You have a valid point ingawa pia umeichanganya na baadhi ya vitu ambavyo sio sahihi.Nakubali kwamba unachoongelea ni kitu cha msingi sana bila kujali huo mchanganyiko uliouweka.
Kama bao EFM wametamka hiyo dhihaka kweli wamefanya makosa yasiyopaswa kabisa kufanywa na chombo cha habari.Inajulikana na watu wote wanaofuatilia michezo kwenye mitandao kuwa hayo maneno ya kumhusisha mkude na barbara yapo tangu siku Simba walipotoa ile release yao.Kwakuwa jamii yetu ina wajinga wengi Basi hilo limebebwa na kusambazwa hadi imekuwa ndo 'talk of the town'!Kwahiyo hiyo redio kulibeba na kuliweka kwenye chombo chao ambacho sio mtandao na kuliongea hata kama sio mojakwamoja ni kumkosea heshima Sana Barbara.Ni Kukosa na kukiuka maadili ya chombo cha habari.Ni kumdidimiza mwanamke.Ni kumdharau na kuendeleza kasumba isiyofaa ya kumchukulia mwanamke kama kitu kisicho na maana yoyote.Kwamba kwa sababu CEO wa Simba ni mwanamke mrembo basi dhihaka dhidi yake juu ya urembo na jinsi yake vionekane ni halali?Anazo credentials zake ambazo watu hawafanyi dhihaka kwazo,bali Wanafanya dhihaka na jinsi na urembo wake.Na watu wanahalalisha!Ni sawa na kipindi fulani Haji Mara aliwahi kufanyiwa dhihaka kutokana na ualbino wake na jamii kwa ujumla wake ililaani Sana hilo jambo.Sasa hakuna tofauti hapa kwa Barbara.Kutumia namna yoyote ya kimaumbile ambayo mhusika hakuwa na uamuzi nayo kumfanyia dhihaka au namna yoyote ya kumkejeli au kumbagua, sio sawa.Haliwezi kuwa jambo linalopaswa kuungwa mkono na jamii inayojali utu na usawa.
Pia kulichanganya hili na porojo za usimba na uyanga,gsm na dewji sijui senzo na kitu gani bado wewe ulielileta inaonekana hujaguswa kwa sababu ya utu,bali kwa mapenzi yako na simba.Kwamba kama ingetokea wewe ni yanga ungekuwa upande wa hao wapuuzi EFM?Hii sio sahihi hata kidogo.Pia ikumbukwe kuna tabia zisizofaa tunazo binadamu bila kujali affiliations zetu kwenye timu tunazozishabikia.Sio lazima mashabiki wote wa yanga wamdhihaki Barbara kwenye hili na sio lazima mashabiki wote wa Simba waumie kwenye hili.Kwahiyo kuliongea hilo kwa namna yoyote inayoweka mpaka wa kishabiki sio sawa .Inatosha tu kusema wote wanaoendeleza suala hilo la mkude kumdhihaki barbara ni wajinga,wapumbavu na wapuuzi kabisa.Kama ni wa Lipuli haiondoi ujinga wao.Kama ni wa Simba haiondoi upumbavu wao na kama ni wa yanga haiondoi upuuzi wao.