TANZIA Shakoor Jongo wa Global Publishers afiwa na kaka yake

TANZIA Shakoor Jongo wa Global Publishers afiwa na kaka yake

nakutumia pm huzipati??
mie nachambwa huku pm eti nipo group lako.
haaaa mie hata siyajuia pm zangu za mitongozo tu asa hilo grupu kivipi.
na mie nawatukana tu

Jamani mi pm imerogwa sijui mi sipati pm,group lipi tena,mi mbona sijaongea na wewe chochote, pole kwa hilo
 
Mdau wenu Shakoor Amefariki Kwa ajali kinondoni Maasai pale Leo Alfajiri. Maiti Kwa sasa ipo Mwanyamala hospitali
 
Kifo bnaa...mwanzisha uzi nae ni marehemu
 
87e8aaa1-f6e5-4c2f-a6e8-bac8dee5345c.jpg

RIP Zungu
 
Warumi jamani a.ka. binamu[emoji25]
 
Mdau wenu Shakoor Amefariki Kwa ajali kinondoni Maasai pale Leo Alfajiri. Maiti Kwa sasa ipo Mwanyamala hospitali
Apumzike kwa amani, kama kuna kuonana huko amsalimie sana binamu yetu warumi
 
Aliyetoa taarifa za msiba binamu warumi nae hatunae tena, shakoor jongo nae leo kaondoka na kaiacha dunia
 
Mwandishi wa habari na mdau mkubwa wa burudani, Shakoor Jongo almaarufu Zungu Fedha, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Septemba 4, 2022 kwa ajali ya kugongwa na gari. Jongo amefikwa na umauti Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Asha Baraka, Mkurugenzi wa Twanga Pepeta ambaye ni miongoni mwa watu wake wa karibu. "Kulikuwa na shoo ya Twanga Pepeta huko Sinza, K-Garden karibu na kwa marehemu Banza Stone, mimi sikuingia ndani sababu nilikuwa natoka kwenye harusi ya Chaz Baba, nikiwa pale nikamuona Jongo akipita, nikamuita, 'wewe Zungu njoo' hakunisikia sababu ya muziki, alikuwa akipanda jukwaani kwa sababu muziki ulikuwa unapigwa. "Baadaye mimi nikaondoka kwenda nyumbani. Nafika tu nyumbani naingia ndani ananipigia simu Kanoute mpiga solo wa Twanga, kwamba wametoka pale Twanga na Zungu, wamekuja sasa yeye Kanoute alikuwa ananunua chipsi, anaangalia anaona watu wapo katikati ya barabara. "Kwenda kuchungulia anamuona Zungu lakini kagongwa na keshakufa na gari imekimbia. Ndipo akaomba wakampakia kwenye gari na kumpeleka hospitali ya Mwanayamala. Zungu ambaye amewahi kuwa mwandishi wa Global Publishers kupitia magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi na Amani, alikuwa mdau mkubwa wa masuala ya Burudani. Global Publishers inawapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa muziki kwa msiba huo. Taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitakuja baadaye. Chanzo @globaltvonline
 
Back
Top Bottom