TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

ndani ya wiki moja wasanii watatu tena wa maigizo wametangulia mbele za haki inasikitisha sana, ila kaz ya mola haina makosa, msalimie kanumba sharo
 
Wana Jf,

Kuna habari za kusikitisha na uhakika kuwa msanii aliyekuwa maarufu kwa jina la Sharo Millionea, msanii wa muziki na maarufu katika kuwepo kwake katika matangazo kwa style ya aina yake amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Tanga.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.



attachment.php

Nitaamin kadri muda uendavyo nt nw,
 
mie mwenyewe nimeipata hii habari facebook nikadhani utani, kumbe jamaa alikuwa anasema ukweli, alale pema sharo.lolo mbona vijana wanaondoka mapema hivi..........au mambo ya freemason as wasemavyo?????
 
Habari nilizozipata hivi sasa wandugu zimenishtua sana. Zinasema kuwa msanii maarufu wa maigizo Sharo millionea mzee wa swagga, umebugi men, AMEFARIKI DUNIA kwa ajari ya gari usiku huu huko Muheza Tanga. Naandika thread hii na tangazo lake la Airtel linapita. Innalillahi wainnailayhi r- aajiun. Tumepoteza jembe lingine.

Source: Channel 5

Channel 5 saa ngapi mi nipo naangalia Top Ten za Western mbona sijaona?
 
ndani ya wiki moja wasanii watatu tena wa maigizo wametangulia mbele za haki inasikitisha sana, ila kaz ya mola haina makosa, msalimie kanumba sharo

1.Mlopelo
2.Big John
3.Sharo Millionea

R.I.P
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo...
 
Du! Kama ni kweli Mungu amrehemu amlaze mahala pema peponi amina.siku zote vizuri havidumu.
 
No men! Nani atanichekesha Bongo! Nilishapata replacement ya Max, sasa nayo imenipotea!

Mungu mkubwa, hesabu zake sio kama za binadamu.
 
Utakumbukwa kwa uwezo wako mkubwa kisanaa, R.I.P Sharo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
......kama ni kweli tasnia ya maigizo kwa upande wa vichekesho imeondokewa na mtu muhimu sana. natamani isiwe habari ya kweli.
 
Ajari ya gari iliyohusisha gari alilikuwa akisafiria msanii maarufu kama Shalo bilionea imepelekea msanii huyu kuaga dunia. Baada ya gari yake ndogo kupinduka akiwa safarini mkoani Tanga, alipoteza maisha hapohapo na kwamba maiti yake imehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya Muheza. ajari hiyo imetokea majira ya saa mbili usiku huu. Kazi yake Mola haina makosa na Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu msanii Shalo
 
Back
Top Bottom