‘Shark loans’ namna taasisi za fedha za nchi tajiri wanavyowalewesha mikopo nchi maskini na kuweka mazingira ya kufubaza uchumi

‘Shark loans’ namna taasisi za fedha za nchi tajiri wanavyowalewesha mikopo nchi maskini na kuweka mazingira ya kufubaza uchumi

Sio kwa serikali tuu mfumo wa mikopo uko sawa hata kwa mtu binafsi. Lazima kuna muda wa kuwajibika
 
Biashara ya kutoa mikopo ni biashara kama biashara nyingine. Unavyouza mikopo Zaidi ndivyo unavyopata faida Zaidi.

Kwa nchi zilizoendelea kama Marekani, mataifa ya Ulaya, Japan, na hata China, hizi ni nchi ambazo zimefanikiwa kuwa na efficiency kubwa sana kwenye mabenki, na pia benki kuu katika nchi hizo kwa ndani ya miaka 15 iliyopita, walikuwa na sera ambazo zilipelekea interest rates (au kiwango cha riba) kwenye hizo nchi, kuwa chini sana.

Matokeo yake ni kwamba, benki, investors na wakopeshaji wengi sana wa hizi nchi tajiri, wamekuwa ni kama wana struggle kwenye kutengeneza faida ndani ya masoko yao, hususani kwasababu, cost of funds ni ndogo lakini pia lending costs ni ndogo, kwahiyo wamekuwa wakitengeneza ‘a very thin margin’ kwenye mikopo ndani ya nchi zao, kitu ambacho kwa investors huwa hakifurahishi.

Kwahiyo trick ikawa ni kwamba, hizi nchi tajiri ikabidi wa dizaini namna ya kuwabambika mikopo nchi maskini the likes of Zambia, Tanzania, Kenya nk. Kwasababu kama nilivosema kwenye utangulizi wangu, biashara ya mikopo, ni kama biashara nyingine, unavyouza mikopo zaidi ndo unavyozidi kutengeneza pesa zaidi.

Na kwa kutumia taasisi hizo hizo zao kwenye assessment ya credit ratings, imejikuta kwamba kumejengeka mfumo wa kuhakikisha kwamba risk profile ya mataifa mengi maskini inakuwa juu sana, ili basi hata riba ya mikopo ambayo watapewa pia itakuwa ni kubwa.

Mikopo inayofubaza uchumi – mikopo isiyoelekezwa kwenye matumizi yenye tija

Kikubwa ni kwamba, hizi taasisi za kifedha za nchi tajiri, wanataka kuhakisha kwamba, mikopo mingi ambayo nchi masikini watakopa, basi isiweze kulipika daima, ili kwamba iwe ni kama vile Ng’ombe unayemkamua maziwa kila siku.

Kwa hivo basi, nchi maskini zimekuwa zikijikuta zina finance miradi ambayo ‘payoff’ yake ni ndogo iki maanisha kwamba, mradi husika unaweza kuwa na impact ndogo kwenye uchumi kitu ambacho kitapelekea kukosekana kwa cash flow ya kulipa hiyo mikopo husika.

Lakini ni kama pia kuna agenda ambayo huwa inajificha kwenye hii mikopo ya kimataifa. Ni kwanini mikopo ambayo huwa inalenga mambo ya kipuuzi huwa inakuwa inatolewa haraka haraka sana? Na ile ambayo ina maslahi mapana nay a muda mrefu huwa inapigwa danadana?

Ukijijibu hayo maswali vizuri, utakuja kuona kwamba, hizi taasisi huwa hazina malengo ya kuona kwamba uchumi wa hizi nchi unaboreka, ndio maana kuna mikopo serikali inapata kwa haraka haraka na ukiangalia matumizi yake unaona ni matumizi ya kipumbavu kabisa.

Zaidi zaidi nadhani hii ni aina mpya ya ukoloni mamboleo kwa kutumia taasisi za kifedha za kimataifa kuhakikisha kwamba wanawalewesha na kufubaza maendeleo ya hizi nchi kupitia mikopo ya kinyonyaji, kwasababu ni mikopo isiyolipika, yenye riba kubwa, na ambayo inabeba systemic risks za kuangusha hata mfumo mzima wa uchumi wa nchi husika – ukiangalia kinachowakuta Ghana kwa sasahivi.

Inavoonekana ni kwamba pia Tanzania, hatuwezi kujikwepa na huu mtego, tayari tupo kwenye ile debt trap, maana kwa miaka saba iliyopita nchi imeongeza deni kwa karibu USD 12 billion (TZS 27 Trillioni) ambazo mimi binafsi ukiniuliza zilipokwenda, bado ntachelea kukupa majibu.

External debt stock as per BOT

December 2015 – USD 15,408 millions

October 2022 – USD 27,482 millions

Changes between Dec 2015 to Oct 2022 = USD 12,074 millions

Watu wengi wanasema ‘Tanzania bado haipo kwenye high risk category na deni ni stahimilivu kwa just kuangalia tu upande wa debt to GDP ratio’ lakini ukiangalia kwenye upande wa ‘cash flow’ iliyopo ambayo ni kodi na tozo za kila uchao na projected cash flow ya hivi vilivyoombewa mikopo ambayo mimi naona bado ni dhaifu, huwezi kuona huo ustahimilivu ulipo.

Nawaachia swali serikali, ‘pesa unayokopa unaifanyia nini?’ hilo swali nadhani ndio tungependa kuskia bunge likijadili kabla ya serikali kwenda kukopa, vinginevyo naona hizi deal zinafanyika kimya kimya na wizara ya fedha, naona kila kukicha kwa miaka 7 iliyopita wapo busy kila siku wakisaini mikataba ya kukopeshwa mabilioni lakini hawataki kutujibu hilo swali, wanafanyia nini mikopo? Je unakopa ulipe mishahara? Je unakopa ili ulipe madeni?

Ni hayo tu.

N.Mushi
Jilaumuni wenyewe kwa kuchagua na kuvumilia mafisi kwenye ofisi za umma. Kwanini watawala wetu wasikatae? Watakataaje wakati hawana sera wala uwezo wa kuendeleza watu wao zaidi ya matumbo yao na nyumba ndogo? Nasi kama mafala, hatuwatii kashkash wakatimka na kujaribu wengine.
 
Na hiyo ndo trick part ya hii mikopo.. sasa kinachotokea ni kwamba ... hizi currency zetu hazipo stable.. matokeo yake ukitaka kulipa marejesho ya mkopo ambayo yapo kwenye currency ya dola, na wewe hauna reserve ya dola, itakubidi utafute namna ufanye devaluation of currency ili uvutie dola nyingi kwenye uchumi ili uweze kulipa mkopo.. matokeo yake inapelekea mfumuko wa bei na pesa yako inapoteza thamani

Angalia currency ya Ghana na kinachowakuta sasahivi
Hatuna nchi nyingine, ndo nchi yetu hii.

Ila kwa hii trick ya mikopo wazungu wamejua kutuweza.
 
Mikopo na misaada ambayo serikali za magharibi wanatoa haraka ni mambo ya Ku empower wanawake,kutetea haki sawa,kupigana na ukimwi,haki za binadamu,na mambo kibao ambayo hayana impact ya moja kwa moja kwenye uchumi..
Fedha nyingi inakwenda katika vitu ambavyo sio tangible, huwezi ukaona impact yake na hata impact ikiwepo huwa sio ya muda mrefu

Matokeo yake, believe me misaada hii katika Mambo haya huwa n chanzo kikubwa cha kuongezeka katika vitendo vya rushwa serekalin na katika mashirika yasio ya kiserekali.
 
Mikopo na misaada ambayo serikali za magharibi wanatoa haraka ni mambo ya Ku empower wanawake,kutetea haki sawa,kupigana na ukimwi,haki za binadamu,na mambo kibao ambayo hayana impact ya moja kwa moja kwenye uchumi..
[emoji1787] ukipewa mkopo ukajidai sijui kununua mashine ya utafiti mafuta au madini umekwisha. Na ajabu Viongozi wetu kwakua wanalamba asali mtajuwa wenyewe watanzania. Bado safari ni ndefu.
 
Wanajua sana.ila uthubutu hawawezi. Yule marehemu aliweza japo mambo mengine aliharibu ila kwenye sera ya uchumi alikua anakwenda vizuri.
Umeongea ukweli,sio kwamba hawaju,wana maarifa,elimu,exposure KUBWA kutuzidi sisi tunao waona hawajui,wanatucheka huku wanakula keki ya Taifa...wao ndio wanufaika wanatatizo gani???shida haziwakuti wao wala familia zao,hizi zetu kama kelele za chura ,,wacha wakope
 
Umeongea ukweli,sio kwamba hawaju,wana maarifa,elimu,exposure KUBWA kutuzidi sisi tunao waona hawajui,wanatucheka huku wanakula keki ya Taifa...wao ndio wanufaika wanatatizo gani???shida haziwakuti wao wala familia zao,hizi zetu kama kelele za chura ,,wacha wakope
Usisikitike watanzania wenye uchungu na hii nchi wapo ila wananyimwa nafasi wasionekane lakini waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha....
 
Anytime.

Nakubaliana na wewe sana. Nimeanza kusoma tu "A Game As Old As Empire". Kinaanza tu na mi data ya kufa mtu kuonesha how the game is stacked against us, halafu nikiangalia tulivyokuwa addicted na mikopo, naona kabisa "this is a train wreck waiting to happen".

Ukisoma "Confessions of An Economic Hitman" unaona kabisa tunapitishwa mulemule.
Kiranga umefungua sana ufahamu wangu kwa hivi vitabu unavyo attach humu.
Nimesoma hivyo vitabu dah shukrani mkuu bila wewe nisingejua kama kuna madini ya namna hii. Kuna kile "philosophy of religion: an anthology" ni kizuri sana.
Angalau akili zinafunguka sasa. Naendelea kukufuatilia.

Thanks bro.
 
Kiranga umefungua sana ufahamu wangu kwa hivi vitabu unavyo attach humu.
Nimesoma hivyo vitabu dah shukrani mkuu bila wewe nisingejua kama kuna madini ya namna hii. Kuna kile "philosophy of religion: an anthology" ni kizuri sana.
Angalau akili zinafunguka sasa. Naendelea kukufuatilia.

Thanks bro.
Anytime bro.

Haya mambo ni muhimu sana kujua.
 
Back
Top Bottom