Watu wanasema Shamimu aachwe katika hali ya kawaida ni sawa kusema hivyo, kisheria ni ngumu labda hicho kitumike kumpunguzia walau miaka.
Lakini kabla hajataka kuonewa huruma kwa sababu ana watoto alipaswa kujionea na kuwaonea huruma wanae, angeweza kujiondoa katika maisha ya Abdul, wala asingepoteza pesa sababu angeendelea kutambuliwa kama baby mama na kikombe hiki kwa kiasi fulani angekiepuka na angeendelea kulea wanae.
Wanawake tunapaswa kuwa ahead of time, Leo hii marehemu Ivan angekamatwa kwa makosa ya zamani ya madawa na utapeli, sidhani kama Zari pia angehukumiwa sababu walishaachana kwa maandishi, ni rahisi kujitetea kuwa sikuwa nafahamu aliyokuwa akiyafanya mume wangu.
Anyways.... Shamimu ni mwana kulitafuta, Yeye sa hivi anaenda jela kwa kushirikiana na Mume wakati yule mchepuko mwenye maduka yake "fulani fulani" likiwemo na lile la BigBone sinza Akiendelea kupeta mtaani anaendelea na biashara zake halali na kulea mwanae.
Wanawake tuwe na akili, kama huwezi kumshauri mume aache basi jiachishe, kwa nia njema tu ili uendelee kulea watoto.