Shamimu Mwasha na Abdul Nsembo wahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha Dawa za Kulevya

Mie namuomba Mungu kila siku hata mahabusu aniepushe nayo. Mtoto kalegea, hapo leo chakula hakipandi, usingizi haupandi.. yaani maisha yameisha rotate 360⁰
Uadilifu ni jambo muhimu...alimuacha mme wa kwanza kwa tamaa tu na kuolewa tena,what goes around comes around.
Mke wangu wa ndoa aliondoka kwa mbwembwe leo anaugua kila muda anaita jina langu...huyo dada analipa sasa.
Hakuna maisha baada ya kifo, malipo ni hapa hapa kabda hujalala
 
Kwa hiyo hata huko mbele drug dealer mwenye uzoefu kama Carlos akikamatwa na shehena ya madawa atakuwa anadunda tu kitaa anapewa kazi mbadala eeeh???
 
Makosa ya dawa za kulevya hayako kwenye plea bargaining. Ila huyu mama angepunguziwa adhabu busara ilitakiwa itumike hapa angalau akalee watoto wale jamani. Waswahili walisema tamaa mbele mauti nyuma
Adhabu haipunguzwi kwa kuwa eti ana Watoto. Ingekuwa hivyo kile mwenye Watoto atakuwa anafanya makosa au atakuwa anauza madawa na akikamatwa anasingizia Watoto
Sheria haitoi huruma, inatoa haki
Kama alijua ana watoto kwa nini akauze madawa?
 
Hii wademu wajifunze. Tamaa mbaya sana, wengi huumia kwa ajiri ya tamaa ya pesa na vitu. Wengi hutuacha kwa mbwembwe ila wanapokimbiliaga huishia kulia kilio cha ng'ombe . Ndio ivyo kaishapotea huyo demu kutoka sio leo wala keshoo..
 
Umeeendeleza story kule mzee baba?
 
Mkuu hakika umenena, huwezi mhurumia Shamimu as if ulikuwa body guard wake. Kama alihusika abebe msalaba wake. Asitafute huruma.
 
Vyombo vya usalama bila ya shika wanawajua wahusika wa biashara hii lakini kwa sababu ya rushwa na kulindana ndiyo tunaona hii biashara haikomi.
Ile list ya Bashite sijui iliishia wapi. Ni kweli Serikali inawajua mapapa wa hii kitu na wengi wao huwa wanapita VIP lounge huko ambako hakuna anayekagua mabegi yao
 
dah hapoo majutoo ndo yataanza. mwanamke nae atajuta kwanini alichukua bwana wa mtu kwanini alimuacha mume wake wakwanza. usiku wa leo utakuwa mrefu sana kwake.


marafiki watakutembelea tembelea baada ya miaka kadhaa wanakusahau tena kama watakuwa wanahamishwa hamishwa magereza ndo biashara imeisha.

polee kwa familia polee kwa watoto. hatima ya maisha yao imeishia hapoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…