TANZIA Shamsa Tale, mke wa Meneja wa Diamond Platnumz (Babu Tale) afariki dunia

Tulia wewe! Tuambie ukweli ni upi! BabU tale ana utajiri wa mapaka ama la?!
Kwa hiyo na wewe ndugu zako waliokufa tuseme wewe ndo umewaua au sio??
Au wewe ukifa pia tuseme ni ndugu zako hao wametenda.
Maana kila nafasi itaonja mauti, kwenye kifo hakuna aliye bora kuliko wenzie, haijalishi uwe ni Rais wa Nchi, Mtu Mashuhuri, Masikini, Mtoto etc.
Na kifo hakina kujali umri eti kiseme wewe bado mdogo basi kwa kikuache mpaka uzeeke, hapana!
 
Umeongea ukweli hapa ukiwa mtu wa kufanya shirki sana aiseeh inakua kama mla unga Kila siku unazidi
Kuna uzi Mshana aliandika kuhusu haya mambo. Anasema mambo huwa yanaanza kwenye vitu vya kawaida sana, usije ukaenda kwa mganga ukaambiwa inatakiwa damu ya kuku ukaona kawaida...kuku tu. Dau linakuwa linapanda kadri unavyoendelea na ukishaingia huko kutoka si lelemama
 
Unavyoongea with confidence sounds like wewe ndo mganga mwenyewe utakayemaliza hilo kafara! Yaani wewe likitokea jambo, lazima uhusishe na ushirikina, manake hata Darrasa alivyopata ajali, ulisema hivi:-
Na inaonekana ni MTU anayeamini sana katika shiriki.
 
HEBU FIKIRIA UKO NA SIMANZI/MAJONZI KWA MISIBA INAKUANDAMA AFU UNASIKIA LIDOMO KAYA LIMOJA LINAROPOKA KUWA ETI WEWE "UMEUA NDUGUZO KISA MALI"
HAPO NDO PALE UNAWEZA SHIKA PANGA NA KUMCHARAZA MTU KWA HASIRA UKIMSIKIA ANAROPOKA..
WAAFRIKA WENGI SIE TUNA SHIDA KUUUUBWA KATIKA MINDSET ZETU na ndo maana wazungu walipata urahisi kututawala. imani potofu!! Watu wa hivo si ajabu hata sasa hivi ndo walewale wanaweza kuamini Risasi inageuka maji ( Maji Maji War)
 
Weee huyo achana nae Hawezi kukuelewa, watu tunawajua hadi Askofu wa jimbo akawa n mchawi, na alikuwa na mradi wa madini, baada ya mambo yake kufukunyuliwa leo hii ni kichaa. Aaaaah atasema nn bhan.
Maaskofu huloga ili wapate vyeo vikubwa
 
Maneno hayo huwa mnatoa wapi? Na mimi siku nikiwa maarufu ntatupiwa mzigo wa maneno mengi sana! Yani watu wanataka wakujue sana kuliko wewe unavyojijua.
 
Maaskofu huloga ili wapate vyeo vikubwa
Ndio mie namuelekeza huyo mtu, maana ana waamini hawa watu wa dini, khaaaaaah wakati wao kwa ulozi ndio penyewe, parokia yetu kule home kulikuwa na mapadri 2 huwez amin padri m1 alimroga mwenzie ukichaa, kweny watawa ndio kabisaa shughuri pevuuuh. Khaaaaah
 
Maneno hayo huwa mnatoa wapi? Na mimi siku nikiwa maarufu ntatupiwa mzigo wa maneno mengi sana! Yani watu wanataka wakujue sana kuliko wewe unavyojijua.
Ungemuuliza aliyeyaandika manake anavyojiona utafikiri hatofikwa na matatizo kama haya.

Ila usiogope maneno kwani mwisho wa siku maneno kaumbiwa binadam cha msingi kuwa mpole ,omba Mungu akutie nguvu na Mungu wako atakufariji.
 
Tanzania hii asilimia kubwa wanaamini ushirikina imagine Hadi wauza maandazi
 
Tanzania hii asilimia kubwa wanaamini ushirikina imagine Hadi wauza maandazi
Hadi wauza sambusa na kachori, yote n kwamba uzalishwaji uwe mkubwa na biashara isife. Aaaah
 
Hadi wauza sambusa na kachori, yote n kwamba uzalishwaji uwe mkubwa na biashara isife. Aaaah
Hahaaa hafu wengi wanaloga hafu bidhaa zao hazina quality, poor customer service. Tuna safari ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…