Shambulizi la Israel katika soko la Gaza laua Wapalestina 18, madaktari wanasema

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Takriban Wapalestina 18 wameuawa baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel kulenga kitengo cha polisi cha Hamas kilichojaribu kudhibiti soko katika mji wa Deir al-Balah katikati mwa Gaza, madaktari wameiambia BBC.

Walioshuhudia tukio hilo walisema ndege zisizo na rubani za Israel ziliwafyatulia risasi vikosi vya Hamas, waliokuwa wamevalia kiraia na kuvaa barakoa, ambao walikuwa wakikabiliana na wachuuzi wanaowatuhumu kwa upandishaji wa bei na kuuza bidhaa zilizoporwa kutoka kwa malori ya misaada.

Wizara ya Mambo ya Ndani inayoongozwa na Hamas ililaani shambulizi hilo, ikiishutumu Israel kwa kufanya "uhalifu mwingine dhidi ya kitengo cha polisi kilichopewa jukumu la kudumisha utulivu wa umma".

BBC imewasiliana na jeshi la Israel kwa maoni yake.
 
HIZO NDO MAMBO ANAZOWEZA,WATOTO,WAZEE NA WANAWAKE UTAJIPIGIA UNAVYOTAKA
 
Hezborh na hamas wataendelea kuwepo
Baba Yako mzazi/mlezi unaona anapewa vitasa hadharani na unashindwa kumsaidia wewe kuona wapi?

Siku 12 hatujaona Hizbullah akirusha hata jiwe tu ndani ya Israel, siku hizi IDF wanawatembezea kichapo kimya kimya cha ajabu wao wenyewe Hizbullah ndio wanaomba msamaha kwisha habari Yao , Hao Hamas kinachowafanya wa survive mpaka Leo ni hao mateka tu na kujichanganya na raia la sivyo habari ingekuwa kama ya wenzao
 
Back
Top Bottom