mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Mmalawi mwarabu ! Au ??Huyu Mmalawi anashangaza sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmalawi mwarabu ! Au ??Huyu Mmalawi anashangaza sana
Tunasemaga Zimwi likujualo halikuli likakwisha !!Nikiri, uhakika na maneno hayo yamesemwa na Fatma kwasababu sikumsikia
Lakini naamini kwa ukubwa wa suala zima na hadhi yake, asingekaa kimya muda wote huo
Kwa 'dhana tu kwamba amesema' Fatma Karume amefanikiwa sana hasa ukiusoma huu uzi
Fatma amecheza ngoma ya CCM inayopigwa kila uchaguzi ukikaribia
Si Fatma tu , yoyote anayetoa madai yenye hisia za udini ana wajibu wa kueleza, kufafanua au kutetea hoja zake kwa ushahidi na vielelezo, sijui kama Fatma amenukuliwa nusu nusu. sina uhakika
Nina uhakika na kitu kimoja, Fatma ni miongoni wa watu waliopigania Katiba mpya mwanzo kabisa akiwa na kampeni ya '' all white' na Maria Sarungi'. Ni mtu aliyeipinga CCM kwa nguvu za hoja na hata vioja ikibidi. Aliichukia
Tangu Rais SSH aingie madarakani Fatma amezalliwa upya, si yule tena.
Ni ' mkimya na mnyenyekevu'' akiyaona yale aliyokemea sasa ni mazuri. Si Fatma yule, mwiba kwa Magufuli.
Hili linanitia shaka kwamba huenda kayasema hayo maneno ili acheze karata ya kizimkazi. Fatma alikemea Chato
Huenda ni sehemu ya kampeni kuisaidia timu yake ya zamani katika usajili mpya chini ya kocha kizimkazi
Fatma anacheza mirindimo ya Lumumba lakini kwa staili ya ngoma ya msewe! kutoka Zanzibar
Swali linalowavuruga wachambuzi na watambuzi ni hili, ni kipi kimebadilika kutoka JPM hadi SSH?
Tena sasa tuna nyongeza ya Sukari achilia mbali mgao wa mwanga! Fatma kipi kilichobadilika?
JokaKuu Pascal Mayalla
Salum Mwalimu pia kuna walakini..Duh! Pamoja na hayo yote ila bado udini na ukabila unawatesa, especially yule mchungaji wao LEMA, natamani siku moja aingie kwenye 18 za Profesa mazinge
Nawashauri hawa ndugu zangu, Salum mwalim na waislamu wenzetu mliopo huko uchademani nawashauri ondokeni haraka.
Hawa ndugu zetu waislamu baadhi yao huwa siwaelewi kabisa, sijui wapo kimaslahi au ni nini! unajua kabisa changamoto ya chama hicho+udini n.k na bado unang'ang'ana kufanyanao kazi! Muislamu anaejitambua hawezi kufanyanao hao watu.Salum Mwalimu pia kuna walakini..
Na kisha tukishawakataa kama ukoma badala yao tuwape kura zetu akina nani watakaotufaa kuongoza hii Nchi ili tufikie Nchi ya Ahadi ???!!!
Hapo tusi liko wapi!?..umetafuta kichaka Cha kukimbilia!!Mjinga akishindwa anakimbilia matusi. Kwaheri.
Amandla...
Yaya gete nkoi 😅😅🙏Mhala sana nkoi? Wewe ni msukuma, unasapoti chadema?
MtanzaniaHuyu Mmalawi anashangaza sana
Baba MmalawiMtanzania
Kumbe unaelewa👍👍👍❤️Kwakweli, hawa wa huku ni Wanafiki tu
Wale wote waliokuwa wakiishi Tanganyika na Zanzibar kabla ya Uhuru na WATANZANIA.Baba Mmalawi
Ndio maana nikauliza, Shangazi yenu kaanza kuliona lini hili?Swala la CDM na udini ni la siku nyingi,ila kwa kuwa wametoa ushuzi wao imebidi watanzania wenye kukemea watakumbushe kuhusu hii dhambi ya chadema
"Nataka kuwaeleza foot soldiers wa CHADEMA kitu muhimu sana. CHADEMA haiwezi kushinda Urais wa Tanzania bila ya Kura za WAISLAMU na WAKRISTO. Huu mchezo wenu wa UDINI ni double edged sword. Utawakata CCM kwa Wakristo but rest assured utawakata CDM tena SANA Kwa Waislamu. Endeleeni tu!"
====
Fatma Karume akemea UDINI wa CHADEMA na kuvunja ukimya wa muda mrefu kuhusu chama hiki kuhusishwa na mlengo wa kidini.
Kawahakikishia hawatopata kamwe kura za waislam kwa siasa zao za udini.
Naunga mkono hoja, mtu akitoa tuhuma, aweke na ushahidi. Hili la udini Chadema, ni tatizo, angalia mimi nilianza kulizungumza lini na ushauri nikawapa!. CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!Si Fatma tu , yoyote anayetoa madai yenye hisia za udini ana wajibu wa kueleza, kufafanua au kutetea hoja zake kwa ushahidi na vielelezo, sijui kama Fatma amenukuliwa nusu nusu. sina uhakika
Zitto Kabwe alipotaka kugombea UenyekitiWanabodi,!.
Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya udini na nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la udini, ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.
Chadema ina tatizo la udini, ukanda na umimi. Kitendo cha Chadema kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za Bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani peke yake, Chadema peke yenu hamuwezi!. Lazima muwashirikishe wapinzani wengine wote hata kama hawastahili. You have to unite and work as one against a common enemy. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
Pasco
Hivyo tuhuma za udini Chadema zipo na tumeisha shauri sana humuChadema nacho kama chama hakina dini, ila wanachama, wafuasi wake na washabiki wake wote wana dini zao. Kwa hao wadini wa Chadema kwao,nafasi za juu kabisa za uongozi wa Chadema, lazima zishikwe na watu wa dini fulani!, ZZK alipogombea uenyekiti kiliwaka na mwenyewe akanywea!. Uchaguzi unakuja tena na this time tutamchagiza Prof. Safari kugombea Uenyekiti, nashauri subirini muone kitakachotokea!. `Vivyo hizo wako wanaompinga ZZK kwa dini yake, hawa watampinga Mkandara, Watampinga Arfi na Watampinga Prof. Safari kugombea top position yoyote kwa sababu tuu ya dini zao. Hawa wapo, tukubali tukatae!. Dawa yao hawa sio kuwabadilisha, bali kuyalazimisha mabadiliko, ili hayo mabadiliko ndiyo yawabadilishe na huo udini wao uwawashe kama koti la chawa na kujikuta wanalazimika kulivua!.Pasco
Babu inasemekana !Baba Mmalawi
Pasko ni kichwa weweNaunga mkono hoja, mtu akitoa tuhuma, aweke na ushahidi. Hili la udini Chadema, ni tatizo, angalia mimi nilianza kulizungumza lini na ushauri nikawapa!. CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Zitto Kabwe alipotaka kugombea Uenyekiti
wa Chadema alipingwa kwa nguvu zote ndani ya Chadema kwasababu ya dini yake!, mpaka Ba Mkwe Mzee Mtey aliibuka!. Urais wa ZZK 2015 Kupitia Chadema: Kwa nini Wanatetemeka!, Kuweweseka! na Kutishika?!.
Hivyo tuhuma za udini Chadema zipo na tumeisha shauri sana humu
P
Hizo ni dalili za kukiogopa chama cha CHADEMA sasa! Tunatakiwa tushindane nacho kwa hoja zenye tija!CHADEMA hawawezi kupata kura za kundi lolote lile katika jamii lenye akili Timamu na linalojitambua.kwa sababu CHADEMA ni genge na mkusanyiko wa watu wasio na busara wala hekima wala adabu. Ni watu wanaofanya vitu kama vipofu na ndio maana chama kimekosa nuru na muelekeo kwa kuwa kinaongozwa na vipofu ambao akili zao zinawaza madaraka na vyeo tu. CHADEMA wapo tayari kushirikiana hata na shetani ilimradi wapate madaraka. CHADEMA wapo tayari kulipasua Taifa kwa Udini ,ukabila ,ukanda na hata kuchochea machafuko hapa nchini ilimradi wao wapate madaraka na vyeo.
Watanzania tunapaswa kuwapuuza CHADEMA na kuwakemea kabla hawajaharibu Taifa letu. Tuwakatae kwa nguvu zetu zote .kamwe tusiwaunge mkono kwa lolote lile .tuwaogope CHADEMA kama ukoma maana hawana dhamira njema na Taifa letu.