Shamsa Ford: Napendelea kuvaa chupi za mtumba

Shamsa Ford: Napendelea kuvaa chupi za mtumba

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
SHAMSA.png


Licha ya baadhi ya mastaa kudai wanavaa nguo spesheli tu, tena zile zilizofungwa kwenye nailoni, staa wa filamu Bongo Shamsa Ford amefunguka kuwa, yeye huwa anapendelea kuvaa nguo za mitumba zikiwemo nguo za ndani ‘makufuli’.

Akizungumzia nguo anazopenda kuvaa, mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Terry alisema, kuna mtu huwa anampelekea nguo ‘classic’ za mitumba na anachagua zile zinazomfaa, ananunua na kuzivaa.

“Niseme tu ukweli kwamba, napenda sana nguo za mtumba, hata makufuli. Huwa nanunua, nazifua na kuziweka ‘sopusopu’ kisha navaa, sioni shida katika hilo,” alisema Shamsa.

Serikali iliwahi kupiga marufuku uuzwaji wa nguo za mitumba za ndani kama vile makufuli, brazia na soksi lakini bado nguo hizo zimekuwa ni kimbilio kwa watu wengi wakidai zina ubora na ni za kijanja zaidi.



Source: Tanzania Today
 
Sijui anafanyaje kuakikisha hizo nguo za ndani ni bacteria free 100%.
 
Aliulizwa kama alishawahi vaa kufuli za mitumba akasema ndiyo lkn hskusema anapendelea.
 
Back
Top Bottom