Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Bank gani ?


Hawakati kati kila mwezi charges zisizoeleweka ?
 
Unasave benki gani..makato yao vipi.?
 
Hongera mkuu kwa uthubutu huo wa kuweka elf 30 per day si kitu kidogo katika hali hii ya vyuma kukaza

(30,000 x 365= 10,950,000 x 5 = 54,750,000)

Je unakumbana na changamoto zipi?
kwa mfanya biashara au mjasiriamali hawezi weka pesa benki miaka mitano bila kutoa, huko ni kukosa akili ya fedha. Pesa inatakiwa izalishwe, hiyo hesabu uliyopiga ww kwa mtu smart ndani ya miaka mitano inatakiwa awe na shilingi 150M hadi 300M.
 
Mimi naweka malengo account ya NBC Kila mwezi nakatwa direct kutoka kwenye mshahara kwa mwaka mzima imenisaidia sana.njia ya vibubu ilinishinda nilikua navunja kabla sijafikisha malengo.
 
Mimi nanunua dhahabu kwa sonara na kuihifadhi na zingine wife na watoto wanazivaa wakihitaji
Ni asset nzuri na thamani haishuki hata siku moja
Unaweza kupeleka bank kama kuna access hiyo kwa huko
Hehehe sasa dhahabu ya hereni nayo utaiita ni dhahabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…