Takriban Wapalestina 18 wameuawa baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel kulenga kitengo cha polisi cha Hamas kilichojaribu kudhibiti soko katika mji wa Deir al-Balah katikati mwa Gaza, madaktari wameiambia BBC.
Walioshuhudia tukio hilo walisema ndege zisizo na rubani za Israel ziliwafyatulia risasi vikosi vya Hamas, waliokuwa wamevalia kiraia na kuvaa barakoa, ambao walikuwa wakikabiliana na wachuuzi wanaowatuhumu kwa upandishaji wa bei na kuuza bidhaa zilizoporwa kutoka kwa malori ya misaada.
Wizara ya Mambo ya Ndani inayoongozwa na Hamas ililaani shambulizi hilo, ikiishutumu Israel kwa kufanya "uhalifu mwingine dhidi ya kitengo cha polisi kilichopewa jukumu la kudumisha utulivu wa umma".
BBC imewasiliana na jeshi la Israel kwa maoni yake.