Nikiri, uhakika na maneno hayo yamesemwa na Fatma kwasababu sikumsikia
Lakini naamini kwa ukubwa wa suala zima na hadhi yake, asingekaa kimya muda wote huo
Kwa 'dhana tu kwamba amesema' Fatma Karume amefanikiwa sana hasa ukiusoma huu uzi
Fatma amecheza ngoma ya CCM inayopigwa kila uchaguzi ukikaribia
Si Fatma tu , yoyote anayetoa madai yenye hisia za udini ana wajibu wa kueleza, kufafanua au kutetea hoja zake kwa ushahidi na vielelezo, sijui kama Fatma amenukuliwa nusu nusu. sina uhakika
Nina uhakika na kitu kimoja, Fatma ni miongoni wa watu waliopigania Katiba mpya mwanzo kabisa akiwa na kampeni ya '' all white' na Maria Sarungi'. Ni mtu aliyeipinga CCM kwa nguvu za hoja na hata vioja ikibidi. Aliichukia
Tangu Rais SSH aingie madarakani Fatma amezalliwa upya, si yule tena.
Ni ' mkimya na mnyenyekevu'' akiyaona yale aliyokemea sasa ni mazuri. Si Fatma yule, mwiba kwa Magufuli.
Hili linanitia shaka kwamba huenda kayasema hayo maneno ili acheze karata ya kizimkazi. Fatma alikemea Chato
Huenda ni sehemu ya kampeni kuisaidia timu yake ya zamani katika usajili mpya chini ya kocha kizimkazi
Fatma anacheza mirindimo ya Lumumba lakini kwa staili ya ngoma ya msewe! kutoka Zanzibar
Swali linalowavuruga wachambuzi na watambuzi ni hili, ni kipi kimebadilika kutoka JPM hadi SSH?
Tena sasa tuna nyongeza ya Sukari achilia mbali mgao wa mwanga! Fatma kipi kilichobadilika?
JokaKuu Pascal Mayalla