Shareholder mkubwa wa NMB ameondoka – Rabobank Nederland

Kuna mdau amesema Rabobank wametransfer hizo share kwa fund yao ambayo inaitwa Arise.. lakini nnavoona hii move itaipa nguvu serikali kwenye decision making maana hiyo Arise atakuwa ni fund tu ya kusimamia investment za Rabobank ila Rabobank hatakuwa tena na influence NMB...
 
Moja ya changamoto kubwa tulionayo sisi watanzania ni tabia ya kutokufuatilia ukweli wa mambo kabla ya kuandika chochote

Kuhusu shares za Rabobank of the Netherlands kwenye benki ya NMB, ambapo Rabobank wanamiliki 34.9% ya shares zote za NMB Plc( Majority shareholder)

Mwaka 2017 kule jijini Cape Town nchini South Africa, taasisi tatu za kifedha za Rabobank of the Netherlands kutoka Uholanzi, Dutch Development Bank ( FMO) kutoka Uholanzi na Norwegian state owned development fund( Norfund), ziliamua kuingia ushirikiano kwa kuunda kampuni moja ya kiuwekezaji itakayokuwa inasimamia uwekezaji wotewa taasisi hizo tatu, kusini wa jangwa la Sahara ikiwemo na nchi yetu ya Tanzania,( Sub Saharan Africa focused Investment Company)kampuni hiyo mpya ya kiuwekezaji inajulikana kama Arise

Kwa hiyo kunachofanyika sasa ni ku transfer shares za NMB zinazomilikiwa na Rabobank of the Netherlands kwenda kwenye kampuni hiyo mpya ya kiuwekezaji ya Arise

Kwa hiyo kimsingi bado Rabobank wataendelea kumiliki shares za NMB kupitia Arise

Kwa hiyo hakuna capital outflow yeyote itakayotokea ndani ya nchi yetu kwa hatua hiyo, kwa mantiki hiyo hakutakuwa na Economic impact yeyotekwenye uchumi wa nchi yetu kwa hatua hiyo ya Rabobank of the Netherlands

Rabobank of the Netherlands wamefikia hatua hiyo ikiwa ni lengo la kuongeza ufanisi kwenye kusimamia rasilimali zao zilizipo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo na uwekezaji wao hapa nchini Tanzania
 
Sasa cha ajabu utakuta taasisi za serikali zinazuiwa kufanya biashara na hata bank hii

Yaani kila kitu BOT wakati hata hii bank na CRDB ni benk za umma..

Hatujui kabisa huu upumbavu unavyoumiza uchumi
Hamna sera mbovu kama hiyo ya kurudisha pesa BOT.. halafu sahivi hiyo sera wameibadilisha kimya kimya.. kuna taasisi za serikali wamerudi tena kufanya banking na commercial banks.

Sema serikali haitaki kukiri udhaifu
 
Sad, tulipaswa kujenga kwenda mbele na sio kubomoa na kujenga upya [emoji35]
 
Hapana, sio "toka kuvunjika kwa jumuia ya East Africa"

Ni toka zamani hata enzi za ukoloni uchumi wa Tanganyika ulikuwa chini, kwa sababu sisi hatukuwa "a settler colony".

Na sio kweli kwamba ni sababu ya mitumba kuvaliwa hadi ulaya ndio iliyosababisha Kenya wavae mitumba. Matatizo ya viwanda vya nguo kutozalisha nguo za kutosha ndio sababu..., na hii sio kwao tu, bali hata kwetu na kwingineko, hata huko ulaya.

Sasa kama ukame ndio uliosababisha wale 'yanga', kwani sisi ukame haukutuathiri? Lakini mara zote sisi hugeuka na kulaumu Nyerere tu kwa kila tatizo tulilopata, kana kwamba sisi tulikuwa na dunia yetu peke yetu.
 
Nahisi kitu kama hicho ukiangalia yule CEO wao mzungu mmama naskia kuna fitna fulani ilifanywa.
 


Ukweli tutaona mengi sana, ndiyo maana hakuna ajira mitaani, yani watu wanatoka kwenye uwekezaji sisi tukitegemea kuwa wawekezaji waongezeke lakini imekua tofauti,

Kuna vile vikao vya mkuu na wafanyabishara pamoja na wawekezaji, hivi huwa zile hoja na malalamiko hufanyiwa kazi? au ni udhaifu uliopo kwa wawekezaji wanaofika kwenye vikao hivyo kushindwa kuwakilisha mambo yanayo wakwamisha
 
Still bado kuna impact maana hiyo fund Arise haiwezi kuwa na knowledge ya banking kama Rabobank.

Fund ni kama mlinzi tu hawezi tena aka play sehemu kubwa ya maamuzi ya benki which means decision making zitabaki kwa serikali kupitia hazina ambaye ni mwekezaji mkubwa wa pili
 
Pia mkuu akutane na wafanyabishara wadogo na wakati ndiyo naona kero nyingi ziko huku chini, na ni kero zinazo athiri kila jambo katika kila sekta na ni eneo muhimu sana kiuchumi, kero nyingi naona zipo katika eneo hili.

Kwa hili haiwapi vishawishi wawekezaji wakubwa
 

Nimetoa mfano wa kuanzia kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika mashariki, maana ndio hasa viongozi wetu wa kiafrika ilikuwa sahihi kuwapima.

Nijuavyo sio lazima kila nchi ijitosheleze kwa bidhaa fulani, bali nazungumzia kuvaa viraka kutokana na mwenendo mbaya wa maamuzi ya kimamlaka. Kenya walivaa mitumba kutokana na nguvu ya soko, na nakisi ya nguo. Ila sisi ilikuwa ni kukosa kabisa kutokana na misimamo ya kiutawala.

Kwenye maelezo yangu ya awali sikuwa nimetaja kula unga wa Yanga, hilo ulilitaja ww. Najua vizuri tofauti ya uwepo wa unga wa Yanga, na nguo za mitumba.
 
marking scheme ya ubongo wa watu dizain yako ninayo
 
Moja ya changamoto kubwa tulionayo sisi watanzania ni tabia ya kutokufuatilia ukweli wa mambo kabla ya kuandika chochote
Tufuatilie vipi mkuu 'Ngamanya Kitangalala'?

Habari kama hii ingetolewa zamani sana katika vyombo vyetu vya habari, tungeshindwa kuifahamu?
Bila shaka sehemu sahihi ya kuelekeza lawama kama hiyo uliyoigusia ni huko kwenye vyombo vya habari, na kama na wao hawatoi habari kama hizi kwa sababu maalum, basi na wao wangelalamikia hicho kinachowazuia.
Nchi yetu imebadilika sana katika hii miaka ya karibuni. Imekuwa kama sisi ndio tumeingia kwenye zile tawala za "Eastern Block" za miaka ile ambapo kila habari ni kama siri kubwa. Waandishi wa habari wenyewe, hata uandishi wao umeathirika kwa sehemu kubwa sana. Ni nadra sana siku hizi kufungua gazeti na kusoma 'a feture article' toka kwa mwandishi na kutoka na hamu ya kutafuta makala zake nyingine.
 
Serikali inaweza kuwa inataka kuzirejesha benki zake, NMB+NBC, makaburu bado wanaweza kufungua benki yao na kujenga mtando kadri wanavyotaka, siyo kujimwambafy kwenye benki ambayo ilikuwa imeshaanzishwa na serikali.
 
Sijui huo "mwenendo mbaya wa kiamaamuzi" unaoulenga.
Hapa tulikuwa na viwanda vya nguo kutosheleza kabisa mahitaji yetu ya ndani; vyote havikufua dafu kwa sababu ya huo ukame uliouzungumzia na hali mbaya ya kiuchumi iliyoikumba dunia hadi hata huko ambako walidharau kuvaa mitumba ikawalazimu kuzivaa. Siyo kweli kuwa hilo lilikuwa ni tokeo la bahati tu la "nguvu ya soko."
 
Ni vyema kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kabla ya kutoa taarifa kama hii ili usiwe sehemu ya upotoshaji.
Weka cha kwako unachojua. Yeye kama mdau wa soko la mitaji ametoa speculation, na speculation ndiyo brain ya biashara kwenye stock exchange. Kila tukio la kijamii, kisiasa na uchumi lina athari kwenye bei na soko la hisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…