Simba na Yanga zilitakiwa ziwe blueprint ya advanced soccer management, lakini mambo wanayoyafanya ni ya kizamani sana.
Labda wanaofaidika na huu utaratibu mbovu wanasumbua kurasimisha.
Mo hajamaliza part yake, isipokuwa amebadilika kuwa mdhamini wa timu, akitoa hela kwa ajili ya uendeshaji wa timu huku akipata nafasi ya kutangaza bidhaa zake.
In short-run, haina shida maana timu inapata matokeo, kitu ambacho wote kama washabiki tunahitaji.
In long-run, Simba tuko pabaya kwa sababu muda wowote akiamua anaweza kusitisha kufanya hivyo kwa sababu yoyote ile, hapo tutahangaika sana. Wakati kama angekuwa aliweka mzigo, sisi tungekuwa kwenye stronghold tofauti na sasa.
Mo katushika, anaweza kuamua chochote ndani ya Simba na hakuna kubisha.