Shaka: Vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA viwe huru kususia uchaguzi

Shaka: Vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA viwe huru kususia uchaguzi

Nini kilitokea sasa maana wananchi wenyewe ndio waliyotaka hiyo au kuona kuna uhitaji wa katiba mpya halafu tena wao ndio wanakaa nyuma na kuacha wanasiasa kuwa ndio mstari wa mbele kupigania katika mpya?
Kimsingi Chadema ilikuwa inawasemea wananchi, na ilikuwa inafanya hivyo kwa kutumia majukwaa ya kisiasa, tofauti na wananchi ambao hawana majukwaa yanayoeleweka kama ilivyo kwa wanasiasa.

Pia, baada ya CCM kuteka mchakato wa Katiba Mpya kwenye lile bunge la Katiba, kwa kuondoa rasimu ya Warioba na kuleta Pendekezwa iliyokuwa kwa manufaa kwa CCM, hapa ndipo palipowafanya Chadema wakazidi kupaza sauti zao, kwa kutaka matakwa ya wananchi yafuatwe..
 
Kwanini sasa wanachi wako nyuma kwenye kudai katiba mpya na kuwaachia chadema hadi inaonekana katiba mpya ni kama hitaji la wanasiasa tu wakati wao ndio waliona uhitaji wa katiba mpya?
Ni platform ipi ambayo wananchi wamepewa kuweza kushinikiza yale wanayoyataka.

Wewe unafahamu kabisa kuwa utawala wetu una mwelekeo wa kidikteta. Mbowe ambaye ni maarufu, kiongozi wa chama, aliyekuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, tena mwenye uwezo wa kuwa na mawakili, kwa kudai tu katiba aliishia kubambikiwa kesi ya ugaidi na kukaa jela takribani nusu mwaka. Hivi huyu mwananchi wa kawaida tu akainuka kudai katiba, unadhani watamfanya nini!!
 
As long as katiba hii inasimama CCM watafanya watakavyo hakuna wa kuzuia.

CCM ni mfumo wa kidola, kupambana na CCM ni kupambana na dola ya nchi.

Hadi hapo katiba yetu itakapotenganisha Dola na vyama vya siasa ndipo sasa uhuru wa kujieleza, shughuli za vyama vya kisiasa, chaguzi huru na utawala wa sheria ndipo zitakapoanza kushuhudiwa kwa mara ya kwanza.

Kwa hiyo huyo katibu yupo sahihi, wapinzani wakisusa ama wakishiriki haina tofauti yeyote, CCM lazima ishinde kwa takwimu wanazotaka wao
 
Ni platform ipi ambayo wananchi wamepewa kuweza kushinikiza yale wanayoyataka.

Wewe unafahamu kabisa kuwa utawala wetu una mwelekeo wa kidikteta. Mbowe ambaye ni maarufu, kiongozi wa chama, aliyekuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, tena mwenye uwezo wa kuwa na mawakili, kwa kudai tu katiba aliishia kubambikiwa kesi ya ugaidi na kukaa jela takribani nusu mwaka. Hivi huyu mwananchi wa kawaida tu akainuka kudai katiba, unadhani watamfanya nini!!
Ila wengine wanashauri wananchi kupewa elimu kuhusu hili la katiba mpya maana inaonekana wananchi wanalichukulia hili suala kama ni la wanasiasa tu.
 
Ila wengine wanashauri wananchi kupewa elimu kuhusu hili la katiba mpya maana inaonekana wananchi wanalichukulia hili suala kama ni la wanasiasa tu.
Hii iliyopo wananchi walipewa elimu kabla ya kupitishwa na kuwa Katiba??
 
Ila wengine wanashauri wananchi kupewa elimu kuhusu hili la katiba mpya maana inaonekana wananchi wanalichukulia hili suala kama ni la wanasiasa tu.
Sio wananchi wanalichukulia hili suala kama ni la wanasiasa, CCM ndio wanaofanya hivyo kwa kuyaita madai ya Katiba Mpya ni ya kisiasa ili watimize malengo yao.
 
Sio wananchi wanalichukulia hili suala kama ni la wanasiasa, CCM ndio wanaofanya hivyo kwa kuyaita madai ya Katiba Mpya ni ya kisiasa ili watimize malengo yao.
Ndio wanasema hivyo kwa sababu wananchi wenyewe hawako mbele kwenye kudai hiyo katiba mpya, lakini pia ni kweli wapo baadhi ya wananchi wenye mtazamo huo.
 
Ndio wanasema hivyo kwa sababu wananchi wenyewe hawako mbele kwenye kudai hiyo katiba mpya, lakini pia ni kweli wapo baadhi ya wananchi wenye mtazamo huo.
Nipe mfano wa wananchi wengine wanaosema madai ya Katiba Mpya ni ya kisiasa tofauti na viongozi wa CCM.
 
Tunazungumzia hiyo mpya ambayo wananchi wenyewe ndio waliyoitaka kwa kuona hii iliyopo sasa kuna mapungufu.
Waelimishwe nini wakati wenyewe ndiyo waliitaka? Kwa nini CCM inaonesha kama vile wananchi hawana akili ya kujua nini wanataka!!??
 
Habari za leo wadau.

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake Wa Uenezi komledi Shaka kimesema Vyama vya upinzani viwe huru kabisa Kususia uchaguzi hususani CHADEMA ambao ndio wamekuwa wakisema watasusia chaguzi zozote bila Tume huru na Katiba Mpya.

Shaka amesema wakisusa CCM wao wataendelea kula.

Wanachadema pokeeni dongo Hilo mtaamua kula au kushinda na njaa.[emoji116]

=====

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamidu Shaka amevitaka baadhi ya vyama vya upinzani kuwa huru kususia uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ni haki yao na hata vikifika maamuzi hayo chama hicho hakitayumba kwa kuwa kimejipanga kuchukua tena dola mwaka 2025.

Ameyasema hayo Unguja wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo amesema kuwa mapokezi makubwa aliyoyapata Rais Dkt. Mwinyi ni ishara ya wazi kuwa wananchi wameridhishwa na uongozi wake.

ā€œNimekuwa nikisikiasikia wameanza kusemasema kwamba wanafikiria sijui tutasusa, sasa sijui msuse msisuse shughuli ipo kitu hiki hapa. Niwaombe wana-CCM wenzangu msipoteze muda wa malumbano na majibizano, tuna kazi ya kujenga chama, tuna kazi ya kujenga nchi hii,ā€ amesema.

Ameongeza kuwa kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama hicho ni ā€˜kutesti mitambo’ tu na kwamba muda ukifika wapinzani wataupata ujumbe, hivyo wakae kwa kutulia kwa kuwa hakuna mjadala katika hilo na wala hakuna kubembelezana.


CHANZO: Swahili Times
Zidumu fikira za shoga la mapinduzi ...zidumu
 
Waelimishwe nini wakati wenyewe ndiyo waliitaka? Kwa nini CCM inaonesha kama vile wananchi hawana akili ya kujua nini wanataka!!??
Wananchi hawaonekani kuwa mstari wa mbele kwenye kudai hiyo katiba mpya, wanaovutana kuhusu katiba ni wanasiasa tu na ni kweli wapo baadhi ya wananchi wenye kuona katiba mpya ni suala la chadema.
 
Back
Top Bottom