Wasaka urais kuelekea mwaka 2025 kuondolewa rasmi ndani ya Baraza la Mawaziri siyo!? Uamuzi huu unapaswa kuangaliwa kwa uangalifu mkubwa sana.
Uwepo wa wateule wa JPM ndani ya baraza bado una umuhimu mkubwa sana kwa utengamano wa CCM ya sasa. Ili kuthibiti pilikaplika za hapa na pale, ni vyema wakazidi kuwepo.
Natambua kauli ya "niguse ninuke" iliyotolewa kule jimbo la kusini wakati wa ziara ya PM inafungua "codes" fulani muhimu ili kuhalalisha mabadiliko tarajiwa. Hamasa inafanyika ili kuondoa makapi ya 'champion" wa Chato.
Ila tahadhari ichukuliwe kama washika hatamu wameazimia kumundoa mtu huyu na huyu katika wizara hizo nyeti kwa muda huu. Ni vyema wavute sunira, ili kwa "timing" kubwa akapanguliwa mmoja baada ya mwingine kuliko kuwaondoa wote kwa pamoja. Kwa pupa hii, hakika chama twawala kinakwenda kupasuka rasmi katika makundi mawili na kuelekea katika kifo chake.