Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Mimi napata 250,000 kwa mwezi. Mwanzoni nilikuwa natumia kwanza afu ikibak ndo nasave unakuta mda mwngne hamna hela ya maana uliyosave. Nikabadilisha njia. Nikawa nikipata tu hela naweka 100,000 kamili bank alaf hyo 150 inayobak ndo nafanya matumizi. Namshukuru MUNGU na kipato changu kidg nimekaa mwaka na zaidi sasa nina akiba ya 1.2m
Hyo ndo njia ninayoitumia na sitoiacha. Naombea niongeze kipato ili kuongeza akiba yangu.
Bank gani ?


Hawakati kati kila mwezi charges zisizoeleweka ?
 
Mimi na trace matumizi yangu na ninachoingiza kwa kutumia app ya monefy ambayo ipo playstore. Hii app inakufanya ujue kiasi ulichotumia kwenye chakula, malazi, gari, starehe n.k kila baada ya mwezi.

Kisha natunza bank kwenye akaunti ya saving kile kiasi nilichopanga. Hii ni hatua ya pili ya kusevu.

Mwisho Nasevu hicho kiasi kwenye kununua kiwanja, kufanya ujenzi wa jengo, kununua shamba, kupanda miti kwenye shamba n.k

Halafu ole wake mtu aje na sera zake za kimasikini miaka 3 ijayo ntakapokuwa naenda likizo ulaya na familia yangu.
Unasave benki gani..makato yao vipi.?
 
Hongera mkuu kwa uthubutu huo wa kuweka elf 30 per day si kitu kidogo katika hali hii ya vyuma kukaza

(30,000 x 365= 10,950,000 x 5 = 54,750,000)

Je unakumbana na changamoto zipi?
kwa mfanya biashara au mjasiriamali hawezi weka pesa benki miaka mitano bila kutoa, huko ni kukosa akili ya fedha. Pesa inatakiwa izalishwe, hiyo hesabu uliyopiga ww kwa mtu smart ndani ya miaka mitano inatakiwa awe na shilingi 150M hadi 300M.
 
9319010a382dd0c8398784b6ce13cf60.jpg
 
Mimi naweka malengo account ya NBC Kila mwezi nakatwa direct kutoka kwenye mshahara kwa mwaka mzima imenisaidia sana.njia ya vibubu ilinishinda nilikua navunja kabla sijafikisha malengo.
 
Mimi nanunua dhahabu kwa sonara na kuihifadhi na zingine wife na watoto wanazivaa wakihitaji
Ni asset nzuri na thamani haishuki hata siku moja
Unaweza kupeleka bank kama kuna access hiyo kwa huko
Hehehe sasa dhahabu ya hereni nayo utaiita ni dhahabu.
 
Back
Top Bottom