Wanachokifanya Zitto na Fatma Karume ni kitu kisicho na mantiki
Niweke wazi, kwenda kutoa maoni, aina ya maoni ni haki yao na isihojiwe na mtu yoyote
Tatizo ni hili, walitakiwa wajiulize;
Maoni ya Wananchi kupitia tume ya Mzee Warioba yanamatatizo gani?
Kikosi kazi kimeundwa kwa utaratibu gani wa katiba?
Tatu, nani anahakiki maoni yanayotolewa yapo kwenye rekodi?
Kikosi kazi kilisema katiba isubiri.2025. kwa Mujibu wa Prof Lipumba aliyekuwa ndani kama Zitto hayakujadiliwa.
Mwisho wa siku 'uzushi' ukaingizwa katika ripoti na kujenga uhalali, vyama vimesema hadi 2025
Zitto anajua huu ni uharamia kwasababu hakuweza kudhibiti wala kukemea uongo huo.
Fatma anakwenda kujenga uhalali akijua maoni yake hayawezi kuwekwa katika mizani sawa na maoni yaliyotengenezwa tayari yanayotafutiwa majibu
Mwisho Fatma atajikuta analalama kama ambavyo Lipumba analalama lakini bila kufanya lolote
Kuwemo katika kikosi kazi au kutoa maoni katika kikosi kazi ni kujenga ''legitimacy' ya kikozi kazi ambayo ni utapeli tu wakati huo huo waki deligitimize maoni ya Wananchi kupitia Warioba
Nitashangaa sana nitakapomsikia Fatma akizungumzia tena Katiba! yeye keshaungana na wasiotaka kwa kuwajengea uhalali na uwezo wa kuendelea. Fatma , Zitto katika boti moja
Jiulize kwanini Msajili anatoa hiyo picha! kuna hoja hapo itakayotumiwa na Fatma ni sehemu yake
JokaKuu Tindo