyumba sana ulifanana nao 100%

2. Ulipoutamani wa EA pia uliyumba braza.

Nikushauri ubaki relini unafaa sana ukiwa relini.
Nikushauri wewe hufai na hufiti kuzongania zile fursa zao hutaweza sababu sio mla rushwa wa kiwango chao.
Na kana unautaka ubunge nafasi yako iko upinzani lkn kwa ccm kamwe huwezi kuteuliwa, sio kwasababu huna sifa la! Unazo sifa na kuzidi ulichopungukiwa ni kuwa mtoa rushwa wa kiwango chao.

Labda upate uteuzi...na huu unakutaka uwe chawa wao kwanza.

Una kiti chako upinzani pekee
 
Cha muhimu ni kutoshiriki uchaguzi haramu, na kuhakikisha, iwe jwa shari au amani, haufanyiki.
Ili kufanikisha haya pia, naamini panahitajika mipango, ila sijui kama imeshaanza kupangwa...

Kuhakikisha uchaguzi haufanyiki, na kuiambia jumuia ya kimataifa sababu zako za kufanya hivyo ikuelewe, hasa ikizingatiwa wengine watakuwa tayari kushiriki, naona halitakuwa jambo dogo.
 
Back
Top Bottom