Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Siku hizi nmeanzisha bajeti yangu ya kila mwezi na najitahidi nsitoke nje ya kile nlichopanga kukitumia
 
Coz kuweka tuu hela kwenye kibubu ni bora ukaweka benk saving account ambapo mwisho wa mwezi unapata faida yko
 
Mwenye Enzi Mungu akupe haja ya moyo wako!
Well done!
 
Mkuu hebu jazia nyama kdg hapo, mkopo kiasi gani kwa riba ya 10% na muda wake wa mrejesho ni upi? Nipo kwenye kampuni moja hv ila hakuna hii system nimehamasika kuwashauri wenzangu tuanzishe haka ka utaratibu ndani ya kampuni yetu! Maelezo kdg mkuu......
 
Hongera mkuu kwa uthubutu huo wa kuweka elf 30 per day si kitu kidogo katika hali hii ya vyuma kukaza

(30,000 x 365= 10,950,000 x 5 = 54,750,000)

Je unakumbana na changamoto zipi?
Siyo Mchezo Kweli Kujiongeza Muhimu
 
Hivi hawa M- PAWA ukiweka akiba wanatoa kweli % ya ulicho weka? Mwisho wa mwezi
Natumia m-pawa kukopa na Kuweka akiba.Ila sijui kama Kuna chochote wanaongoza.Tatizo ni kunifungia kukopa mpk nimechoka.
 

Mkuu salama,

nimesoma bandiko lako na nimeelewa kama ifuatavyo;

Kwanza wewe ni lazima muajiliwa so unajaribu kushauri wengine pia katika level uliopo.

Pili nataka nikuchalleges kama unafanya saving ili ununue gari au nyumba unakua sahihi lakini you will never be reach(hauwezi toboa kwa kusave).

Njia sahihi ya kujikomboa kumaisha, kwanza futa hizo mentality za kusave and instead anza kufikilia kubuld businesses(you can start small) kwa hyo hyo pesa unayosave(remember savers are loosers).

Jaribu kufatilia watu wote matajiri wanaokuzunguka kwa haraka uliza au jiulize wametoboa kwa kusave au kwa kufanya biashara...Ukipata majibu utaungana na mimi 100%.

I wish you best of luck hope nimeeleweka!

[HASHTAG]#stoppoormentally[/HASHTAG]!!!
 
Sio salama pia, bank ikizingua utaambulia mil. 1.5 tu.
Itanzinguaje mkuu wakati kibubu ulikuwa unakaa nacho mwenyewe? Na ukifika benki wanakukabidhi ufunguo unatoa mpunga wako unajiondokea!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…